PDA

View Full Version : Utetezi wangu wa Mhe. Sophia Simba dhidi ya Ukosoaji usio wa haki



mwanakijiji
01-16-2009, 09:01 AM
Nikiri ya kwamba nimesikitishwa na kushangazwa sana na baadhi ya ukosoaji wa Mhe. Simba kufuatia mahojiano yangu naye siku chache zilizopita. Kilichonisikitisha zaidi ni jinsi gani baadhi yetu tuna angalia vitu ambavyo si vya msingi na kuviacha vya msingi; kilichonishangaza zaidi ni jinsi gani wengine wamekuwa wa kali kiasi cha wao wenyewe kuwa kile wanachomtuhumu Mhe. Simba.. arrogance!

Katika mahojiano yangu na watu mbalimbali (kama Dr. Migiro, Dr. Salim, na wengineo) sijawahi kujaribu kumtetea mtu yeyote kwa majibu yake. Hata hivyo katika hili la Mhe. Simba nimeona kilele cha kebehi na kina cha parapanda ya unafiki wa uongo. Wengi wamemhukumu Mhe. Sofia kwa ukali ambao haukustahili na umeenda zaidi ya ukosoaji wa kumjenga mtu!

Kwa hawa nina ujumbe ufuatao: Sikiliza!

BONYEZA HAPA KUSIKILIZA (http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/2009-01-15T21_40_42-08_00)

Unaweza kusikiliza pia kwenye ukurasa wetu wa mbele kwenye Podcasts au hapo juu kwenye podcasts.

skasuku
01-17-2009, 07:29 PM
MMM, nimepata fursa yakuisikiliza interview yako na Waziri Simba, binafsi nimependa sana mlolongo wa hayo mahojiano, na kwa kweli sijaona ishu kubwa ambayo wakosoaji wameweza anika katika analysis zao.

Mtazamo wangu, katika jamii utakuta tuu watu wenye fikira tofauti, hili mimi ninaona ni afya. Tutasikiliza yale yanayo make sense na hayo mengine we just ignore.

ps: ukisaga mahindi, unapata uga safii, ila pia kuna pumba.....