PDA

View Full Version : Inawezekana kuwa mauaji ya albino yalianza zamani?

hofstede
01-12-2009, 06:23 PM
Ninakumbuka zamani kulikuwa na uvumi kuwa, albino hawafi, yaani wanaishi ukifikia muda wao hutoweshwa na kwenda kusikojulikana. Ilifikia mpaka watu wakawa wanabishana kuwa ni nani aliwahi kuhudhuria mazishi ya albino?. Kwa kweli hakuna mtu aliyekuwa na jibu na wote niliowafahamu walisema hawajawahi. Kutokana na kuzuka kwa mauji ya albino kwa kasi hivi sasa mtu anaweza kufikiria kuwa huenda mauaji haya hayakuanza leo ni mambo yaliyokuwepo tangu zama kwa imani hizo hizo za kishirikina na wahenga wakaamua kuleta dhana hiyo ili kuficha yaliyokuwa yanajili gizani kuhusu hawa ndugu zetu.

My take: Kutokana na kuongezeka kwa watu na hali ya uchumi huenda kuna waliojaribu kuona kuwa demand imekuwa kubwa na hivyo kuanza vitendo vya ukatili vya hawa ndugu zetu albino kwa uwazi. Na kama uvumi huo ungekuwa ni kweli kuwa Albino hutoweka basi leo hii nafikiri tusingeshuhudia mauji ya kinyama ya hawa ndugu zetu, nafikri hili suala tuliangalie kwa upana zaidi, kuwa kwa nini zamani watu waliaminishwa kuwa albino hawafi? hutoweka?

mwanakijiji
01-12-2009, 06:34 PM

nadhani hili linahitaji mwangalizo zaidi, nadhani huko nyuma maalbino walikuwa wanakufa vifo vya kawaida kama sisi wengine na hakuna aliyekuwa anatilia maanani hasa "wanakufaje". Hata kama wangekuta kwa mwaka mmoja albino anauawa haikuwa rahisi kuhusisha hilo na imani za kishirikina.

Pia tukumbuke kuwa katika jamii nyingine (za kiafrika na hata za magharibi) Maalbino mara nyinge wamekuwa wakihusisha na mambo ya maajabu ya Mungu au mizimu na wamekuwa wakihusishwa na baraka na mikosi.

Mimi hofu yangu zaidi iko kwenye serial killers. Wazo hili la serial killers bado hatujalipatia vizuri nchini.