View Full Version : Hii Deci Deci, Deci ni ponzi scheme?
mwanakijiji
01-14-2009, 06:21 PM
najaribu kufanya utafiki ili niandike kwa kina kitu ninachokijua kuhusu hii Deci kampuni/ngo ambayo inaonekana kuwatajirisha watu bila kufanya biashara yeyote ile.
a. Wako wapi?
b. Viongozi wao ni nani?
c. Wanafanya biashara gani ya kuzalisha pesa?
d. Walifungua biashara hiyo kwa mtaji gani?
mwanakijiji
01-15-2009, 10:12 PM
1: Kijiji kina watu 10000
2. Watu wa 10 wa kwanza wasio na fedha wanaanzisha mradi wa DECI.
Wanasema kujiunga nao ni Shs. 200,000
Watu 1000 wanajiunga kwa kutoa Tsh200,000 kila mmoja. (Kijiji kinabakia na watu 8990.
Kwa kiyo Mtaji wa kwanza ni: Tsh. 200,000,000 (za wale watu 10)
Hawa wanaambiwa wasubiri miezi minne ili “wavune” faida.
3. Wanatangaza na watu wengine 1500 wanajiunga kijiji kinabakiwa na watu 7490
Watu wale 1500 wanaleta mtaji mpya wa milioni 300,000,000
Miezi minne inapopita wale 1000 wa kwanza wanalipwa fedha yao milioni 200, na kila mmoja anapata “faida” ya laki moja moja hivyo kila aliyeingia na laki mbili miezi minne anatoka na laki tatu!
4. Wanaingia watu wengi zaidi sasa nao wanafikia 2000 nao wanataka haya mavuno! Kijiji kinabakiwa na watu 5490 ambao sio wanachama.
5. Wale watu 2000 wanaingia na mtaji wa 400,000,000.
Sasa hapa ndipo kuna kitu cha kuangalia vizuri
a. kuna watu 1500 ambao wanatakiwa kulipwa laki mbili zao (kwa jumla ya milioni 300 za mbegu). Lakini pia wanatajia kupata kila mmoja laki moja zaidi kama faida.
b. Hivyo pamoja na kiasi hicho unatakiwa mradi wa milioni 150 zaidi kama faida ya kundi lile la pili.
c. Kiasi hicho kinatolewa kwa wale waliokuwa na milioni 400 na hivyo kufanya wale wanaoingia na milioni mia nne kimsingi kuwa wamekingia na milioni 250! (hilo si tatizo kwa sasa).
d. So wale wa kundi la pili wanaondoka na wao na laki tatu tatu kwa furaha ya “mvunaji”
6. Hivyo kampuni yetu inaanzisha recruitment drive nyingine na watu wengine 3000 wanajiunga na kampuni yetu hii ya mavuno. Kijiji kinabakiwa na 2490 ambao wengi wao wanaonekana kuwa ni wanachama wa JF!! Hao nao wanaingia na mtaji wa 600,000,000!
7. Hivyo muda umefika wa kuwalipa walioingia na milioni 400! So wale milioni mia nne kwanza wanalipwa “seed money yao) ambayo ni kiasi hicho hicho. Lakini wanataka faida yao ya laki moja moja kila mmoja.
- Hivyo zinahitajika milioni 200 nyingine na hivyo kuchukua kabisa mtaji wa wale wa milioni 600, kuwalipa wao na hivyo wale wa milioni 600.
So wale wa milioni mia nne wanaondoka kwa furaha kwani wamepata fedha yao.
8 Wale wa milioni mia sita (ambao ni wengi zaidi – 3000) na wenyewe wanaambiwa wasubiri fedha zao hadi mwisho wa miezi minna.
9. Sasa recruitment inaenda na kuwashawishi wale 2490 waliosalia kijijini kujiunga ili “wavune. Nao wanaingia na mtaji wa 498000! (mara moja tunaona kuwa wanaingia na kiasi pungufu.
