PDA

View Full Version : Serikali kuwachukulia hatua wafanyabiashara wa mafuta

mwanakijiji
01-13-2009, 09:39 AM
Vyanzo mbalimbali vinadokeza kuwa serikali itachukua hatua dhidi ya wamiliki wa vituo mbalimbali vya mafuta ambavyo jana viliamua kusitisha huduma ya kuuza mafuta. Hatua hizo hatujui kwa wakati huu ni zipi lakini kuna dalili kuwa Waziri Ngeleja anaweza kutangaza hatua nzito. Hata hivyo kuna baadhi ya watendaji ambao wanataka serikali isiwe wakali sana wasije ku "escalate" hali iliyopo sasa na kusababisha mgomo wa mafuta kwa nchi nzima.

hofstede
01-13-2009, 01:40 PM

Hapo nilipo bold Mkjj naona haingii akilini. Tukianza kuwaogopa hawa jamaa kuwa watagoma maana yake ni kwamba serikali imeshindwa kazi. Kama wameweza kuwafutia uzamini wanafunzi 2000 wa UDSM na wengine 4000 hawajui hatima yao basi ni dhahiri kuwa serikali ni chombo chenye uwezo na hakipaswi kufanya kazi kwa kuogopa kundi fulani la watu bali ni kwa maslahi ya wananchi walioiweka madarakani tu.

Kuna wakati madaktari waligoma serikali ikasema itaagiza wengine kutoka nje na kuwafukuza wote waliogoma, nafikiri na hawa wauza mafuta pia wengi hii ni kazi inayowaweka mjini sasa serikali inapaswa kutoa tamko kuwa kwa yeyote atakayegoma anawekwa kwenye black list ya kutofanya biashara yoyote ya nishati hapa Tanzania na watu wengine wanapewa nafasi hiyo, hao watendaji wanaopinga hatua kali ni wamiliki wa vituo na hawafanyi kazi kwa niaba ya wananchi bali ni kwa niaba ya hawa mabepari(kuna conlict of interest hapo). Umefika wakati wa watendaji wote kupigwa marufuku kuwa na hisa katika makampuni binafsi, Baba wa Taifa aliona mbali sana katika hili.

mwanakijiji
01-13-2009, 06:57 PM

Malima amesema kuwa serikali haiko tayari kufanya kazi kwa "kushikiwa kisu shingoni"..

hofstede
01-13-2009, 10:10 PM
Malima amesema kuwa serikali haiko tayari kufanya kazi kwa "kushikiwa kisu shingoni"..

Wakikimbia kisu sasa hivi basi tusione 2010 wakileta shingo zao. Tatizo la kuchaguana kwa kulipa fadhila huku, mtu anapewa nafasi ili ale sio atoe huduma. Angekuja huku kwa watu wanaoogopa public justice asingetoa kauli kama hizo unashikiwa bango ubwage manyanga, ngoma huiwezi wewe.

mwanakijiji
01-13-2009, 11:18 PM
Nimezungumza na Mhe. Malima leo na nadhani kesho (Jumattano) watakuwa katika mazingira mazuri ya kujua nini kinaendelea. Kinachofanyika sasa hivi ni kutoa mafuta kwenye meli mbili hadi saa sita hizi za usiku halafu usiku huu kusambaza kwenye vituo mbalimbali kisha asubuhi waone hali ikoje.

Ach-F
01-13-2009, 11:53 PM
Nchi inawekwa rehani tena na wafanya biashara uchwara ambao hata kodi hawalipi? Maajabu ya Mussa haya.