View Full Version : Breaking News: Mmiliki wa Richmond afikishwa mahakamani kwa kufoji!
mwanakijiji
01-13-2009, 04:36 PM
Mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Richmond Development ambayo iliwahi kuingia mkataba na Tanesco wa kuleta majenera ya umeme amefikishwa mahakamani. Bw. Gire ni mmoja wa ndugu karibu saba waishio eneo la Houston ambao wamekuwa wakijishughulisha na biasharra mbalimbali hasa ya kuchapa vijitabu n.k
Bw. Gire ni mmoja wa wandugu waliobakia Tanzania wakifanya shughuli mbalimbali pia za kibiashara. Mkataba wa Richmond ambao haukufuatwa taratibu zinazofaa ambazo baada ya uchunguzi wa Kamati Teule ya Bunge ulitakiwa kuvunjwa.
Kashfa ya Richmond kama ilivyokuja kujulikana ndiyo ilisababisha mwaka jana mwezi wa Pili, kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe. Edward Lowassa na kusababisha Baraza la Mawaziri kuvunjwa.
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/criminalcase.jpg
Habari nzuri hiyo...wasiwasahau Lowasa na wenzake.
Sheria Msumeno!
Gire ni mmoja wa ndugu karibu saba waishio eneo la Houston ambao wamekuwa wakijishughulisha na biasharra mbalimbali hasa ya kuchapa vijitabu n.k
kutoka kwenye vitabu mpaka kwenye umeme ama kweli kuna watu wanajua kucheza na akili za watu
mwanakijiji
01-14-2009, 09:39 PM
Gire ni mmoja wa ndugu karibu saba waishio eneo la Houston ambao wamekuwa wakijishughulisha na biasharra mbalimbali hasa ya kuchapa vijitabu n.k
kutoka kwenye vitabu mpaka kwenye umeme ama kweli kuna watu wanajua kucheza na akili za watu
wenyewe wanasema ujanja kupata..
kurutamatata
01-15-2009, 03:50 PM
This is yet another of Plenty of Free Ride for unsuspecting Danganyikans! Playing Cats and Mouse! Whatever the Outcome, one thing for sure NI kwamba Serikali IMEUMBUKA KUPITILIZA!Sasa watanzania wametambua fika kwamba usifikiri kila king'aacho ni dhahabu! Mbaya wetu siyo mtu wa Nje.Bali KIKULACHO KI NGUONI MWAKO.Hawa wasingepata mwenyeji wao wa kuwakaribisha yote hayo yasingetendeka na yasingewezekana.Hakimu NYANI kesi ya NGEDERE! MASHAHIDI SIJUI KINA NANI? Mahindi yatapona kweli shambani?
kurutamatata
01-15-2009, 03:57 PM
Jamaa kanitonya hapa kwamba Hakimu NYANI kesi ya NGEDERE, eti Mashahidi watakuwa kina KENGE WATUPU! Rufaa atasikiliza NANI?
Jamaa kanitonya hapa kwamba Hakimu NYANI kesi ya NGEDERE, eti Mashahidi watakuwa kina KENGE WATUPU! Rufaa atasikiliza NANI?
Karutamatata sijakuelewa unamaanisha nini? hebu tufafanulie tafadhali
wenyewe wanasema ujanja kupata..
na watakuwa wamepata sana tu kwa style yao ya briefcase office, but this time wamepatikana {kama serikali yetu haitufanyii mazingaombwe}
Jamaa kanitonya hapa kwamba Hakimu NYANI kesi ya NGEDERE, eti Mashahidi watakuwa kina KENGE WATUPU! Rufaa atasikiliza NANI?
Tuseme na hao mahakimu ni Mafisadi? Au wanahusika vipi na kashfa ya Richmond?
mwanakijiji
01-15-2009, 09:28 PM
Baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana (mwananchi)
Nora Damian
http://mwananchi.co.tz/image/%5Crichimond.jpg
MFANYABIASHARA Naeem Adam Gire, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kughushi na kutoa taarifa za uongo kwamba kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini, amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Gire alirudishwa rumande jana majira ya saa 7:00 mchana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, yaliyomtaka awe na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya Sh100 milioni au mali isiyohamishika yenye thamani inayolingana na kiasi hicho cha pesa kila mmoja.
Masharti mengine ya dhamana ni kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kuripoti polisi mara moja kwa mwezi.
Gire alipandishwa kizimbani juzi mbele ya Hakimu Mkazi Wariyalwande Lema wa Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashitaka matano.
Mshitakiwa huyo anadaiwa kuwa Machi 13, 2006 akiwa jijini Dar es Salaam, alighushi nyaraka akionyesha kwamba, Mohamed Gire ambaye ni mwenyekiti wa Richmond Development Company LLC ya Texas nchini Marekani, alisaini kumruhusu kufanya shughuli za kampuni hiyo hapa nchini.
Pia anadaiwa kuwa Machi 20 mwaka 2006 katika eneo la Ubungo umeme, alitoa hati za uongo ambazo zilionyesha kwamba, Mohamed Gire amezisaini kumuidhinisha yeye kufanya shughuli za kampuni hiyo nchini.
Mshitakiwa huyo pia anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwa, Kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini Tanzania.
Inadaiwa kuwa mshitakiwa huyo alitoa taarifa hizo, ili wajumbe wa bodi hiyo waweze kuipendekeza Kampuni ya Richmond kufanya kazi hiyo.
Katika shitaka la nne Gire anadaiwa kuwa mwezi Juni mwaka 2006, alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa Timu ya Majadiliano ya Serikali kwamba, Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme ili wajumbe hao waweze kuipendekeza.
Na katika shitaka la tano, mshitakiwa huyo anadaiwa kuwa Juni 2006 alitoa nyaraka za kughushi zinazoonyesha kwamba, Mohamed Gire amezisaini kumuidhinisha mshitakiwa kufanya shughuli za kampuni hiyo Tanzania.Kesi hiyo itaendelea leo katika mahakama hiyo.
Wakati huo huo, upelelezi wa kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania inayowakabili, Johnson Lukaza na Mwesiga Lukaza umekamilika.
Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya alieleza hayo jana mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Euphamia Mingi.
Hata hivyo Hakimu Mingi aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 27 mwaka huu washitakiwa watakaposomewa maelezo ya awali.
Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya mwezi Desemba 2003 na Desemba 2005 waliiba katika Benki Kuu kiasi cha Sh6,300,402,224.64.
Pia wanadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kupitia kampuni ya Kernel Ltd ya Tanzania, baada ya kudanganya kuwa kampuni hiyo imerithishwa deni na Kampuni ya Marubeni Corporation ya nchini Japan.
Wakati huo huo, kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini, Jayantkumar Chandubhai Patel (Jeetu Patel) na wenzake imeahirishwa hadi Februari 13, mwaka huu itakapotajwa tena.
Kesi hiyo iliahirishwa baada ya Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya, kudai mahakamani hapo kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Jeetu Patel na wenzake, Amit Nandy na Devendra Patel wanadaiwa kuwa mwaka 2005 waliiba Sh10,562,922,828.60 kutoka BoT, kupitia Kampuni ya Bencon International Ltd baada ya kudanganya kuwa wamerithishwa deni na Kampuni ya Marubeni Corporation.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.