Kampuni yetu ifanye nini basi;
10. Kampuni inawashawishi wale waliokwisha pewa mavuno yao kuzizungusha fedha hizo hizo tena kwenye mfumo huo. Kwa hiyo wale wa 1000, na wale 1500 na wanatakiwa kuzungusha fedha zao humo kwa humo.
NOW THIS HOW THE SYSTEM COLLAPSES:
SCENARIO ONE:
a. Baada ya wale 2490 kuingia na kulipa milioni 498 wale wa milioni 600 watajikuta wanapungukiwa Sh 102! Bila ya fedha kuzungushwa tena kundi la milioni 600 wataanza kulalamika.
b. Wakati hao wanaanza kulalamika kundi lile la 2490 linasubiri kiasi walichoingia nacho (kwa maana angalau waliokwishalipwa awali idadi kama yao wawe wamzungusha tena fedha). Na pia wanasubiri milioni 249 kama faida! (kwa maana ya kwamba wanahitajika watu wengine kama 50 hivi kujiunga kuweza kuzalisha hiyo faida.
SCENARIO TWO:
a. Hii inategemea idadi ya watu ambao wako tayari kuzungusha fedha zao ndani kwa ndani. Kinachofanyika hapa ni saikolojia ya fedha. Wakikupa laki moja faida na wakakuambia uziingize tena kwenye system itabadi urudishe laki mbili kwao tena, na wewe unabakiwa na laki moja! Katika mfano halisi wa DECI ni kwamba wanakulipa laki tatu, na unaweza kuzirudisha kwa mafungu laki mbili mbili, hivyo utarudisha kwao zile za kwako (laki mbili) za kwao (laki mbili) na wewe unabakia na laki moja! Ulichofurahia kimsingi ni wewe kuwa na “laki tatu” kwa muda fulani, siyo kuzitumia.
b. Hili hata hivyo linatabia ya kuchosha huwezi kuwa na fedha usiyoitumia! Hivyo collapse ya pili itatokea pale watu ambao wamekuwa wakizungusha fedha zao huko kwenye kampuni watakapoamua kuziondoa kwenye mzunguko! Kwa maneno mengine wale 1000, na wale 2000 na wale wa 3000 watakapoamua kuondoka na fedha zao wale wa mwisho 2490 watajikuta wameliwa karibu milioni 500!
Akajase
01-16-2009, 01:40 PM
Mkuu mkjj, nimekupata vizuri. lakini pia naomba kujua.
1.Je kunauwezekano wa DECI kuja kuwaingiza watanzania katka mkenge kama ule wa UPATU?
2.Je kunauwezekano wa kuja kuishitaki DECI ikiwa watu watalizwa pesa zao kwa minajili ya kurudishiwa?
mwanakijiji
01-16-2009, 04:41 PM
sidhani kama hii scheme iki collapse kuna mtu atarudishiwa kitu chochote kile..
Akajase
01-16-2009, 06:03 PM
Sasa mkuu,tuwaweke kundi gani hawa watendaji wa serikali yetu ambao ni wachumi na mabwana/mabibi fedha waliopo pale hazina na vikosi vya upelelezi, ambao wanaliona hili likitendeka, wanajua madhara yake yatakayotokea lakini wao wapo kimya ofisini wanasubiri kuandikiwa barua watu wakiisha lizwa?
Nina mashaka na jambo moja nalo kwa DECI kutojitangaza waziwazi. kuna mTz mwezangu aliniambia "Wao DECI hawajitangazi wala hawataki kujitangaza kwa sababu wapo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi".Kumbe kuna mkakati wa kuwaliza watu.
Kama pana mtu anawafahamu vizuri hawa DECI tunaomba mchango wako.
mwanakijiji
01-16-2009, 06:12 PM
Sasa mkuu,tuwaweke kundi gani hawa watendaji wa serikali yetu ambao ni wachumi na mabwana/mabibi fedha waliopo pale hazina na vikosi vya upelelezi, ambao wanaliona hili likitendeka, wanajua madhara yake yatakayotokea lakini wao wapo kimya ofisini wanasubiri kuandikiwa barua watu wakiisha lizwa?
