PDA

View Full Version : Wanakijiji wako waoga kuchangia!

Mr. XXX
01-14-2009, 11:51 PM
Kwanini wanakijiji wa hapa wanaogopa kuchangia wanakuja na kuangalia tu na kudonoa kisha wanaenda zao. Baada ya kutoka mapumziko marefu nimeamua kuhamisha kabisa nyumba na kukaa hapa hapa hadi mkuu wa kijiji anifukuze!

Kwa vile inaonekana mnaogopana hapa hasa watu kukuogopa wewe mkuu wa kijiji, ndiyo maana nadhani wanaogopa kutoa mawazo yao hapa kwani wakipingana na wewe wanaweza kujiona kuwa siyo mahali pao.

Mzee wa hoja waache waoga waende zao na sisi vidudumtu na tuendelee kubanana hapa hapa. Nimegundua hata wanaochangia wanachanggia utadhani kuna watu wanawasimamia nyuma.

Na hata kazini kuna watu hawataki kuonekana wamefungua website hii wasije kudhaniwa kuwa ni wanachama!

Je tunaturusiwa kuwazomea watu kama ilivyokuwa shule za msingi? Mkuu kibaraza hiki chetu kitakuwa na nguvu kama jamaa zetu hawa watatoa woga na kuwa watazamaji tu.

My more
01-15-2009, 02:03 AM
Sidani kama kweli ni uoga, ama ni uchoyo wa michango, SIna hakika kama wanamgwaya Wakjj pia, kwa sababu kuna baadhi ya threads ziko huru sana tu na bado watu hawachangii. Labda tuseme bado watu wanafanya warm up kama ndugu yetu Quemu alivyosema!! hebu tuwapatie kaji-muda

kurutamatata
01-15-2009, 03:36 PM
Tatizo hapa siyo Uoga bali ni Uelewa Mdogo miongoni mwa wachangiaji wetu wa Kitanzania
pamoja na gharama kubwa za Internet kwenye ma Cafe ya watu binafsi.Kama mtu hana access
na Internet ya Kazini kwake au kwa Jamaa yake mwenye uwezo kidogo wa kifedha lazima tukiri
kwamba suala hili siyo jepesi kama wengi wetu watakavyo lichukulia.Achilia mbali Mtandao huu
wa mwanakijiji, bali hata viwango vya Uandishi wa Habari katika Magazeti yetu mbalimbali hapa nchini viko chini sana.Huwa naingiwa na wasiwasi kwamba usije kuta Wahariri wa baadhi ya Magazeti hayo wameshatiwa Mfukoni na wenye Nazo.Habari nyingi zilizopaswa kuwa za uchambuzi wa kina utazikuta ziko Shallow ile mbaya, hazizami kina kinachotakiwa, ni habari za kupapasa papasa tu bila kukwaruza, za kumpendezesha Kiongozi fulani,pengine kwa matarajio ya kupewa vijisafari vya masomo mafupi nchi za nje au zaidi ya hapo,hakuna anayejua!Lakini imefikia mahali kiasi kwamba Mtu atasita kulinunua gazeti maramoja bila kuliperuzi ndani haraka haraka ili ajiridhishe na kilichomo mle ndani yake.Ni aibu.Siamini kama kweli kwamba hatuna Waandishi wa Habari wenye Uwezo Mkubwa Kitaaluma na hata Kipaji katika kazi hiyo.Kwa hiyo tusikiri hapa kwamba wanakijiji ni waoga kuchangia,la hasha.Yapo matatizo kadha wa kadha yakiwemo Uelewa Mdogo, Gharama za Mitandao hapa nchini, pengine VAT nayo imechangia katika hili.Tumetanguliza sana mbele PESA NA MAPATO YA SERIKALI kuliko Elimu na Maendeleo!

mwanakijiji
01-16-2009, 10:36 PM

naamini wanachama wetu wana uwezo wa kutosha kabisa kujadili jambo lolote lile ambalo wanajua wana uwezo wa kulijadili. Nafahamu itachukua muda kidogo ili watu waweze kuwa comfortable hapa. Tuko pamoja na tusikatishwe tamaa na watu ambao wanasubiri tujikwae tuanguke.

Ach-F
01-17-2009, 01:36 AM
Mr xxx

Yamekuwa haya tena? Wanakijiji wakirudi kijijini huwa wanajipumnzisha na hivyo kuchangia kimkanda mkanda. Wewe endelea kulima tu wakija shituka mvua zimeacha kunyesha na wewe CRUNCH haiwezi kukugusa utakuwa unaisikia tu. Gambile... Longa.........Say.......

