PDA

View Full Version : Hongera Rais Kikwete!

Mr. XXX
01-14-2009, 11:46 PM
Wapinzani wakubali au wasikubali mkuu umeonyesha njia na unaonyesha mfano wa uongozi!

- ulikubali Waziri wako Mkuu ajiuzulu kwa kashfa na wala hukujaribu kumtetea

- ulikubali baraza livunjike na serikali yako iaabike ili uweze kuanza upya

- ulipuuza maneno ya wapinzani ambao wamejaribu sana kukukatisha tamaa na kukufanya uonekane wewe wa kuja.

- uliruhusu mmoja wa mabalozi kufikishwa mahakamani bila kuchelewa

- watuhumiwa wa EPA ambao watu walisema hawatachukuliwa hatua sasa hivi wanahaha

- Mawaziri waliokuwa na kiburi na waliokifanya chama chetu kionekane vibaya hawana tena pa kuficha nyuso zao.

- Mtu wa Richmond amefikishwa mahakamani huku wenzake ukiwaweka tayari kuwabanika kama kuku wa kienyeji

- watu wa Kagoda nao nina uhakika hawako mbali.

- Umesababisha hata aliyekuwa Waziri Mkuu mwenye kimbelembele cha kujifanya anapiga vita rushwa aanze yeye mwenyewe kujitetea kabla ya kushtakiwa!

kutoka kwa wanachama watiifu wa CCM, vijana ambao tumenyweshwa maji ya bendera tunasema hongera baba, ongeza mwendo mpaka vyama vyote vya upinzani vitoweke nchini na taifa letu liwe katika demokrasia ya chama kimoja!

Baija Bolobi
02-23-2009, 01:53 PM
Haiwezekani kijana akawa na mawazo ya namna hii yaliyoganda. Huyu JK mwenyewe au mwandishi wake wa hotuba. Pamoja na shopping list listi ya mafanikio yaliyotajwa, ni vigumu kusema serikali hii ina mwelekeo wowote unaoeleweka. Hata vita hii ya ufisadi, tungependa awaguse Kagoda na Deep Green ndipo asimame na kusema nimefanya kazi.

dickabudi
02-23-2009, 02:54 PM
Siku ambayo Kikwete kama Rais atawagusa Kagoda na Deep Green atakuwa amefanya kazi isiyo yake, tuwakabe Kurugenzi ya upelelezi Jeshi la Polisi, Kurugenzi ya mashtaka, Msajili wa makampuni na TAKUKURU watimize wajibu wao, tuone Rais ataingilia kuwaachilia?

mwanakijiji
02-23-2009, 06:08 PM
Lakini ikitokea hivyo watu watampa kudos Kikwete!

Ach-F
02-24-2009, 01:00 AM
Wapinzani wakubali au wasikubali mkuu umeonyesha njia na unaonyesha mfano wa uongozi!

- ulikubali Waziri wako Mkuu ajiuzulu kwa kashfa na wala hukujaribu kumtetea

- ulikubali baraza livunjike na serikali yako iaabike ili uweze kuanza upya

- ulipuuza maneno ya wapinzani ambao wamejaribu sana kukukatisha tamaa na kukufanya uonekane wewe wa kuja.

- uliruhusu mmoja wa mabalozi kufikishwa mahakamani bila kuchelewa

- watuhumiwa wa EPA ambao watu walisema hawatachukuliwa hatua sasa hivi wanahaha

- Mawaziri waliokuwa na kiburi na waliokifanya chama chetu kionekane vibaya hawana tena pa kuficha nyuso zao.

- Mtu wa Richmond amefikishwa mahakamani huku wenzake ukiwaweka tayari kuwabanika kama kuku wa kienyeji

- watu wa Kagoda nao nina uhakika hawako mbali.

- Umesababisha hata aliyekuwa Waziri Mkuu mwenye kimbelembele cha kujifanya anapiga vita rushwa aanze yeye mwenyewe kujitetea kabla ya kushtakiwa!

kutoka kwa wanachama watiifu wa CCM, vijana ambao tumenyweshwa maji ya bendera tunasema hongera baba, ongeza mwendo mpaka vyama vyote vya upinzani vitoweke nchini na taifa letu liwe katika demokrasia ya chama kimoja!

Stupidity is an art. Kwa nini Waziri mkuu aliyejiuzulu hakushitakiwa kwa uhujumu wa uchumi? Hii inaonyesha jinsi Jakaya Kikwete alivyo, kuwalinda wezi na marafiki zake. haya ni mambo ya kinafiki ambayo yamepitwa na wakati, huwezi leo hii kusifia kiongozi anayefanya mchezo wa ukuti ukuti cha mnazi.