mwanakijiji
01-21-2009, 05:13 PM
Taarifa kutoka Arusha zinasema kuwa kuna magari kama matano yametumbukia katika mto Nduruma nje kidogo ya mji wa Arusha. Kw amujibu wa vyanzo vyetu ajali hiyo imesababishwa na lori la Coca Cola kugongana na magari mengine madogo na kusababisha magari hayo kutumbukia mtoni na mengine kuning'inia kwenye kingo ya mto huo. Hadi hivi sasa kuna watu kadhaa waliofariki na wengine kujeruhiwa. Tutawaletea taarifa kamili hivi punde.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Bw. Robert Boaz ameiambia KLHN kuwa ajali hiyo imetokea mchana wa leo kwenye barabara ya Arusha Moshi ambalo semi-trailor iligonga basi ambalo nalo likagonga magari mengine madogo. Hadi hivi sasa Bw. Boaz amethibitisha kuwa waliofariki ni watu 16 miongoni mwao ni wanaume 10 na kina mama 6.
Bw. Boaz amesema kuwa walifika eneo la ajali mara moja ambapo waliweza kupata msaada wa wananchi kutoa miili ya marehemu na kuwasaidia majeruhi na kuwakimbiza katika hospitali za Arusha kwa matibabu. "Wananchi wametupatia ushirikiano mkubwa" alisema Bw. Boaz.
Alipoulizwa kuhusu chanzo cha ajali Bw. Boaz alisema kuwa hadi hivi sasa uchunguzi unaendelea ingawa alitoa ushauri kuwa madereva na watumiao vyombo vya usafiri kuwa wanaozinggatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali nyingine ambazo kwa kweli si za lazima.
Hii ni ajali kubwa ya tatu kutokea nchini tangu mwaka huu mpya uanze. Ajali moja kubwa nyingine ilitokea karibu wiki moja na kitu iliyopita ambapo watu 27 walikufa baada ya basi la Tashrif kugonga lori la magogo lililokuwa limeegeshwa pembezoni maeneoo ya Hale kwenye barabara ya kuelekea Tanga (Muheza - Segera).
Ajali hiyo ya basi ilitanguliwa na ajali iliyotokea huko Himo Moshi ambapo watu 11 wa familia moja walipoteza maisha yao Januari 4 wakiwa wanarudi kutoka kwenye sherehe za Ubarikio. Basi dogo la (hiace) nalo liliparamia lori lililokuwa limeegeshwa pembezoni.
Ajali za namna hii zimekuwa zikitokea mara kwa mara huku serikali na vyombo vya usalama vikitupa lawama nyingi kwa madereva na watumia barabara wengine kuwa waangalifu wakiwataka wafuate sheria za usalama barabarani.