View Full Version : Hodi Kijijini!!!!
Mwipagi
01-22-2009, 08:42 AM
Na mimi naomba hifadhi katika Kijiji hiki japo ni kuku mgeni kweli,tena mwenye kamba ya katani.
mwanakijiji
01-22-2009, 08:47 AM
Na mimi naomba hifadhi katika Kijiji hiki japo ni kuku mgeni kweli,tena mwenye kamba ya katani.
karibu sana Mwipagi.. jisikie uko kijijini.. chagua cha kunywa..
Quemu
01-23-2009, 12:58 AM
Na mimi naomba hifadhi katika Kijiji hiki japo ni kuku mgeni kweli,tena mwenye kamba ya katani.
Karibu Bw. Mwipagi.
Usalama wa hapa kijijini ni wa hali ya juu. Yaani unaweza kuacha mlango wa zizi la ng'ombe zako, na ukaamka asubuhi kukuta idadi ile ile. Kuku hapa ni wakijiji. Kwa hiyo ukiona kuku barabarani; wewe kamata, chinja, na kula.
Kitu cha kuzingatia hapa kijijini haturuhusu utupaji wa takataka hovyo. Mkokoteni wa kuchukua takatakata unapita kila Jumanne na Ijumaa. Kwa hiyo hakikisha unakusanya takataka zako kwenye pipa. Wasiliana na mzee wa kijiji kuweza kupata hilo pipa.
Onyo: mwaka huu ni zamu yangu kuangua mabuyu kwenye ule mbuyu wa kijiji. Kwa hiyo chonde chonde naomba usiyaangue. Kuweza kupangiwa zamu yako, wasiliana na mzee wa kijiji.
Ni hayo tu mwanakijiji wetu mpya.
Mwipagi
01-24-2009, 12:28 PM
karibu sana Mwipagi.. jisikie uko kijijini.. chagua cha kunywa..
Ahsanteni wenyeji wangu,nilikuwa nazunguka kijijini kutafuta ulanzi au kangara ili nikate kiu! Si unajua tena nilikotoka jua kali kweli,naam nimekaa chini ya mti nakunywa taratiibu
Mwipagi
01-24-2009, 12:33 PM
Karibu Bw. Mwipagi.
Usalama wa hapa kijijini ni wa hali ya juu. Yaani unaweza kuacha mlango wa zizi la ng'ombe zako, na ukaamka asubuhi kukuta idadi ile ile. Kuku hapa ni wakijiji. Kwa hiyo ukiona kuku barabarani; wewe kamata, chinja, na kula.
Kitu cha kuzingatia hapa kijijini haturuhusu utupaji wa takataka hovyo. Mkokoteni wa kuchukua takatakata unapita kila Jumanne na Ijumaa. Kwa hiyo hakikisha unakusanya takataka zako kwenye pipa. Wasiliana na mzee wa kijiji kuweza kupata hilo pipa.
Onyo: mwaka huu ni zamu yangu kuangua mabuyu kwenye ule mbuyu wa kijiji. Kwa hiyo chonde chonde naomba usiyaangue. Kuweza kupangiwa zamu yako, wasiliana na mzee wa kijiji.
Ni hayo tu mwanakijiji wetu mpya.
Nimekupata mkuu,nitajitahidi kutokutupa takataka ili nisije tupiwa mizigo bure,lakini kwakuwa wewe umeamua kujimilikisha ule mbuyu,wacha mimi niende kwenye mapera na mafenesi ili nikaponee huko.
Kuleni kwa size jamani . matunda pori ni matamu lakini ukivimbiwa( ukizidisha kiasi mmmmhhh) panakuwa [pagumu
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.