mwanakijiji
01-15-2009, 08:18 PM
Dk. Mwakyembe awakatalia wapiga kura kuondoka CCM (Mwananchi)
Richard Kilumbo,Kyela
MBUNGE wa Jimbo la Kyela Dk Harrison Mwakyembe,amesema hana mpango na wala hafikirii kukiacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kujiunga vyama vya upinzani nchini.
DK. Mwakyembe alisema hakuna Chama chochote cha upinzani kinachoweza kufananishwa kwa ubora , umakini, uzuri wa sera na hata uwingi wa wanachama na CCM.
Kauli hiyo aliitoa juzi kwenye mkutano wake na wananchi wa jimbo lake uliofanyika viwanja vya Siasa mjini hapa ambapo baadhi ya wananchi walimtaka kuihama CCM ili afanye kazi ya kufichua mafisadi kupitia kambi ya upinzani.
Mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Erick Satta mkazi wa mjini hapa alisema wananchi wa jimbo lake wanamwamini mbunge huyo kwa kiwango kikubwa, lakini wanaingiwa na shaka na mahali aliko (CCM)ambako alisema wananchi wanaamini, mbunge wao anabanwa, na hawezi kusema lolote linalopingana na sera na itikadi ya Chama.
Satta alisema ili aweze kufanikisha azma ya kuwakomboa wananchi wa Tanzania mbunge huyo hana budi kubadilika na kujiunga na mageuzi ambako ataungwa mkono kutoka kwa wananchi na viongozi wenzake wa vyama vya upinzani.
Alimtaka mbunge huyo kukubaliana na matakwa ya wananchi wengi wanaomshinikiza kuihama CCM kwa madai kimejaa mafisadi wasiowezwa kushughulikiwa na kiongozi wa ndani ya Chama hicho.
" Tunakupenda,tuko nawe na tutakuchagua mwaka 2010, ukiwa ndani ya Chama kingine, cha Siasa na siyo CCM" alisema Satta.
Akijibu hoja kwa kupinga msimamo huo, Dk. Mwakyembe aliwabeza wale wote wanaomshinikiza kuihama CCM na kusisitiza kwamba, hapa nchini hakuna Chama cha siasa kilicho makini na chenye sera safi zinazotekelezeka na chenye wanachama wengi kuliko CCM.
Dk. Mwakyembe alisema, mtu yeyote anayetaka kupambana na maovu yanayofanywa na baadhi ya watu walio na nia mbaya na Taifa lao hana budi kuendelea kubaki ndani ya CCM.
"Ukitaka kufanya mambo yako vizuri,na unataka usikilizwe, uishi maisha marefu ni bora, ubaki CCM kuliko ukawa kwenye upinzani na kupayuka mambo bila ushahidi wa kutosha.
Alisema utetezi na uchungu wa mtu yoyote hauwezi kusikika, na kufanyiwa kazi kwa kina, kama utafanywa na wapinzani walio nje ya CCM.
Akitetea msimamo wake alisema ni lazima watu washindane na kubezana kwa hoja kuliko kuleta ubishi usio na manufaa.
"Fikiria ujasiri unaofanywa na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete , ni mkubwa mno, lakini wapo watu wanaobeza jambo ambalo hata CCM ingefanya nini, wapo watu ambao wataendelea kubeza tuu.
Alisema, Rais Kikwete amefanya mambo mengi na yenye ushujaa kwa kuweza kuwafikisha viongozi waandamizi aliowahi kufanya nao kazi katika awamu mbalimbali akiwa Waziri , lakini amefanikisha kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya dola wakituhumiwa kuitia hasara Serikali ya awamu ya tatu kwa kuruhusu msamaha wa kodi ya Sh 11 bilioni.
"Hivi, ni nani kati yenu, anayeweza kuruhusu rafiki yake wa karibu akamatwe, hata kama amekosea?, na ni Kiongozi gani katika awamu zote tatu zilizopita aliyeweza kuwa jasiri akaruhusu marafiki na viongozi wenzake wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya dola kama si Rais Kikwete"aliwauliza wananchi Dk.Mwakyembe.
Hata hivyo, pamoja na kusifia mafanikio mbalimbali yaliyoletwa na Serikali ya awamu ya nne, Dk Mwakyembe alizungumzia pia kazi nzuri iliyofanywa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye alisema aliimarisha na kuinua Uchumi wa nchi.
Kuhusu sakata la kukatika katika kwa umeme wilayani Kyela , mbunge huyo alisema atayapeleka mawazo ya wananchi waliomtaka mbunge wao ayafikishe mambo hayo kwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngereja ya kuruhusu wananchi wa Kyela wautumie umeme unaozalishwa na Kiwira Coal Mine ili kuepuka na kero hiyo.