PDA

View Full Version : Wamewaonea kina Nsia Swai!

mwanakijiji
01-16-2009, 06:16 PM
Mojawapo ya vituko vya siku hizi ni kusimamishwa masomo kwa wanafunzi wawili wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino pale Nyegezi Mwanza ni kusimamishwa masomo kwa wanafunzi wawili ambao picha zao zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao mbalimbali! Ninaamini kuwa kwa kuangalia picha hizo tu si sababu tosha ya kukatisha elimu ya mabinti hawa na nitatoa sababu zangu muda si mrefu.

Mojawapo ya picha hizo ni hii hapa:

http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1232088837_nsiapic.jpg

outlier
01-16-2009, 11:07 PM
Duh!
Anaita!
Haya tupe hizo sababu ndugu mwenyekiti-

mwanakijiji
01-16-2009, 11:32 PM
Kwanini naamini wamewaonea:

a. Kupiga picha ambazo zinaonesha maumbile ya kike/ya kiume katika hali ya uzuri (good taste) siyo kosa. Mabinti hawa sio Watanzania wa kwanza kupiga picha zinazoonesha maumbile yao namna hii. Wengine kabla yao ni Flaviana Matata, Richa Adhia, na Amanda Ole Sulul

- Huyu Amanda

http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/entertaiment/amande.jpg

- Huyu Richa Adhia

http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/entertaiment/richaadhia.jpg

- Huyu hapa Flaviana Matata

http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/entertaiment/misstanzania.jpg

Tofauti kati ya picha hizo ni "mahali tu walipopiga".. hao wengine wamepiga mbele ya kamera za kimataifa na hawa kina Swai wamepiga vyumbani mwao!

Hiyo sababu ya kwanza: Nitaendelea...

Zingatia: Ninafanya haya kwa uzalendo mkubwa kwa nchi yangu!!! God bless Tanzania!

911
01-18-2009, 09:11 AM
Gud mkjj,but hebu tuangalie namna ulivyowalinganisha hao akina Nsia na hao wengine.Ni vema ikawa wazi kuwa hao akina Richa etal walipiga picha hizo "kikazi" au ktk mazingira ya kuutangaza urembo wao.Infact they are models.Ila inapokuja kwa hawa akina Nsia mkuu itabidi uone tofauti ya mazingira.They are students pia ni katika chuo chenye mtazamo wa kidini.Ni taswira ya namna gani chuo hiki kitaijenga kwa jamii kama kitaacha tabia za namna hii zikiendelea bila kukemewa na kuchukuliwa hatua nyingine?Hata hao warembo wengine uliowataja hapo ni kuwa picha hizo au kuonekana kwao katika kivazi cha "vichupi" kimekuwa kikipigwa vita sana hapa Tz.Hawa wanafunzi wamefika kiwango cha kushow off their breasts,wat for???Adhabu waliyopewa wanaistahili na ikibidi wafukuzwe kabisa hapo chuoni.
Tanzania tunayoililia ni ile isiyo na ufisadi na yenye neema LAKINI sio tena pasiwe na maadili.Ni hayo kwa sasa.

duru langu
01-18-2009, 09:26 PM
Binafsi naamini kwamba hawa mabinti Nsia na mwenzake ni victims na wanastahili zaidi huruma na msaada wa kisaikolojia kwa dhahama iliyowapata ya kuanikwa mtandaoni.

Hata hivyo mzee mwanakijiji picha walizotolewa ni zaidi ya hiyo ya kimiss kwa hiyo sidhani
ulinganishi wa picha uliofanya ni sawa. Hizo picha ambazo hukuzitowa ndio zilipaswa
kuwa kigezo cha kuwaonea huruma kuliko kuwaadhibu.

mwanakijiji
01-20-2009, 12:38 AM

duru langu hata hizo nitafika huko katika utetezi wangu unaoendelea kesho...

mfumwa
01-20-2009, 07:08 AM
Hawa hawajaonewa, ukishiriki show katika Casino na ukawa upo uchi, si sawa ukayafanya hayo mtaani, hilo linakuwa jambo la aibu mbele ya jamii. Inategemea hukokukaa uchi ulikufanyia wapi. Tuangalie hawa hawa mamiss na nguo zao (vichupi) waende Msikitini ama Kanisani, hawa ni watu wa kuombewa waache hivyo vivazi, lakini wakiwa katika mashindano ya urembo, ndio vigezo vyao hivyo vya uvaaji.

