View Full Version : Nini kitangulie kati ya Hamas na Israel?
mwanakijiji
01-13-2009, 11:46 PM
Katika kutafuta utulivu huko mashariki ya kati pande mbili zinazopigana yaani Hamas na Israel kila moja inatoa sharti moja kubwa ili mapigano yakome.
Hamas wanasema hadi Israel iondoke maeneo inayokalia ya Gaza ndiyo kusimamisha mapigano (truce) kunaweza kutokea.
Israel wao wanasema hadi Hamas ikubali kutorusha makombora yake kuelekea Israel ndipo wako tayari kuzungumzia suala la utulivu na amani.
Unafikiri hizi pande mbili zinaweza kweli kukubaliana?
outlier
01-14-2009, 03:51 AM
Hapo hakuna suluhu mpaka mmoja aji-sacrifice. Namaanisha vipiganwe mpaka Gaza iwe totally under control ya Israel ama Israel ikubali kuondoka rockets zikiendelea kuvurumishwa. Binadamu hatupendani kabisa, sijui tutaishia wapi! Tusubiri WW III nyuklia zirushwe tuangamie wote.
Nziku
01-14-2009, 01:48 PM
Hapa ni pagumu sana, Israel haioni raha kuwapiga Wapalestina ila Hamas inaona raha kuwapiga Israel. Kwa mantiki hiyo, Hamas wakiacha kurusha makombora wala hakutakuwa na vita tena. Israel wangependa sana kuishi kwa amani ndo maana wamechukua msimamo mkali wa kujilinda ambao umefikia hatua ya kutowaamini Wapalestina na kuwanyima baadhi ya haki zao kama vile kuingiza silaha.
Hata hivyo katika suala la truce bado kunamasuala mawili ambayo hawajakubaliana.
1) Israel wanataka kuwe na kikosi cha kudumu cha jeshi la umoja wa mataifa ili kulinda na kuangalia mchokozi.
2) Israel wanataka mipaka ya gaza na Misri ifungwe ili Hamas wasiendelee kuingiza silaha kupitia eneo hilo.
Hoja hizi zote zimekataliwa na Hamas. Pia tukumbuke kwamba moja ya malengo ya kuanzishwa kwa Hamas ni kuiondoa Israel duniani, you see, so hawawezi kukubali mpango wowote wa kudumu wa kuleta amani.
outlier
01-14-2009, 03:05 PM

Usiusemee moyo- JD
kurutamatata
01-15-2009, 02:30 PM
Taifa ambalo litaweza kusuluhisha mgogoro baina ya Wapalestina na Waisraeli kwa ukamilifu kabisa ni Wamisri au Nchi ya Egypt.Zipo sababu nyingi kwa nini Egypt wanazo kila sifa za kuweza kusuluhisha mzozo huo ambao umesababisha vifo vya wapalestina wengi sana wasio na hatia yoyote,hususan watoto na wanawake.Wamisri, Wapalestina na Wayahudi au Wana wa Israel wana Historia ya pamoja kwa kipindi cha muda mrefu sana toka enzi za maandiko matakatifu ya Biblia.Enzi hizo za Biblia ya mwanzo ungeweza kusema kwamba mataifa hayo matatu tofauti hivi leo nyakati hizo lilikuwa taifa moja tu.Lakini kutokana na sababu za kihistoria mataifa hayo matatu yamejikuta yakigawanyika katika makundi makubwa matatu! Wayahudi wamejikuta wakizama zaidi katika Jumuia ya Ulaya(western civilisation) japo wapo Mashariki ya Kati.Wapalestina nao wamejikuta wakizama zaidi katika Jumuia ya Waarabu, wenyeji wa Mashariki ya Kati. Wamisri wao wapo katika mjumuiko wa Waafrika kwa upande mmoja na Waarabu kwa upande mwingineo.Kwa ujumla utasema mzozo uliopo sasa baina ya waisraeli na wapalestina ni baina ya waarabu na wayahudi wenye tamaduni tofauti na imani za kidini tofauti japo Mungu wao ni yuleyule mmoja. Israeli ni nchi ndogo sana iliyozungukwa na nchi nyingi za Kiarabu.Waisraeli ndiyo wenye tatizo la uhaba au ukosefu wa ardhi ya kutosha LAKINI wapalestina wao wangeweza kabisa kuishi katika baadhi ya maeneo yanayokaliwa na Waarabu wenzao kwa hivi sasa.Na ndiyo maana nikasema kwamba Egypt inao uwezo mkubwa sana wa kuwapatanisha hawa mahasimu wakubwa lakini ni ndugu wa damu, wapalestina na wayahudi.Hebu utazamwe uwezekano wa Egypt kuitoa ardhi yake ya Sinai Peninsula, wapalestina wakaruhusiwa kuishi na kuweka makazi yao hapo pia ili kupunguza msongamano uliopo sasa katika