PDA

View Full Version : Je serikali ya CCM ni safi?

mwanakijiji
01-22-2009, 07:21 PM
Ukisikia mtu anasema (awe mwanasiasa au vinginevyo) kuwa CCM ni "safi" unakubaliana naye au utampinga? Je yawezekana kuwa na "baadhi" ya watu wachafu bila kukichafua chama?

mfumwa
01-22-2009, 10:55 PM
Ukisikia mtu anasema (awe mwanasiasa au vinginevyo) kuwa CCM ni "safi" unakubaliana naye au utampinga? Je yawezekana kuwa na "baadhi" ya watu wachafu bila kukichafua chama?

Inategemea uwingi wa hao wachafu, ama huo uchafu. Manake CCM sio chama cha Malaika, na hata vyama vya upinzani (CUF, CHADEMA, NRA, TLP, CHAUSTA, NCCR nk) navyo vina watu wachafu manake si vyama vya Malaika. Lakini kwa kuwa CCM ndio chama tawala, tukipima utekelezaji wa sera zake, utakuta kuwa bado wameshindwa kuzitekeleza sera zao mpaka wale maadui wetu ujinga, maradhi, na njaa bado wapo. Pia pengo kati ya walionacho na walalahoi linazidi kuongezeka siku hadi siku.

mwanakijiji
01-22-2009, 11:43 PM

Mfumwa.. uchafu kwa kawaida huwa unatabia ya kuvutia uchafu zaidi.. uchafu hauvutii usafi.

mfumwa
01-23-2009, 12:05 AM
Mfumwa.. uchafu kwa kawaida huwa unatabia ya kuvutia uchafu zaidi.. uchafu hauvutii usafi.

Ni kweli, ninakubaliana nawe. Mtu msafi kuja kupata uongozi mkubwa CCM ni kazi kubwa. Wanajuana wenyewe nani anaweza tunza maslahi yao. Lakini na hivi vyama pinzani navyo vina matatizo, angalia mfano sasa wanatumia nguvu kubwa kutupiana lawama. Wakati huu ndio tunaelekea kwa uchaguzi. Wapinzani wangeweza kuungana, wananchi wako tayari, mfano si lazima kujitahidi kupata uRais, wangeweka nguvu kwa wabunge na kuachiana maeneo, wabunge wa upinzani wakiongezeka Bungeni. Sauti yao itasikika, na hiyo italeta chachu zaidi kwa wananchi.

mwanakijiji
01-23-2009, 12:16 AM

Unajua hadi hivi sasa sijaona upinzani halisi, ukiondoa mtu mmoja mmoja. Bado hatujawa na upinzani kwa sababu zaidi wako katika hatua ya kutafuta mwelekeo.

ilongo
01-23-2009, 10:28 AM
Ni kweli, ninakubaliana nawe. Mtu msafi kuja kupata uongozi mkubwa CCM ni kazi kubwa. Wanajuana wenyewe nani anaweza tunza maslahi yao. Lakini na hivi vyama pinzani navyo vina matatizo, angalia mfano sasa wanatumia nguvu kubwa kutupiana lawama. Wakati huu ndio tunaelekea kwa uchaguzi. Wapinzani wangeweza kuungana, wananchi wako tayari, mfano si lazima kujitahidi kupata uRais, wangeweka nguvu kwa wabunge na kuachiana maeneo, wabunge wa upinzani wakiongezeka Bungeni. Sauti yao itasikika, na hiyo italeta chachu zaidi kwa wananchi.

Tanzania tuna upinzani kweli ama ni waganga njaa tu hao ... hebu ona wale tuliowaamini na ile "list of shame" wanavyotugeuka sasa baada ya kuona ndugu zao wanapelekwa Kisutu!!

Mwipagi
01-24-2009, 12:43 PM
Ukisikia mtu anasema (awe mwanasiasa au vinginevyo) kuwa CCM ni "safi" unakubaliana naye au utampinga? Je yawezekana kuwa na "baadhi" ya watu wachafu bila kukichafua chama?