911
01-18-2009, 08:49 AM
Sio uoga,bali ni taratibu tu za 'kikwetu'.Bongo hii mgeni ambaye anakuwa na maneno mengi huwa watu wanam_perceive kuwa ni tapeli au mwongo!!!

ponda
01-20-2009, 10:54 AM
Tatizo hapa siyo Uoga bali ni Uelewa Mdogo miongoni mwa wachangiaji wetu wa Kitanzania
pamoja na gharama kubwa za Internet kwenye ma Cafe ya watu binafsi.Kama mtu hana access
na Internet ya Kazini kwake au kwa Jamaa yake mwenye uwezo kidogo wa kifedha lazima tukiri
kwamba suala hili siyo jepesi kama wengi wetu watakavyo lichukulia.Achilia mbali Mtandao huu
wa mwanakijiji, bali hata viwango vya Uandishi wa Habari katika Magazeti yetu mbalimbali hapa nchini viko chini sana.Huwa naingiwa na wasiwasi kwamba usije kuta Wahariri wa baadhi ya Magazeti hayo wameshatiwa Mfukoni na wenye Nazo.Habari nyingi zilizopaswa kuwa za uchambuzi wa kina utazikuta ziko Shallow ile mbaya, hazizami kina kinachotakiwa, ni habari za kupapasa papasa tu bila kukwaruza, za kumpendezesha Kiongozi fulani,pengine kwa matarajio ya kupewa vijisafari vya masomo mafupi nchi za nje au zaidi ya hapo,hakuna anayejua!Lakini imefikia mahali kiasi kwamba Mtu atasita kulinunua gazeti maramoja bila kuliperuzi ndani haraka haraka ili ajiridhishe na kilichomo mle ndani yake.Ni aibu.Siamini kama kweli kwamba hatuna Waandishi wa Habari wenye Uwezo Mkubwa Kitaaluma na hata Kipaji katika kazi hiyo.Kwa hiyo tusikiri hapa kwamba wanakijiji ni waoga kuchangia,la hasha.Yapo matatizo kadha wa kadha yakiwemo Uelewa Mdogo, Gharama za Mitandao hapa nchini, pengine VAT nayo imechangia katika hili.Tumetanguliza sana mbele PESA NA MAPATO YA SERIKALI kuliko Elimu na Maendeleo!

Ili mtu aweze kuchangia sio uelewa wala nini pengine inategemea na posting yenyewe kama yuko interested nayo au inamsisimua. wakati mwingine ni bora uwe observer kuliko kukurupuka na kwenda nje ya msitari.

mfano hii post ya kutochangia inhusianaje na waandishi wa habari kwenye magazeti? au mimi ndio sijaelewa

Mpita Njia
01-21-2009, 01:50 PM
Kwa vile inaonekana mnaogopana hapa hasa watu kukuogopa wewe mkuu wa kijiji....

Kwa nini wamuogope Mwanakijiji?

Matigari
01-21-2009, 04:46 PM
salam.

Sidhani kama watu ni waoga kuchangia. Ninaamini kuwa kuna baadhi ya watu hawapendi kuchangia hoja kama hawana taarifa kamili hasa hasa kwa watu walio nje ya nchi. Ni vigumu kuchangia mada kama hujui hali halisi, na huna habari za kutosha kuzungumzia hilo suala.

Wengi wetu tuna mazoea ya kuwa empirical.

Kitu ninachoipendea hii forum ni kuwa watu hawashikani mashati bila ya sababu na kupoteza muelekeo wa thread. Kwa mfano watu hapa wanapozungumzia ubakaji wa watoto hoja haiishii kuwa ya kidini au kikabila au ya wa mjini Vs wa shamba. Nadhani subconsciously watu wanaavoid malumbano ya namna hiyo.

mwanakijiji
01-21-2009, 05:11 PM

hapa umesema kwani katika baraza hili mambo yasiyo na msingi hayana nafasi. Na tutajitahidi sana kuhakikisha hatuachi malumbano yasiyo na msingi au yenye mrengo wa mgogoro kutokupata nafasi.

Akajase
01-21-2009, 07:00 PM
Ninachojua ni kuwa mtupa mshale mbali ni yule anayevuta upinde sana. Sasa wakati anavuta sana upinde, watu wengine huweza fikiri kuwa mbona anachelewa kuuachia. Ukitoka hapo wewe sikilizia vilio vyake.
Jamvini hapa ndivyo palivyo,watu wanavuta pinde kwa nguvu, siku watapoachia mishale yao usistaajabu kelele zakutaka jamvi lifungiwe, wanakikao kuanza kutafutwa kwa juhudi na kadhalika. kisa zile cheche za fikra sahihi zimewasha moto kwa watu hawataki kudanganywa tena na kufanywa maamuma wakuitikia wasichokijua.

Baraka
04-20-2009, 07:41 PM
Mimi ni mgeni katika kijiji, kilichonivutia, ni 'ustaarabu' hapa watu hawapayuki, wanajadili, hata hao wanaodonoa, wanajifunza, ingekuwa haiwavutii, wasingepoteza muda wao kuichungulia. Lengo kubwa ni kuibua mambo na mijadala na zaidi ya yote kuelimishana. Mwanakijiji hakikisha watu wa rika zote wanashiriki kwa kulinda maadili.