PDA

View Full Version : Mdahalo: Kuishi kwa kipato chako



mwanakijiji
01-21-2009, 08:53 AM
Ni vigumu kwa mfanyakazi wa Tanzania anayepokea mshahara kuweza kuishi kwa kutegemea kipato hicho cha kila mwezi na kuweza kutimiza mahitaji yake yote. HIvyo mfanyakazi huyo analazimika kutumia ujanja ujanja na mbinu mbalimbali kujiongezea kipato hata ikibidi kwa kuvunja sheria (rushwa n.k) au kupinda sheria (kujipangia per diems, na viposho vya kila aina). Mtu huyo tuelewe analazimika kufanya hivyo na tusimchukulie kuwa ni mvunja sheria au fisadi. Inatupasa tumwelewe.

QUTE
01-25-2009, 07:07 PM
M'KJJ wafanyakazi wote tunaolipwa mishahara ya kawaida tunaweza kuishi kwa kipato chetu i mean kuanzia kima cha chini mpk cha kati. wanaoshindwa kuishi kwa kipato chao ni wale wote wanaolipwa mishahara mizuri na ambao wana uwezo wa kujitengenezea visafari na per diem na kinachowasumbua ni tamaa na maisha ya juu ambayo yako nje ya uwezo wao, wanajikuta kwamba ndani ya siku kumi mshahara umeisha ndio hapo inabidi aanze kuandaa per diem, ili apate za kumuwezesha kumalizia mwezi

lakini kama ww ni mfanyakazi wa kawaida huna chanzo chochote cha kuongeza salio lako inabidi ujipange vizuri na mshahara wako kwa kujua kuwa ukiishia katikati ya mwezi basi ujue itakuwa imekula kwako, na asikwambie mtu tunajua kupanga bajeti yetu na mishahara yetu hiyo hiyo midogo

ChingaMzalendo
01-25-2009, 10:12 PM
trying to ask a question

mwanakijiji
01-29-2009, 12:39 AM
Ni vigumu kwa mfanyakazi wa Tanzania anayepokea mshahara kuweza kuishi kwa kutegemea kipato hicho cha kila mwezi na kuweza kutimiza mahitaji yake yote. HIvyo mfanyakazi huyo analazimika kutumia ujanja ujanja na mbinu mbalimbali kujiongezea kipato hata ikibidi kwa kuvunja sheria (rushwa n.k) au kupinda sheria (kujipangia per diems, na viposho vya kila aina). Mtu huyo tuelewe analazimika kufanya hivyo na tusimchukulie kuwa ni mvunja sheria au fisadi. Inatupasa tumwelewe. Unakubaliana na mtazamo huu au unaupinga? na kwanini?