Ukanda wa Gaza.Egypt iondoe mpaka wake wa Sinai na kuruhusu wapalestina wahamie katika ukanda huo.Wapalestina watakao penda kuendelea kuishi ndani ya Israel basi wakubali kufuata taratibu na sheria za serikali ya Israeli bila masharti yeyote.Ardhi inayo kaliwa na Waarabu katika Mashariki ya Kati ni Kubwa Mno na haijatumika kikamilifu au kuzidiwa na idadi ya watu kwa sasa.Lakini Wayahudi, taifa dogo katika ardhi ndgo sana pia na wao wapewe haki ya kuishi katika ardhi yao ya asili bila ya uhai wao kuhatarishwa na taifa lingine lolote.Ni suala la kutumia busara tu.Vinginevyo uhasama huo hautakwisha kabisa na uwezekano uliopo ni kwamba wapalestina wataipoteza hata hiyo fursa iliyopo sasa kwa wao kuweza kupewa ardhi ya kutosha na wao waishi salama bila ya uhasama wowote kutoka kwa ndugu zao wa Kiyahudi.Mimi nigepewa uwezo huo ningethubutu kuwasuluhisha wapalestina na wayahudi hadi maafikiano yapatikane.Katika hilo, nchi zinginezo za Kiarabu ina wajibu na Mchango mkubwa katika kuhakikisha kwamba Mzozo huo ama unamalizika kabisa kwa manufaaa ya pande zote mbili au Mapambano hayo hayatokwisha milele na milele, na ama Wapalestina watapoteza kabisa ardhi yao au Wayahudi watapoteza kabisa ardhi yao na Ulimwengu utafika pabaya.
outlier
01-15-2009, 05:03 PM
Taifa ambalo litaweza kusuluhisha mgogoro baina ya Wapalestina na Waisraeli kwa ukamilifu kabisa ni Wamisri au Nchi ya Egypt.
Sidhani kama uko sahihi; huo mgogoro unaweza kutulizwa na MAREKANI, ndiyo nchi yenye influence kubwa zaidi duniani- na hasa Israel.
Ardhi inayo kaliwa na Waarabu katika Mashariki ya Kati ni Kubwa Mno na haijatumika kikamilifu au kuzidiwa na idadi ya watu kwa sasa. Tatizo sio ardhi tu kama ardhi, ni 'specific ardhi'- JERUSALEM. Wote wanautaka huo mji.
Soma historia na jiografia ya eneo lile utapata mwanga zaidi na utafurahi mwenywe.
Taifa ambalo litaweza kusuluhisha mgogoro baina ya Wapalestina na Waisraeli kwa ukamilifu kabisa ni Wamisri au Nchi ya Egypt.Zipo sababu nyingi kwa nini Egypt wanazo kila sifa za kuweza kusuluhisha mzozo huo ambao umesababisha vifo vya wapalestina wengi sana wasio na hatia yoyote,hususan watoto na wanawake.Wamisri, Wapalestina na Wayahudi au Wana wa Israel wana Historia ya pamoja kwa kipindi cha muda mrefu sana toka enzi za maandiko matakatifu ya Biblia.Enzi hizo za Biblia ya mwanzo ungeweza kusema kwamba mataifa hayo matatu tofauti hivi leo nyakati hizo lilikuwa taifa moja tu.Lakini kutokana na sababu za kihistoria mataifa hayo matatu yamejikuta yakigawanyika katika makundi makubwa matatu! Wayahudi wamejikuta wakizama zaidi katika Jumuia ya Ulaya(western civilisation) japo wapo Mashariki ya Kati.Wapalestina nao wamejikuta wakizama zaidi katika Jumuia ya Waarabu, wenyeji wa Mashariki ya Kati. Wamisri wao wapo katika mjumuiko wa Waafrika kwa upande mmoja na Waarabu kwa upande mwingineo.Kwa ujumla utasema mzozo uliopo sasa baina ya waisraeli na wapalestina ni baina ya waarabu na wayahudi wenye tamaduni tofauti na imani za kidini tofauti japo Mungu wao ni yuleyule mmoja. Israeli ni nchi ndogo sana iliyozungukwa na nchi nyingi za Kiarabu.Waisraeli ndiyo wenye tatizo la uhaba au ukosefu wa ardhi ya kutosha LAKINI wapalestina wao wangeweza kabisa kuishi katika baadhi ya maeneo yanayokaliwa na Waarabu wenzao kwa hivi sasa.Na ndiyo maana nikasema kwamba Egypt inao uwezo mkubwa sana wa kuwapatanisha hawa mahasimu wakubwa lakini ni ndugu wa damu, wapalestina na wayahudi.Hebu utazamwe uwezekano wa Egypt kuitoa ardhi yake ya Sinai Peninsula, wapalestina wakaruhusiwa kuishi na kuweka makazi yao hapo pia ili kupunguza msongamano uliopo sasa katika Ukanda wa