SAUT ni chuo kikuu, kina sheria na miongozo yake. Hivyo kuwafukuza itakuwa wamefuata sheria hizohizo ambazo wakina Nsia walipojisajili walitakiwa kuzifuata. HEBU TUFIKIRI Mtakatifu Augustine anafufuka leo na kukuta Nsia na kichupi, angesemaje?

911
01-20-2009, 09:45 AM

Nashukuru mkuu,kwa kuliona hilo.Ifikie kipindi watu waache kuchanganya context za matukio.Kwani hao mamiss et al waliopiga hizo picha za "kufanana" na hizo za akina Nsia ni wanafunzi wa wapi??Come on people,hawa wanachuo ndo wasomi wetu ambao tunatarajia wawe mstari wa mbele katika kuijenga Tz.Ningekuwa convinced kama kungekuwepo na wanachuo wengine hapo SAUT waliowahi kufanya kitu kama hicho kisha hawakuchukuliwa hatua kama hizo or wapo waliofanya baada yao na wakaachwa.Hapo tungesema hawa WAMEONEWA.
Nimefanikiwa kuziona picha zake/zao zipatazo nne hivi,bila kujiumauma ni kuwa ni aibu iliyopitiliza kwa chuo,lettin alone wazazi wao,ndugu,wachumba/wapenzi(if any)!!Hakuna social justification kwa upigaji wa picha za aina ile.Yamewakuta,then wengine wajifunze kutoka kwao.

duru langu
01-20-2009, 11:19 PM

Hivi kuna sheria yoyote inayokatazwa mtu kujipiga/kupiga picha akiwa mtupu (bila nguo) chumbani kwake? Kama hizo picha wangekuwa wamezisambaza wenyewe kwenye mtandao kwa utashi wao hilo lingekuwa na mushkiri. Hao mabinti huenda walikuwa wana "admire" miili yao na pengine kutaka kuwa na kumbukumbu ya miili yao wakati wa ujana (kitu ambacho wengi hatuna) ili baadae hata miili "ikichoka" wajifariji kwamba enzi zao walikuwa wamo!

Hizo picha zimeibiwa na kuwekwa mtandaoni na wakuadhibiwa ni hao walioiba hizo picha.

911
01-23-2009, 09:22 AM

mkuu,naamini kuwa sio sahihi kama tutakuwa tunaangalia uhalali wa mambo kwa kutizama sheria tu.Licha ya sheria zetu kuwa na mapungufu mengi tu(sitalizungumzia kwa undani) lakini napenda kukumbusha kuwa sometimes masuala huwa "judged" from ETHICS point of view.Na hili ndilo hasa lililotumiwa na watu hadi kupelekea kuona kuwa hawa wadada ni wakosefu.Pia siko sure na sheria za chuo chao zinasemaje kuhusu vitendo kama hivi,nadhan wachangiaji wanaolifahamu hili wataliweka sawa.Hao walioziweka mtandaoni wamesaidia kutufumbua macho juu ya mambo yanayoendelea ktk vyuo vyetu(not all inclusive).Kwa nijuavyo ni kuwa kwa maadili ya kiTanzania,kupiga picha za uchi its unacceptable.

pundamilia
01-23-2009, 11:07 AM
Mimi nitatofautiana kidogo na baadhi ya wachangiaji walionitangulia hapo juu.

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustine nadhani hawakwenda mbali zaidi katika kutafakari suala hili la hawa mabinti. Kazi moja wapo ya Chuo kile ni kuwalea wanafunzi katika misingi bora ya kimaisha na hata kiroho. Nsia na mwenzake mimi ninawaona ni kama kondoo waliopotea, walistahili kupata mchungaji ambaye atawarudisha kundini na si vinginevyo. Kosa lao hao vijana adhabu yake ni kupewa wasaa wa kujutia waliyoyafanya na wala siyo kuwafukuza shule.
I believe kabisa makosa yao yalistahili adhabu nyingine ya kawaida na wala si hiyo ambayo ni kubwa hailingani na kosa lenyewe.
Inawezekana adhabu hiyo imetolewa kwa hamaki bila ya kutafakari uhalisi wa matatizo ya vijana. Ningeshauri adhabu yao ipunguzwe, wapate councellor wakuzungumza naye juu ya fikra zao, na mwisho wapewe nafasi ya kujutia makosa waliyoyafanya. Ninaamini hawa kondoo hatutawapoteza na wanaweza kuja kuwa kondoo wa msaada kwa wanafunzi wengine hapo chuoni na kwa jamii kwa ujumla.
Give them a second chance.