Nina mashaka na jambo moja nalo kwa DECI kutojitangaza waziwazi. kuna mTz mwezangu aliniambia "Wao DECI hawajitangazi wala hawataki kujitangaza kwa sababu wapo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi".Kumbe kuna mkakati wa kuwaliza watu.
Kama pana mtu anawafahamu vizuri hawa DECI tunaomba mchango wako.
mimi nadhani siwezi kushangazwa watakapoanza kulia serikali ikiunda tume kuchunguza suala hili. Na hapo litauma sana pale vigogo wengine nao watakapoonekana walikuwemo humo humo!! Itakuwa ni kashfa ya DECI!!
Yale yale ya upatu yatajirudia muda si mrefu, sijui kwa nini sisi watanzania ni wepesi wa kusahau haraka. na watakaokuja kuumia zaidi ni wafanyabiashara ndogo ndogo ambao sasa wamesimamisha biashara zao na kufungua biashara mpya ya deci
Ach-F
01-18-2009, 09:52 PM
Warning Guys!
That's known as pyramid scheme. Very few people get rich, the ones who run this idiotic scheme. It has made a lot of people more poor. It operated in South Africa, Zimbabwe, Germany and UK. In actual fact its a criminal offence in UK and if caught you end up in Jail.
Unaweza google au nenda wikipedia na search Pyramid scheme.
Pyramid schemes exploit greed and gullibility. A successful pyramid scheme combines a fake yet seemingly credible business with a simple-to-understand yet sophisticated-sounding money-making formula. The essential idea is that the mark, Mr. X, makes only one payment. To start earning, Mr. X has to recruit others like him who will also make one payment each. Mr. X gets paid out of receipts from those new recruits. They then go on to recruit others. As each new recruit makes a payment, Mr. X gets a cut. He is thus promised exponential benefits as the ''business'' expands.
Such ''businesses'' seldom involve sales of real products or services to which a money value might be easily attached. However, sometimes the ''payment'' itself may be a non-cash valuable. To enhance credibility, most such scams are well equipped with fake referrals, testimonials, and information. Clearly, the flaw is that there is no end benefit. The money simply travels up the chain. Only the originator (sometimes called the "pharaoh") and a very few at the top levels of the pyramid make significant amounts of money. The amounts dwindle steeply down the pyramid slopes. Of course, the worst off are at the bottom of the pyramid: those who subscribed to the plan, but were not able to recruit any followers themselves.
Some network or multi-level marketing businesses, which sell real products and rely on the price differentials between the manufacturer's dispatch ramp and the retail counter, may verge on the borderline between ''smart'' and ''scam''. When a pyramid does involve a real product, such as Holiday Magic cosmetics in the United States in the 1970s, new "dealers" who've paid enrolling fees are encouraged, in addition to selling their products, to become "managers" and recruit more new "dealers" who will also pay enrolling fees. As the number of layers of the pyramid increases, new recruits find it harder and harder to sell the product because there are so many competing salesmen. Those near or at the top of the pyramid make a lot of money on their percentage of the enrolling fees and on commissions for the supplied products, but those at the bottom are left with inventories of products they can't sell. However, most multi-level marketing businesses are not pyramid schemes.
Pyramid schemes are not to be confused with Ponzi schemes, named after Charles Ponzi, which also rely on greed and gullibility but are quite different. In a Ponzi scheme, all new money is paid to "Mr. Ponzi" for investment in his incredibly profitable business and he distributes a portion of it to other members as "interest" or "investment income" whereas in a pyramid, money is paid to the next level upward in the pyramid.
http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/4c/Pyramid_scheme.svg/350px-Pyramid_scheme.svg.png
Ach-F
01-18-2009, 10:11 PM
A pyramid scheme is a non-sustainable business model that involves the exchange of money primarily for enrolling other people into the scheme, often without any product or service being delivered.
