PDA

View Full Version : Kweli UDSM imetushinda?

mwanakijiji
01-19-2009, 05:21 PM
Wakati mwingine hata kushangaa mtu huwezi. NI kwa miaka mingapi tumesikia na kushuhudia haya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu mlimani kugongana na serikali? Imekuwa kama kibwagizo cha wimbo usiokwisha. Leo kwa mara nyingine tena wanafunzi wanne wamekamatwa ikiwa ni siku ya wanafunzi kurudi tena chuoni baada ya kundi kubwa kutimuliwa kufuatia mgomo wako mwishoni mwa mwaka jana.

Jambo la kujiuliza ni hivi kweli katika Tanzania hakuna mtu mbunifu na mwenye uwezo wa kutatua au kutafuta ufumbuzi muafaka na wa kudumu wa matatizo ya Mlimani? Wataendelea kukamatana, kugoma, kutishiana, kufukuzana hadi lini?

Matigari
01-22-2009, 04:53 PM
Hivi tatizo hasa nin nini ( yaani shina la tatizo siyo hizo ishara kama mikopo etc) Who owns the University? Je bado kipo chini ya serikali?

Kwa nini kisipewe consortium fulani kukiendesha?

Can it be run profitably?

Nadhani tatizo linaweza kuwa mgongano kati tya profit motive ya chuo ( kama kinategemea kupata faida through ada ya wanafuzi) na kutoa huduma bora kwa wanafunzi. Tafadhalini wanakijiji nifumbueni macho.

Hekima ni Uhuru.

mwanakijiji
01-22-2009, 05:38 PM

yaani sijawahi kuona mahali ambapo panatumia nguvu sana kuendesha kama UDSM... yaani akili imekwenda likizo!

ROY G BIV
01-23-2009, 08:02 AM
Wakati mwingine hata kushangaa mtu huwezi. NI kwa miaka mingapi tumesikia na kushuhudia haya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu mlimani kugongana na serikali? Imekuwa kama kibwagizo cha wimbo usiokwisha. Leo kwa mara nyingine tena wanafunzi wanne wamekamatwa ikiwa ni siku ya wanafunzi kurudi tena chuoni baada ya kundi kubwa kutimuliwa kufuatia mgomo wako mwishoni mwa mwaka jana.

Jambo la kujiuliza ni hivi kweli katika Tanzania hakuna mtu mbunifu na mwenye uwezo wa kutatua au kutafuta ufumbuzi muafaka na wa kudumu wa matatizo ya Mlimani? Wataendelea kukamatana, kugoma, kutishiana, kufukuzana hadi lini?

Kwani hapa si ndio tunaambiwa kuna wasomi waliobobea? Inakuwaje matatizo hayaishi?

Nziku
01-23-2009, 08:43 AM
Kwani hapa si ndio tunaambiwa kuna wasomi waliobobea? Inakuwaje matatizo hayaishi?

kwasababu ya mkono wa Serikali kuu

Matigari
01-23-2009, 10:10 AM
Kwani hapa si ndio tunaambiwa kuna wasomi waliobobea? Inakuwaje matatizo hayaishi?

Kuwa msomi aliyebobea na kuwa na uwezo wa organization ni vitu viwili tofauti. Unaweza ukawa unapata maksi mia kwa mia lakini vitabu vyako wakati mwingine hata hujui viko wapi. Mimi nadhani kama tuna mapenzi na chuo ni kutafuta kwanza nini kiini cha tatizo halafu tukashauri jinsi ya kutengeneza strategy. Nimeingia kwenye website yao, hakuna mahali popote panapoeleza kinachoendelea ( kwa mfano, kutuarifu alumni kuwa kuna mgomo na chuo kimeuelewa vipi huo mgomo, au kusimamishwa shule kwa baadhi ya wanafunzi) Nimeingia kwenye alumni site pia kuna vingi ambavyo wangeweza kufanya kuanzisha mjadala ( perhaps a forum) ili watu wengine wachangie.

The site was not very user friendly, kwa mfano sikuona urahisi wa kuregister kama alumni i ili niweze kutoa mchango wangu wa hali.

Bado ninaamini kuwa tatizo lipo katika kutokuwa na uwiano kati ya tuition na service zinazotolewa.

Hekima ni Uhuru.

Nziku
01-23-2009, 11:27 AM
Hekima ni Uhuru.

tehe tehe .... nadhani hii moto haifanyi kazi kwasasa.

Matigari
01-23-2009, 04:34 PM
tehe tehe .... nadhani hii moto haifanyi kazi kwasasa.

Ni jukumu la alumni kuhakikisha kuwa inafanya kazi na kuirudisjia hadhi iliyokuwepo. Sijui campuslife ikoje. Mtakumbuka wakati ule kulikuwa na panel discussions hosted by students etc. Sijui kama wanafuzi wana muda wa kuorganize hivyo vitu, ukiangalia kuwa muda mwingi unatumika kuhakikisha kuwa masuala yao yanasikilizwa; sijui wallimu na wanataaluma wengine wanafanyaje kazi zao za kila siku kama kuna interruption za mafunzo kila wakati .

Hekima ni Uhuru.

mwanakijiji
01-23-2009, 04:47 PM

yaani kila mwaka ni migomo, kufukuzana, masharti mapya ya kurudi chuoni, migomo, kufukuzana, n.k Huwa najiuliza kama VYuo vikuu vimegeuka kuwa vyoo vikuukuu!!

Matigari
01-23-2009, 05:30 PM
yaani kila mwaka ni migomo, kufukuzana, masharti mapya ya kurudi chuoni, migomo, kufukuzana, n.k Huwa najiuliza kama VYuo vikuu vimegeuka kuwa vyoo vikuukuu!!

Jambo mzee.

Hapana siyo vyoo vikuu, matatizo yanayotokea Dar. sasa ni ya kawaida kwa chuo chochote kinapotoka kuwa totally supported na Govt. na kuanza kujiendesha chenyewe ( japo partial kujiendesha) kama tumekubaliana kuiendesha nchi kibepari ( kitu ambacho nadhani ndiyo kinaendelea) Kuna maamuzi mengi makali ambayo yanatakiwa kufanywa. Kama kuanzisha endowments, kushirikiana na mashirika na makampuni binafsi ili kukusanya pesa na hata kustreamline mishahara ya wanataaluma,. Si tunafahamu kwa mfano nchi za ugaibuni unaweza ukakuta waalimu wawili wenye elimu sawa na wanafundisha kozi moja, mmoja anaweza akawa anapata mshahara mkubwa kuliko mwingine, kisa anayepata mshahara mkubwa anakuwa anaingiza pesa nyingi chuoni kutokana na uwezo wake wa kuingiza research grants hivyo kukiletea chuo pesa. Hivyo structure nzima ya mapato na matumizi ya chuo itabidi yaangaliwe upya.

Taizo la mlimani litaendelea tu kama chimbuko la tatizo halitafutwi na kufanyiwa ukarabati unaostahili.

Hekima ni Uhuru