duru langu
01-25-2009, 04:59 AM
mkuu,naamini kuwa sio sahihi kama tutakuwa tunaangalia uhalali wa mambo kwa kutizama sheria tu.Licha ya sheria zetu kuwa na mapungufu mengi tu(sitalizungumzia kwa undani) lakini napenda kukumbusha kuwa sometimes masuala huwa "judged" from ETHICS point of view.Na hili ndilo hasa lililotumiwa na watu hadi kupelekea kuona kuwa hawa wadada ni wakosefu.Pia siko sure na sheria za chuo chao zinasemaje kuhusu vitendo kama hivi,nadhan wachangiaji wanaolifahamu hili wataliweka sawa.Hao walioziweka mtandaoni wamesaidia kutufumbua macho juu ya mambo yanayoendelea ktk vyuo vyetu(not all inclusive).Kwa nijuavyo ni kuwa kwa maadili ya kiTanzania,kupiga picha za uchi its unacceptable.

Ethics za wapi zinazosema kujipiga (manake siku hizi unaweza kujipiga picha) bila nguo ni kosa?
Mwishoni watu watasema hata kulala chumbani kwako bila nguo ni kinyume cha ethics.
Hao mabinti ni victims tu na watu wanajaribu kujificha nyuma ya vivuli vya aina mbali mbali ili kutokubali victimization iliyotokea kwa mabinti hao.

magoma
02-10-2009, 04:18 PM
mkuu,naamini kuwa sio sahihi kama tutakuwa tunaangalia uhalali wa mambo kwa kutizama sheria tu.licha ya sheria zetu kuwa na mapungufu mengi tu(sitalizungumzia kwa undani) lakini napenda kukumbusha kuwa sometimes masuala huwa "judged" from ethics point of view.na hili ndilo hasa lililotumiwa na watu hadi kupelekea kuona kuwa hawa wadada ni wakosefu.pia siko sure na sheria za chuo chao zinasemaje kuhusu vitendo kama hivi,nadhan wachangiaji wanaolifahamu hili wataliweka sawa.hao walioziweka mtandaoni wamesaidia kutufumbua macho juu ya mambo yanayoendelea ktk vyuo vyetu(not all inclusive).kwa nijuavyo ni kuwa kwa maadili ya kitanzania,kupiga picha za uchi its unacceptable.

to be honnest hawa wadada hawna akili hata kidogo, nadhani turudie tamaduni zetu jamani tanzania/tanganyika hatukuwa hivyo na mimi sidhani kama wana miili mizuri ya kuonekana uchi kuliko wanawake wengine,vlvl hawa ni wanafunzi tena chuo cha dini jamani kumbuka hapo chuoni kuna seminari sasa hawa mabinti wanataka tupate watumishi wa serikali wa aina gani kama mtu kama huyo akihitimu then anakuwa afisa ustawi wa jamii au wilaya/mkoa upi na jamii na watatoa mafundisho /makemeo yapi kwa jamii kama viongozi. Then mtu mwingine anasema wameonewa, niliona mwingine anajiita eti kaka mtu anatoa onyo kwa watu kuhusu dada yake, familia ya malezi mabovu huwa mbovu hata kizazi chake pia

magoma
02-10-2009, 04:26 PM
Mimi napendekeza wafukuzwe kabisa, huo umalaya na tabia za aina hiyo zIkomeshwe hapo chuoni, ASIYEFUNZWA NA MAMAYE HUFUNZWA NA ULIMWENGU. NA HUO NDO ULIMWENGU UMEWAFUNZA, MALEZI YA HOVYOHOVYO,ENZI ZA MWALIMUUUUUUUUUUUUUUUUUUU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! !!1

mwanakijiji
02-10-2009, 06:24 PM
to be honnest hawa wadada hawna akili hata kidogo, nadhani turudie tamaduni zetu jamani tanzania/tanganyika hatukuwa hivyo na mimi sidhani kama wana miili mizuri ya kuonekana uchi kuliko wanawake wengine,

Kweli unataka turudie tamaduni zetu? Unajua mambo ya jando na unyago yalikuwaje? Unajua binti wa kimakonde (hata makabila mengine) wakitolewa unyago wanatoka vifua wazi? Kama mtu akipiga picha hizo hawana tofauti na wale mabinti wa King Mswati! Je ni mila hizo? Ukienda kule Umang'atini, hata leo hii kuna mabinti hawavai kitu chochote juu wako watupu je tutasema wako uchi wakipiga picha au ndiyo tamaduni zao?

vlvl hawa ni wanafunzi tena chuo cha dini jamani kumbuka hapo chuoni kuna seminari sasa hawa mabinti wanataka tupate watumishi wa serikali wa aina gani kama mtu kama huyo akihitimu then anakuwa afisa ustawi wa jamii au wilaya/mkoa upi na jamii na watatoa mafundisho /makemeo yapi kwa jamii kama viongozi.

