PDA

View Full Version : KLHN Exclusive: Mahojiano na Mhe. Sofia Simba

mwanakijiji
01-14-2009, 07:01 AM
http://mwanakijiji.podomatic.com/mymedia/thumb/13384/460%3E_1507880.jpg

Mojawapo ya chaguzi ambazo zimekuwa na mvuto wa muda mrefu ndani ya CCM ni ule uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita ambapo Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (T) alipatikana.

Mshindi huyo si mwingine bali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Sofia Simba. Safari ya ushindi wake ilikuwa ni safari ambayo wachache wako tayari kuipitia. Ilikuwa ni safari ambayo unapofika mwisho inabidi ujiuliza ulianzaje safari hiyo.

Hivyo KLHN ilipata nafasi ya kuzungumza naye kwa kirefu kuhusu ushindi wake huo na hasa kutupa mwanga kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea kati yake na mpinzani wake katika uchaguzi Mhe. Janeti Kahama.

Pamoja na hayo tumemuuliza maswali ya kutaka kujua kama kweli Rais Kikwete ndiye aliyemtaka agombee na kama ni kweli hotuba ya Rais Kikwete kwenye ufunguzi wa uchaguzi ilikuwa ni ya kumpa mkono wa baraka ili achaguliwe. Pamoja na hayo tulitaka kujua zaidi kuhusu UWCCM utakuwaje chini ya uongozi wake?

Kwa maoni au mawazo tuandikie mhariri@klhnews.com

BONYEZA HAPA KUSIKILIZA (http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/2009-01-13T19_47_49-08_00)

QUTE
01-14-2009, 03:28 PM

Mwanakijiji huyu mama nimemsikiliza nimesikitika sana. Yaani Tanzania tuna aina ya viongozi kama hawa, kweli sasa nimepata jawabu kuwa kwa nini miaka 47 ya UHURU bado hatuna maendeleo.

Mimi ninaona kuwa sasa umefika wakati wa kutangaza nafasi za mawaziri kwenye vyombo vya habari na kuhojiwa na PwC au hata KPMG kabla ya rais kuteua.

Hivi kweli waziri wa wizara nyeti anafanya interview kama mtoto wa darasa la saba anahojiwa kujiunga na form one. Hawa ndiyo type ya viongozi wetu ooooh no, tubadilike sasa haya majibu ya huyu waziri yalikuwa chini ya kiwango cha cheo anachokishikiria, tuache kubebana jamani, tufikirie nchi, kuwa na kinamama wengi kwenye baraza la mawaziri ambao most of them ni type hii ni kudidimiza nchi. Hivi huyu anaweza hata kubuni kitu kweli zaidi ya kusubiri taarifa na kusign cheque tu. Haya hii ndiyo Tanzania yetu, tupo 2009 lakini tuna viongozi wenye mtazamo wa 1961,

mwanakijiji
01-14-2009, 06:53 PM

mbona umekuwa mkali hivyo.. sasa ungesikiliza mahojiano yote uncut na unedited si ndiyo ingekuwa vurugu? Unachosikiliza that is the best cut!