View Full Version : NSSF na Vifo Tabora
Ach-F
11-09-2008, 10:42 PM
Baada ya watoto 19 kufa kwa uzembe wa NSSF, Dr. Dau anaendelea kula kuku tu kama vile hao waliokufa ni kuku tu na sio binadamu. Tuliona yalipotokea mauaji Mwanza waziri wa mambo ya ndani wakati huo Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliachia ngazi.
Ni lini Tanzania itabadilika. Dr.Dau hujaona CHANGE iliyotokea marekani? Jakaya Kikwete kama huyu kiongozi alipewa dhamana na hawezi kutimiza wajibu wake kwa nini anaendelea kuwepo pale? Utachukua hatua tu pale marafiki zako wanapofanya makosa? Tuliona jinsi ulivyoweza kumlinda kipenzi rafiki yako Dito lakini mauti yalimkuta tu. Huu ni wakati wa kubadilika na sio kulindana.
mwanakijiji
11-10-2008, 07:04 AM
Hapa umenikumbusha lililotokea Haiti ambapo watoto karibu themanini wamekufa baada ya jengo la shule yao kuwaangukia kwa sababu limejengwa vibaya. Nasikia "mmiliki" wa jengo hilo keshafikishwa kizimbani.
Ach-F
12-06-2008, 04:27 PM
Watoto 19 wamekufa serikali ya Tanzania imekaa kama Bubu hawataki kusema chochote.Je tusubiri wengine 10 wafe ndio tuone uwajibikaji? Je, Dr. Dau amemlipa JK na serikali yake kuwa mabubu?
Mr. XXX
12-07-2008, 08:08 PM
Vifo vya Tabora ni bahati mbaya iliyotokea. Tukubali hilo na tuendelee kuenzi kumbukumbu ya watoto hao. Kuendelea kuwahusisha kina Dr. Dau ni kuwaharibia nafasi zao huko mbeleni kwani ninavyojua Dr. Dau anataka kuja kugombea huko mbeleni au kuteuliwa katika nyadhifa fulani ya kisiasa.
Ach-F
12-07-2008, 09:37 PM
Vifo vya Tabora ni bahati mbaya iliyotokea. Tukubali hilo na tuendelee kuenzi kumbukumbu ya watoto hao. Kuendelea kuwahusisha kina Dr. Dau ni kuwaharibia nafasi zao huko mbeleni kwani ninavyojua Dr. Dau anataka kuja kugombea huko mbeleni au kuteuliwa katika nyadhifa fulani ya kisiasa.
Bahati mbaya mara ngapi? Huko NSSF ndio nyumbani kwa kufuja pesa za walipa kodi na baadaye utaambiwa kwenye pensheni nako mfuko umetoboka. Asiachiwe huyu kujiona kama yeye ni mola kwa uzembe wake.
Kama ameshindwa kuwajibika kwa jambo dogo kama hili ataweza kuhimili mikiki mikiki ya kuongoza Watanzania millioni 40? Hatuhitaji viraka vya namna hii!
Ach-F
12-08-2008, 01:21 AM
Umeona Ugiriki baada ya polisi kufyatua risasi na kumuua kijana aliyewatupia mawe wakati wakiwa katika doria moto unawaka huko, sisi vijana kumi na tisa hakuna anayeshituka inakuwaje mauaji kama haya ya kikatili tuko kimya na wakuu wa NSSF wanaendelea kula kuku kwa mrija?
Fresh riots erupt in Greek cities (http://news.bbc.co.uk/2/hi/europe/7770086.stm)
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.