PDA

View Full Version : Breaking News: Vituo vya Mafuta vyagoma



mwanakijiji
01-12-2009, 06:00 PM
Habari zinazoingia ni kuwa vituo vya mafuta jijini Dar vingi vimeacha kutoa mafuta kwa kisingizio kuwa hakuna mafuta. Hata hivyo inaonekana uamuzi huo umechukuliwa katika kukaidi agizo la kushusha bei ya mafuta nchini.

Mambo kama haya yalitokea miaka ya themanini na kuanzisha ile operesheni maarufu ya Wahujumu Uchumi. Je yawezekana serikali kuthubutu kutumia sheria ile tena?

Foleni ya Mafuta (PIcha toka Michuzi)

http://www.mwanakijiji.com/images/resized/mafuta1.jpg

http://www.mwanakijiji.com/images/resized/mafuta2.jpg

http://www.mwanakijiji.com/images/resized/mafuta3.jpg

Dua
01-13-2009, 12:50 AM
Urais una hadhi yake na wakati aliyepewa dhamana na wananchi wa kuongoza anapokwenda kukinga bakuli kila jioni kwa Patel matokeo yake ndio hayo. Je, tunahitaji another revolution? Watanzania tukiengelea kuchagua sura, na wababaishaji kama JK hivi sasa ndoto ya maisha bora kwa kila Mtanzania itaendelea kuotwa kama kwenye vitabu vya Abunuwasi.

Wapo wengine ambao wanafaidika isivyo halali na Serikali ya JK na tayari wanaashiria ushindi wa kimbunga 2010, sitashangaa kesho JK atawapa miezi sita wajirekebishe na adha yote hii itabaki kuwa hadithi na kila mfanyabiashara ya mafuta atasema huyu ndiye rais. Hatujasahau miezi sita aliyowapa wauza unga, na wiki mbili mbili alizokuwa amemuamrisha askari kanzu wake ambaye anataka kurudi madarakani. JK tunafahanu mbinu zako!

Akajase
01-13-2009, 07:59 AM
Mkuu,sasa chuma kinashikamoto sijui ni nani ataweza kukikamata. Tusubiri.
Hawa, jamaa wameanza kugoma ikiwa ni siku ya mapumziko na wakati wakuu wengi wako visiwa vya karafuu.
Kama Dar hali ndiyo hivyo,sijui huko Kagera,Kigoma,Tabora,Rukwa,Songea na Lindi itakuwaje.
Tulipiga kelele kipindi ambacho yule mama ZHM alipokuwa pale fedha kwa kuwatishia 'wakubwa" hawa nyau bila matendo.
Mh! Ari mpya tuliiona,NGUvu mpya tuliiona sasa tuangalie KAsi mpya itakavyokuwa (ANGUKA)

bulesi
01-13-2009, 08:34 AM
Ukaidi wa hawa wauza mafuta lazima una sababu, haiwezekani amri ya serikali inayoheshimika ikadharauliwa na wafanyabiashara hivi hivi. Ni wazi wanajua hao viongozi wetu ni wadau katika biashara zao na ndio maana wanatutesa sisi walalahoi. Serikali ni lazima iwaonyeshe kuwa nchi hii ina utawala wa sheria ama sivyo tutasambaratika.