Pyramid schemes are illegal in many countries, including the United States[1], the United Kingdom, France, Germany, Canada, Romania[2], Colombia[3], Malaysia, Norway, Bulgaria, Australia[4], New Zealand[5], Japan[6], Nepal[citation needed], Philippines[7], South Africa[8], Sri Lanka[9], Thailand[10], Iran[citation needed], and the People's Republic of China[11]. These types of schemes have existed for at least a century.
Mod if possible stick this for people to see.
mwanakijiji
04-05-2009, 06:25 AM
Police probe DECI as BoT disowns schemes
By Mkinga Mkinga and Florence Mugarula
Police are said to be investigating the Development Entrepreneurship for Community Initiative (Deci) for operating an illegal funds management scheme.
This comes as the central bank issued a statement on Wednesday warning the public not to invest their money in the company.
Enthusiastic investors kept thronging the company's Mabibo offices in Dar es Salaam this week to deposit their money despite warnings the scheme was illegal and risky.
Deci, run by the Jesus Christ Deliverance Church, is understood to be promising investors 300 per cent interests within a period of between three and 12 months.
Local bankers have said the company is running an illegal pyramid scheme and cautioned depositors against risky investments.
The Bank of Tanzania (BoT) and Capital Market and Securities Authority (CMSA) issued a joint statement Wednesday evening saying the scheme was illegal.
A police official speaking anonymously told The Citizen yesterday the company was now under investigations for the illegal scheme.
The probe team comprises officers from the Criminal Investigations Department, Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) and state intelligence, he said.
It emerged this week that a Kenyan company with a similar name to the revolving fund scheme that has wooed thousands of investors in Tanzania collapsed last December with Ksh600 million (over Sh10 billion) of investors� savings.
The Kenyan government is also said to be currently investigating the defunct company, which is called the Development Entrepreneurship for Community Initiative (Deci) Kenya Limited.
It is not yet clear whether the two are sister companies. Deci Tanzania officials have not confirmed any links with the Kenyan scheme.
Thousands of defiant Tanzanian investors have reportedly deposited billions of shillings into the company as bankers express concern it could collapse with investors' deposits.
Deci's 37 branches countrywide have become a popular spot for low-income earners and local business owners.
At its Mabibo headquarters in Dar es Salaam, the company is said to be receiving deposits from an estimated 3,000 people per day.
Deci officials last week told The Citizen that they had paid back Sh35 billion in profits and registered more than 500,000 members since last year when their activities picked up.
While the police yesterday remained tight-lipped on the said probe a source who spoke to The Citizen said some investigators had asked CMSA to confirm whether or not Deci was operating an illegal business.
In the joint statement, BoT governor Prof Benno Ndulu and CMSA chief executive officer Fratern Mboya said the company was not registered to operate the scheme.
They denied ever issuing Deci a licence to run a funds scheme and said the firm was involved in an illegal pyramid scheme that collapsed once in the country and in Kenya.
"It should be noted that, the promotion and participation in any pyramid schemes is an offence in terms of the provisions of the Penal Code,� part of the statement read.
The statement confirmed there is a "thorough investigation" to establish the scope and nature of the company�s operations in the country.
The central bank warned investors to discontinue any dealings of a revolving fund scheme nature with the company.
For its part, the CMSA, a government agency, said it was not aware of how Deci Tanzania was investing the money from its thousands of depositors.
Deci officials dismissed the criticism and claims the firm is running an illegal scheme as "unfounded and witch hunting," but did not explain how the firm made huge profits to pay depositors such attractive interests.
"We are not doing any business here, what we do is just revolve the funds, and that is why we call this programme 'tushikamane' revolving fund, we are just providing services and God watches over everything that we do," the firm's chairman, Reverend Jackson Mutalesi, said.
But media reports on the collapse of a similar firm in Kenya heightened suspicions on the sincerity of the scheme.
There are striking similarities between the Deci Tanzania Limited and the Kenyan company. The two have a similar name and both were started and run by religious organisations.
According to reports in the Kenyan media, Deci Kenya Limited operations went under when the Kenyan government launched a crackdown on suspected pyramid schemes.