Gaza.Egypt iondoe mpaka wake wa Sinai na kuruhusu wapalestina wahamie katika ukanda huo.Wapalestina watakao penda kuendelea kuishi ndani ya Israel basi wakubali kufuata taratibu na sheria za serikali ya Israeli bila masharti yeyote.Ardhi inayo kaliwa na Waarabu katika Mashariki ya Kati ni Kubwa Mno na haijatumika kikamilifu au kuzidiwa na idadi ya watu kwa sasa.Lakini Wayahudi, taifa dogo katika ardhi ndgo sana pia na wao wapewe haki ya kuishi katika ardhi yao ya asili bila ya uhai wao kuhatarishwa na taifa lingine lolote.Ni suala la kutumia busara tu.Vinginevyo uhasama huo hautakwisha kabisa na uwezekano uliopo ni kwamba wapalestina wataipoteza hata hiyo fursa iliyopo sasa kwa wao kuweza kupewa ardhi ya kutosha na wao waishi salama bila ya uhasama wowote kutoka kwa ndugu zao wa Kiyahudi.Mimi nigepewa uwezo huo ningethubutu kuwasuluhisha wapalestina na wayahudi hadi maafikiano yapatikane.Katika hilo, nchi zinginezo za Kiarabu ina wajibu na Mchango mkubwa katika kuhakikisha kwamba Mzozo huo ama unamalizika kabisa kwa manufaaa ya pande zote mbili au Mapambano hayo hayatokwisha milele na milele, na ama Wapalestina watapoteza kabisa ardhi yao au Wayahudi watapoteza kabisa ardhi yao na Ulimwengu utafika pabaya.
kurutamatata samahani uwe una press inter kila baada ya mistari miwili unatupa tabu sisi wenye matatizo ya macho kukusoma vizuri
[/QUOTEUnafikiri hizi pande mbili zinaweza kweli kukubaliana?[/QUOTE
kitendawili cha Hamas na Israel ni kigumu sana na hakuna mtu anaeweza kukitegua zaidi ya wao wenyewe, na bahati mbaya ni kuwa hawa wote ni mafahari hawawezi kuishi zizi moja.
Kinachosikitisha ni kuwa hakuna upande unaojali mauaji ya raia unaoendelea si Hamas wala Israel
a2faces
01-26-2009, 04:02 PM
Hakuna jambo lisilo na mwisho, uwe mzuri au mbaya lakini nina ushauri kwa ndugu zetu wapalestina, vita ni vita, huwa havichagui..........kabla hawajaamua kuingia vitani wanawajibika kutengeneza mazingira ya usalama kwa raia wao kwanza badala ya kutegemea huruma za kimataifa, tunajua kuwa wanapouawa wanawake na watoto na raia wengine wasio na hatia kimsingi HAMAS wanapata ushindi wa propaganda kutokana na mauaji hayo kupitia habari na picha zinazoonyeshwa na vyombo vya habari lakini wajue kuwa hata jumuia za kimataifa zikipiga kelele hazitasaidia kitu kwani ISRAEL ni mwenzao kwa namna moja ama nyingine. Nawashauri HAMAS kujipanga kwanza kabla hawajakaribisha namna yoyote ya vita au mashambulizi toka ISRAEL. Kwani haoni mlingano wa tathmini ya hasara inayopatikana mara kwa mara baada ya vita kati yao na ISRAEL? Huo siyo ushujaa, wanawajibika katika kuwalinda raia wao kwanza......
Japhet
02-06-2009, 08:38 PM
Vita ya Hamas na Israel naifananisha na ugonmvi uliokuwepo kati yangu (Israel) na madogo wangu (Hamas) wakati wa utoto wetu. Nilikuwa mpole sana lakini mdogo wangu alikuwa mchokozi na mgonvi sana. Angenipiga bila sababu, lakini as long as ningevumilia vipigo vyake, walikuwa wanakaaa kimya. Kama ingetokea kwamba niekasirika na kumzaba kibao kimoja tu, angepiga mayowe na wazazi wangeingilia kati, eti kwa nini unampiga mtoto??????
So, Hamas wakirusha Makombora kwa Waisrael, dunia nzima hukaa kimya. Israel akijibu mapigo walu kwa siku moja tu. Utasikia kelele kutoka kila pande duniani.
Nionavyo mimi, Hamas wanawajibika kwa vifo vya Wapelestina (hasa wakina mama na watotot) kwani wanatumia wapestina kama ngao yao.
Kibaya zaidi, Viongozi wa Hamas na famila zao hawako Gaza, wako nchi nyingine salama kabisa.
Hitimisho: Hamas waache kurusha maombora kwenye ardhi ya Israel, hatutakaa tusikie mapigano.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.