dRU
01-22-2009, 01:24 PM
Kwa mantiki ya waraka huu, nitatumia tafsiri ya neno SIASA kama lilivyo andikwa kwenye Wikipedia, kamusi elezo huru ? kwamba ?Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika taifa, mji au hata dunia mzima (siasa ya kimatatifa). Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu?.
Takriban watu wote ndani ya maisha yao ya kila siku huguswa na SIASA ama kwa namna moja ama nyingine, hili si geni na hakika halina mjadala maana katika kila kona ya maisha patakuwepo na mjadala wa KISIASA.
Panapotokea mjadala (majadiliano) kati ya kundi moja na jingine ama baina ya mtu mmoja na mwingine, makubaliano ama kutokubaliana na maamuzi ama hoja, huwa havikosi nafasi katika uga kama huu. Asilani, hapa si pahala pa msema pweke kwamba hakosei!!. Si vibaya kujikumbusha kwamba hapa si pahala pa kutafuta nyingi nasaba na hatima ya kufikwa mwingi msiba. Maana haya tumeyaona na bado yatazidi kuonekana ndani ya hii mijadala yetu ya KISIASA.
Ni hivi karibuni tu tumeanza kuona mwelekeo mpya wa mijadala huria ya KISIASA, pale ambapo Chama Cha Mapinduzi kimepata mbadala ama mwenza wa kuwa adui nambari wani wa CUF. (?CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeendelea kukishambulia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisema chama hicho hakina nia ya dhati ya kuwakomboa wananchi kwa vile viongozi wake hawana historia nzuri ya kutetea wananchi.? ?
?Awali, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho, Abdul Kambaya, alisema baada ya Chadema kuonyesha kuwa hawataki siasa za kweli, hivi sasa chama chake kinawahesabu kuwa ndiyo maadui zao namba moja pamoja na CCM.).
Sitegemei kwamba hili litaishia hapa maana bado tuna vyama vya SIASA vingi kwa uwingi wa idadi hapa nchini kwetu. Uwezekano upo wa baadhi kutafuta ?MUUNGANO? na vingine kujimega na kurusha tuhuma za kutodendewa haki kwenye majukwaa na baadhi ya vyama vingine ?ukiondoa? ama kujumlisha na Chama tawala (CCM). ? Ninasema hivi kwa sababu siku za nyuma ilikuwa ni CCM ndiyo yenye kutupiwa makombora kutoka kwenye viringe vya SIASA ? na sasa hali inonyesha kuwa tofauti na zamani, sasa makombora yanakwenda mchanganyiko kwa wote na hasa vyama ambavyo vina idadi kubwa ya wanachama nchini.
Haya maji yetu tutayakoga na ikibidi kuzama basin a tuzame huku tukiyashika maana huo ndiyo uzalendo ni kama kusema mume wa mama ni baba!!! Na tuwe waangalifu katika mijadala hii wahenga walisema Mwapiza la nje hupata la ndani.