A number of religious leaders later admitted to having misled their followers into joining the pyramid scheme.
Deci officials refused to talk to The Citizen yesterday when asked about the police probe. The firm's executive director, Mr Ole Loiting'ye curtly said he had nothing to say before disconnecting his phone.
But at the company's headquarters in Dar es Salaam investors seemed unmoved by the recent media reports. Some people jam the offices from as early 3am to late hours.
Mpita Njia
04-05-2009, 07:08 PM
Lakini hawa jamaa wamekuwa waki-operate kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, wakati wote huu wahusika walikuwa wapo kutowazuia kuendelea na shughuli zao?
Ach-F
04-05-2009, 11:28 PM
Serikali ya CCM na Jakaya ina kichwa cha mwendawazimu, wezi kama hawa ati wanachunguzwa? Uchunguzi utakwisha wakati Jakaya amemaliza temu yake ya pili ya urais. Good work.
mwanakijiji
04-06-2009, 04:25 AM
Majira
Benki Kuu ya Tanzania imekana kuitambua kampuni ya DECI inayojishghulisha na uendeshaji wa biashara ya kudunduliza maarufa kama ?Vuna kutokana na mbegu uliyopanda?.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki hiyo, BoT haikuwahi kuipatia DECI leseni yoyote ya kuendesha biashara ya aina hiyo nchini, jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za kampuni za mitaji na mikopo.
Licha ya kuikana, wananchi pia wanafahamishwa DECI hawajapatiwa leseni kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitani ja Dhamana (CMSA) inayoruhusu kuendesha biashara hiyo ya kudunduliza nchini.
?Kwa kuzingatia kwamba uendeshaji na ushirika kwenye shughuliza upatu kama hizo zifanywazo na DECI ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Adhabu na kuwa mwananchi atakayejishughulisha na shughuli zinazoendeshwa na DECI atakuwa anahtarisha mtaji wake mwenyewe? ilieleza taarifa hiyo.
Iliongeza kuwa mamlaka zinazohusika zimeshaanza upelelezi wa kina kuhusu shughuli za DECI yenye ofisi za Mabibo na Tegeta, Dar-es-Salaam ili kujiridhisha juu ya upeo wa mtandao wake wna misingi ya shughuli hizo ambapo kwa sasa umma unadharishwa kutoshiriki biashara ya ?vuna kutokana na ulivyopanda?
?Hatua kama hizi ikiwemo kufungiwa kwa kampuni ya namna hii zimewahi kuchukuliwa ambapo Faidika Investment 2007 iliyokuwa ikijihusisha na shughuli kama hizi za upatu ilifungiwa na wamiliki kufikishwa mahakamani huku ikiwaacha mamia ya wakazi wa Dar-es-Salaam wakilia kw akupoteza kiasi kikubwa cha fedha, kwani biashara hizo hazikuwa halali na ni kinyume cha sheria za nchi,? ilieleza taarifa hiyo.
mwanakijiji
04-06-2009, 04:34 PM
Tanzania Daima
SIKU chache baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuwatahadharisha wananchi kuhusu uwekaji wa fedha katika Kampuni ya Tanzania Care Revolving Fund (T) Limited (DECI), baadhi ya wanaupatu jijini Dar es Salaam wametishia kuandamana hadi BoT kwa madai kuwa wamewavuruga wao na viongozi wa DECI.
Wanaupatu hao walikuwa katika kikundi wakijadili jinsi ya kukusanyika na wafanyabiashara wa maeneo mengine ili kwenda BoT kwa kile walichodai kutokana na tahadhari hiyo imewafanya wachanganyikiwe, kwani DECI imewanufaisha sana.
Mmoja wa wanaupatu hao akizungumza na Tanzania Daima, alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na kile wanachodai kuwa serikali inawaingilia na kwamba walishaanza kupata mafanikio katika vuna vuna hiyo.