Wenyewe wanakuambia mambo ya mtu binafsi yasijumulishe katika Chama,ajabu ni kwamba hao hao ambao ndio wachafu (mtu binafsi) ndio wanaheld key positions tena za maamuzi makubwa katika Chama.Ukistaajabu ya Musa.................

Mwipagi
01-24-2009, 12:50 PM
Ni kweli, ninakubaliana nawe. Mtu msafi kuja kupata uongozi mkubwa CCM ni kazi kubwa. Wanajuana wenyewe nani anaweza tunza maslahi yao. Lakini na hivi vyama pinzani navyo vina matatizo, angalia mfano sasa wanatumia nguvu kubwa kutupiana lawama. Wakati huu ndio tunaelekea kwa uchaguzi. Wapinzani wangeweza kuungana, wananchi wako tayari, mfano si lazima kujitahidi kupata uRais, wangeweka nguvu kwa wabunge na kuachiana maeneo, wabunge wa upinzani wakiongezeka Bungeni. Sauti yao itasikika, na hiyo italeta chachu zaidi kwa wananchi.

Mfumwa,njaa ni kitu kibaya sana,hiyo migogoro na lawama zilizojitokeza sasa hivi ni strategic plan za wajanja wachache ambao wanafaidika,I can assure you,wapo kazini.

Tom
01-26-2009, 06:58 PM
Ni kweli, ninakubaliana nawe. Mtu msafi kuja kupata uongozi mkubwa CCM ni kazi kubwa. Wanajuana wenyewe nani anaweza tunza maslahi yao. Lakini na hivi vyama pinzani navyo vina matatizo, angalia mfano sasa wanatumia nguvu kubwa kutupiana lawama. Wakati huu ndio tunaelekea kwa uchaguzi. Wapinzani wangeweza kuungana, wananchi wako tayari, mfano si lazima kujitahidi kupata uRais, wangeweka nguvu kwa wabunge na kuachiana maeneo, wabunge wa upinzani wakiongezeka Bungeni. Sauti yao itasikika, na hiyo italeta chachu zaidi kwa wananchi.

Kuungana kwa vyama ni dhana nzuri pale ambapo kuna benefits, kuaminiana na kila chama kinachokuja kwenye umoja kina nguvu fulani. Tuache kukariri mambo. Kuungana kwa vyama Kenya kulikuwa na benefit kwasababu vilikuwa na political base. Hivi vya kwetu karibia vyote ni vyama vya idara ya habari maelezo (vya Dar). Mfano ,2005 ni wapi ambapo vyama vingeungana vingepata wabunge zaidi?

Vyama vingine vinatumiwa tu kuvuruga vingine. Unawezaje ukaelezea kauli ya mbatia kuhusu ufisadi (kama vyombo vya habari vilivyo ripoti)? au mambo ya kifo cha wangwe na yaliyotokea tarime? Unaweza ukaunganisha kura za cuf, tlp na nccr mageuzi huku bara ukashinda ubunge? Unawezaje ukaelezeaje pingamizi la cuf huko mbeya dhidi ya CHADEMA?

mfumwa
01-26-2009, 07:35 PM

Unadhani kuungana kwa vyama ni kupata Ubunge tu, wanaweza kuanzia katika udiwani na wenyeviti wa vijiji/mitaa. Kuanzia huko wanapanda taratibu. Lakini kuungana sio ushindi, bali ni mojawapo ya njia za ushindi. Na kuungana sio kwa uchaguzi tu, bali kwa kudai jambo muhimu sana la kusukuma mageuzi Tanzania. Nalo ni kudai Katiba, ili humo sheria za uchaguzi ziboreshwe, na kupatikane tume huru.

Hawawezi dai yote haya kama hawatakuwa wamoja. Hivi kweli tume ichaguliwe na chama tawala, hapo unategemea upinzani kufanya vizuri. Hivyo wakiungana (neno zuri kushirikiana) hata watapanga mikakati ya kwenda vijijini kutoa elimu ya uraia ili watu wengi waelewe haki zao, na ndio itakuwa mwanzo wa mabadiliko ya kweli. Lakini kama kila chama kitasimama kivyake, ili tu kiweze kupata wabunge wengi, na kupata wabunge ni kuongeza ruzuku itolewayo na Serikali, hatufiki kokote.