Hawa watoto wamepiga picha chumbani kwao, in the privacy of their bedroom, hawakuzisambaza picha hizo wao wenyewe sasa imekuwaje wawe na hatia? Kama alivyosema mtu mwisho mtawakataza mabinti kujiangalia kwenye kioo wakiwa uchi wanajipaka mafuta!!

Then mtu mwingine anasema wameonewa, niliona mwingine anajiita eti kaka mtu anatoa onyo kwa watu kuhusu dada yake, familia ya malezi mabovu huwa mbovu hata kizazi chake pia

Kuonewa wameonewa, kwani hawajavunja sheria yoyote, wala kukiuka maadili yeyote. Hivi umewahi kwenda Vaticani kwenyewe uone mapicha na masanamu yaliyouchi?

duru langu
02-12-2009, 03:31 AM
to be honnest hawa wadada hawna akili hata kidogo, nadhani turudie tamaduni zetu jamani tanzania/tanganyika hatukuwa hivyo na mimi sidhani kama wana miili mizuri ya kuonekana uchi kuliko wanawake wengine, vlvl hawa ni wanafunzi tena chuo cha dini jamani kumbuka hapo chuoni kuna seminari sasa hawa mabinti wanataka tupate watumishi wa serikali wa aina gani kama mtu kama huyo akihitimu then anakuwa afisa ustawi wa jamii au wilaya/mkoa upi na jamii na watatoa mafundisho /makemeo yapi kwa jamii kama viongozi. Then mtu mwingine anasema wameonewa, niliona mwingine anajiita eti kaka mtu anatoa onyo kwa watu kuhusu dada yake, familia ya malezi mabovu huwa mbovu hata kizazi chake pia

duh! bora usijetamani na wale wenye tamaduni za kukeketa waazirudie

I hope tatizo haliko kwenye ulinganishi wa uzuri wa miili

Watu wanawashambulia mabinti hawa kama vile wao ndio wameweka hizo picha mtandaoni.
Badala ya kusakama yule aliyezileta mtandaoni wanawasakama victims. Kweli shida ipo!

mwanakijiji
02-12-2009, 05:01 PM
duh! bora usijetamani na wale wenye tamaduni za kukeketa waazirudie

I hope tatizo haliko kwenye ulinganishi wa uzuri wa miili

Watu wanawashambulia mabinti hawa kama vile wao ndio wameweka hizo picha mtandaoni.
Badala ya kusakama yule aliyezileta mtandaoni wanawasakama victims. Kweli shida ipo!

mwenzangu ulipotea mkuu tukalikosa "duru lako"..

Unajua inaonekana hadi sasa tufikie mahali kina dada wasivue nguo zao vyumbani mwao!

Mpita Njia
02-12-2009, 06:20 PM
duh! bora usijetamani na wale wenye tamaduni za kukeketa waazirudie

I hope tatizo haliko kwenye ulinganishi wa uzuri wa miili

Watu wanawashambulia mabinti hawa kama vile wao ndio wameweka hizo picha mtandaoni.
Badala ya kusakama yule aliyezileta mtandaoni wanawasakama victims. Kweli shida ipo!

Kwani hizi picha ziliingiaje mtandaoni?

duru langu
02-14-2009, 04:10 AM
Kwani hizi picha ziliingiaje mtandaoni?

Naamini kabisa si hao mabinti walioweka hizo picha zao.
Huyo mtu mwengine aliyeziweka aulizwe yule jamaa anayejing'ata
ulimi kwa sukari

duru langu
02-14-2009, 04:15 AM
mwenzangu ulipotea mkuu tukalikosa "duru lako"..

Unajua inaonekana hadi sasa tufikie mahali kina dada wasivue nguo zao vyumbani mwao!

Nipo mkjj mihangaiko tuu. Mtaani kwetu transfoma ililipuka
jumamosi iliyopita na leo ndio jamaa wameirekebisha.
Bongo kazi kweli kweli :-(

Pia watu watadai ule utamaduni wa watu kudinyana
:o gizani urudi vinginevyo mmoja shurti ageuke upande wa
pili au afumbe macho ili mwenza apate nafasi ya kuingia shukani.