Martine Abondo, ambaye ni mmoja wa wanaupatu wanaoandaa maandamano hayo, alisema wanaamini DECI inafanya kazi na inawasaidia Watanzania wengi na kutolea mfano kwake kuwa ameweza kufanikiwa kibiashara pamoja na kujenga nyumba kutokana na mafanikio ya DECI.
Aidha, alisema katika vocha yake anayopatiwa na DECI pindi anapokwenda kuweka fedha kuna TIN namba ambayo inaonyesha kampuni hiyo inalipia ushuru serikali.
Alisema serikali imekuwa haiwatakii mema Watanzania kiasi kwamba wao walitoa sh bilioni moja za kila mkoa, lakini hazijulikani zilikokwenda huku Watanzania walio maskini wakiendelea kuwa maskini na walio matajiri wakiendelea kuwa matajari.
?Hawa hawana lolote, wameona mashirika mengine na mabenki hayapati wateja ndiyo sababu wanaanza kuwatisha Watanzania wasiwekeze hapo, tunajua kuwa kuna wakubwa wanamiliki taasisi za kuwekeza fedha ambazo zina riba kubwa ndiyo sababu za kutaka kuibana DECI ambayo inatusaidia sana. Nimejenga nyumba, nimesomesha watoto kwa kuvuna hapo hapo DECI,? alisema Abondo.
Naye Jenispher Martine, alisema kampuni hiyo imemsaidia na kusema kwamba kama ni kweli kampuni hiyo ni ya kibabaishaji waache wapate hasara.
?Katika hiyo DECI viongozi wa serikali wenyewe wanawekeza fedha nyingi kweli, na ukifika pale majira ya asubuhi utasikia wakurugenzi wanaita kwa mafungu huku wakianza na makundi ya wafanyakazi wa serikalini, hasa wanajeshi ndio walio wengi,? alisema Martine.
Naye Pascazia Rwezahura alisema tangu DECI ianze ndiyo anayoitumia na imemsaidia katika kujenga nyumba na kusomesha watoto.
Aidha, alisema kuwa hawezi kuwekeza benki au kukopa kwa kuwa kuna riba kubwa.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki baadhi ya wanaupatu ambao wamewekeza katika kampuni hiyo walifurika katika ofisi hizo wakitaka ufafanuzi wa kina kuhusu tuhuma hizo kutoka kwa viongozi wa kampuni hiyo.
Wanaupatu hao walionekana kutofautiana kimawazo kwa kuwa kulikuwa na baadhi ya wanaupatu waliandika barua kwa lengo la kutaka kurudishiwa fedha zao na wengine walionekana kuendelea kuwekeza huku wakidai kuwa inawasaidia kuvuna fedha nyingi.
Wiki iliyopita BoT ilitoa tangazo la kuwatahadharisha wananchi kuhusu athari zinazoweza kutokea kutokana na kuwekeza katika kampuni hiyo kwa kuwa haikuwa na usajili.
Ukistaajabu ya Musa,utaona ya wapandaji wa DECI...Tatizo ni kuwa wengi wanaozidi kung'ang'ania ni wasio na elimu ya 'uhakika'.So ikitokea mtu wa hali hiyo anaweka pesa yake na anavuna kisha ukaja kumwambia kuwa huo ni mradi wa kitapeli,hatakuelewa.No matter wat!
mwanakijiji
04-07-2009, 10:59 PM
Mkuu mkjj, nimekupata vizuri. lakini pia naomba kujua.
1.Je kunauwezekano wa DECI kuja kuwaingiza watanzania katka mkenge kama ule wa UPATU?
2.Je kunauwezekano wa kuja kuishitaki DECI ikiwa watu watalizwa pesa zao kwa minajili ya kurudishiwa?
Akajase.. naona maswali yako yameanza kujibiwa!
Mwipagi
04-08-2009, 01:30 PM
Hapa ofisini pana member wa DECI ambaye kwa sasa amechanganyikiwa na hajui nini cha kufanya,amekwenda kutaka arudishiwe mbegu zake (pesa) lakini jibu alilopewa ni kwamba.unapopanda mbegu unasubiri mavuno na siyo kuing'oa/kufukua mbegu!!!!!
Nziku
04-11-2009, 06:59 AM
Ni kweli mbegu huwa hazing'olewi hasa tukichukulia mfano wa mkulima. Hili hata wewe Mkuu Mwipagi unalijua. Ninachokiamini DECI wana sheria zao ambazo kila mwanachama anaridhia kabla ya kujiunga je hizo sheria zinasemaje?
Kwako Mkuu wangu Mwanakijiji, umekuwa mstari wa mbele kulikomalia suala la DECI kama ilivyo katika masuala mengine yaliyomuhimu kwa ustawi wa Taifa letu. Katika kufanya kazi zako, umekuwa ukiweka mbele nyaraka muhimu au kuongea na wahusika. Hili ndo jambo nililokupendea kuliko wanahabari wengine wanao-base katika hear say. Hata hivyo katika suala hili la DECI naona hujafanya jitihada zozote za kutafuta data from the source. I mean viongozi wa DECI au hata Askofu Shegah, Gwamanya et al.
Mkuu sikulaumu ila hili la kuweka nakala za magazeti, concepts from books etc mimi bado sijazikubali.
Ombi: Mkuu Mwanakijiji naomba uwatafute wahusika na uwahoji maswali ya msingi juu ya utata wa biashara yao pamoja na usajili.
pasaka njema wana forumn wote.
Kama wananchi wanaamshwa kuwa kumekucha wao wanaendelea kuvuta shuka na kung'ang'ania bado ni usiku waachwe time will tell. Hakuna sababu ya kuendeleza malumbano, kilichopo ni kuwa wapewe onyo kuwa mambo yatakapogeuka wasije wakailaumu serikali
mwanakijiji
04-13-2009, 09:13 PM
Nziku, kama kuna mtu ana contacts za hawa watu wa DECI niunganisheni tu.. simu yao ya ardhini wala haipokelewi. Mimi ningependa ya mkononi.. hata ya huyo askofu wao. Hivyo kama kuna mtu anayo nitumieni hata kwenye email: mwanakijiji@mwanakijiji.com nitashukuru.
Ach-F
06-13-2009, 07:42 PM
Warning Guys!
That's known as pyramid scheme. Very few people get rich, the ones who run this idiotic scheme. It has made a lot of people more poor. It operated in South Africa, Zimbabwe, Germany and UK. In actual fact its a criminal offence in UK and if caught you end up in Jail.
Unaweza google au nenda wikipedia na search Pyramid scheme.
http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/4c/Pyramid_scheme.svg/350px-Pyramid_scheme.svg.png
http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Dec1.jpg
DECI leaders in the dock at Kisutu Resident Magistrate`s Court in Dar es Salaam yesterday to answer charges of running an illegal pyramid scheme.They are (from-R) Arbogast Francis, Samuel Mtares, Timotheo ole Loiting`ye, Dominick Kigendi & Jackson Mtares.
(Photo Credit: Edwin Mjwahuzi)
Serikali walikuwa wapi? Nani amewajibishwa kwa ucheleweshwaji huu? Raia wamepoteza pesa zao walizovujia jasho?
Saturday June 13, 2009
Local News
Five DECI officials land in court
BETTY BHOKE, 12th June 2009 @ 12:27, Total Comments: 0, Hits: 194
Five officials with the Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) yesterday appeared before the Kisutu Resident Magistrate?s court in Dar es Salaam, all charged with conducting and managing a pyramid scheme and accepting deposits from the general public without licence. The five senior DECI officials pleaded not guilty before Principal Resident Magistrate Addy Lyamuya ? whom the prosecution led by Prosper Mwangamila identified as Jackson Sifaeli, Dominic Kigendi, Timotheo Saiguran ole Loitg?nye and Arbogast Francis, all Dar es Salaam residents.
However, the accused were refused bail, for which defence counsel Abduel Kitururu had earlier applied following submissions by Principal State Attorney Justus Mulokozi who said in a sworn affidavit before Assistant Commissioner of Police (ACP) Eseka Mugasa that the accused should not be granted any bail. The case was adjourned until June 17, when it will be mentioned, also a time when the court would be presented with a counter-affidavit from the defence. The accused were meanwhile ordered to remain in custody.
It is alleged that on various dates between 2007 and March, 2009 at the headquarters of DECI Tanzania Limited, the accused conducted and managed a pyramid scheme, collected money from the public on promises that individual depositors would be entitled to receive ?greater? sums of money as return on their investment. The prosecution further alleged that the accused accepted deposits from the general public without a licence, contrary to Section 911 8(2) of the Banking and Financial Institutions Act number 5 of 2006.
Earlier, it was stated that the firm was run by the Jesus Christ Deliverance Church, and that it was listed as a religious institution to offer soft loans only. The government subsequently froze over 46 DECI accounts to enable people get their money back. It is also believed that hundreds of policemen, teachers, college students and petty traders stand to lose billions of the money they deposited with DECI, allegedly because the firm didn?t have sufficient funds to settle 'matured' claims ? or even repay depositors who wanted to withdraw their monies following the warning that DECI was a pyramid scheme ? and that DECI had no bank account ? except that deposits were stashed in personal accounts.
While warning signals caught up across the country, a company with a similar name in Kenya had allegedly gotten itself involved in similar schemes that also collapsed last December with about 600m Kenya shillings (over Tsh10bn/- ) in deposits. The Kenyan government is currently investigating the defunct company, but it?s not clear whether the two are sister companies.
DECI Tanzania officials have not confirmed any links with the Kenyan scheme. According to DECI officials, the firm has so far paid out over 35bn/- and registered more than 500,000 members since last year when their operations began picking up.
Ach-F
12-15-2009, 10:40 PM
http://www.dailynews.co.tz/pics/12_09_96z4x0.jpg
Directors of the Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) being taken to court to face conspiracy and theft charges before the Kisutu resident Magistrate today.
(Photo by Yusuf Badi).
Ach-F
03-17-2010, 02:25 PM
Magistrate pulls out of DECI case
, 16th March 2010
A RESIDENT Magistrate, Mr Aloyce Katemana, today disqualified himself from hearing the 118m/- theft case against four directors of the Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI). Mr. Katemana who was hearing the case at the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam, reached the decision after the accused wrote a letter showing that they have lost confidence in him. The accused, Dominic Kigendi, Jackson Sifaeli Mtares, Timotheo Saiguran ole Loitg'nye and Samwel Sifael Mtares, had claimed in the letter that the magistrate would not do justice in the future, as he had denied them bail for 'unjustifiable' reasons.
Following his disqualification, the magistrate adjourned the case to April 12 and returned the case file to the magistrate-in-charge for reassignment of another presiding magistrate. The accused appeared before the court for the first time on December 15, last year, charged with conspiracy and theft of more than 118m/-, property of the company. It was alleged by the prosecution, led by State Attorney Mutalemwa Kishenyi, that the accused, being directors of DECI and with intent to defraud the public, conspired to commit the offence of stealing between December 1 and 8, last year.
The prosecutor told the court that on December 8, last year, at Standard Chartered Bank, Kariakoo Branch in Ilala District, the accused stole 118,440,000/-, property of DECI. They denied the charge. Magistrate Katemana ordered them to go in remanded until December 21, last year, to wait a decision on their bail application following submissions by the prosecution and defence, led by advocate Hudson Ndusyepo on whether or not they should be granted bail. State Attorney Kisheni had wanted the accused denied bail on ground that they committed the offences while under the bail of another case against them, in which they are accused of conducting and managing a pyramid scheme and accepting deposits from the public against the law. Advocate Ndusyepo had strongly opposed the prosecution's move, submitting that in the previous case there was no bail condition restraining them from executing DECI activities, including drawing money which was within their powers as directors.
On December 21, last year, the magistrate denied the accused bail after upholding the prosecution's objection. The accused were dissatisfied by the decision and appealed to the High Court, which overruled the lower court's decision and granted the accused bail.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.