PDA

View Full Version : News Alert: ATCL waanza kupanguliwa

mwanakijiji
01-24-2009, 08:26 PM
Habari zinazoingia kutoka Dar zinadokeza kuwa watendaji mbalimbali wa ATCL wameanza kupanguliwa. Hata hivyo hatujajua hasa kama wanapanguliwa kwa sababu wanahamishwa au wanatimuliwa na wengine kupewa nafasi ya "ulaji' badala ya kulitumikia shirika.

Wanaotarajia kuwekwa pembeni ni pamoja na: Mark Manji, Eliaseph, na David Mattaka!

pundamilia
01-25-2009, 12:51 AM
As I said earlier, kuruka kwa ndege ni mwanzo tu wa kutatua matatizo yaliyopo katika ATCL. Na niliendelea kwa kuongeza kuwa ndani ya Miezi mitatu ninatarajia Mh Rais atakuwa ameendelea kutatua matatizo mengine yaliyobaki ndani ya ATCL.
Tuendelee kuvuta subira

Atubonekisye Massapa
01-26-2009, 02:38 PM
Wamesahau mataka alivyolishughulikia shirika la NPF (sasa NSSF)? Wasipoangalia huyu bwana atuliza tena na tena.

Janjaman
01-26-2009, 05:19 PM
Ndugu Massapa, David Mattaka alikuwa Director General wa PPF na sio NSSF.

mfumwa
01-26-2009, 05:41 PM
Habari zinazoingia kutoka Dar zinadokeza kuwa watendaji mbalimbali wa ATCL wameanza kupanguliwa. Hata hivyo hatujajua hasa kama wanapanguliwa kwa sababu wanahamishwa au wanatimuliwa na wengine kupewa nafasi ya "ulaji' badala ya kulitumikia shirika.

Wanaotarajia kuwekwa pembeni ni pamoja na: Mark Manji, Eliaseph, na David Mattaka!

Mabadiliko tu yanaweza yasiwe chanzo cha kuikoa ATC. Manake lazima tuangalie na hao wapya watakaoletwa. Kweli inatakiwa ipatikane timu yenye utashi wa kuliokoa lile shirika, ni aibu nchi kushindwa kuwa na shirika imara la ndege. Hata Precision Air wanajitahidi kuishinda ATC. Muda utajibu...

Mpita Njia
01-27-2009, 10:23 AM
Ni vema serikali ikachana kabisa na biashara hii ya ATCL. Kwa kuwa wanasema kuwa shirika haliwezi kuuzwa hivi sasa kutokana na hali lilivyo, nashauri serikali izungumze na Precision, iwapo ATCK kwa makubaliano ya serikali ya kuwa hisa kadhaa katika shirika jipya litakaloundwa na Precision baada ya kuiunganisha na ATCL

dickabudi
03-03-2009, 11:53 AM
1.Kumbuka Precision ni Mbia na Kenya Airways na anaujutia mkataba mbovu aliyouingia na KQ

2. Kuna ukaribu sana wa Precision Air na Basil Mramba siku ya siku msije mkaona serikali imekumbatia mafisadi, na hapo ndipo ujue uzuri na ubaya wa Basil Mramba maaana ni Thinktank na policy maker wa Precision Air na ndiye ameiweka PW hapo ilipo

Mpita Njia
03-03-2009, 01:00 PM

Hivi, kama Precision wakiichukua ATCL kwa clean deal na kufanikiwa kuigeuza na kuwa shirika linalojiendesha kwa faida, kuna ubaya wowote hata kama Mramba ni sehemu ya PA?

dickabudi
03-03-2009, 01:08 PM
Unaiangalia PW kwa nje ukiona ndege zipo angani na wenye mali wanaoza watoto kifahari unaona PW wanafanya vizuri, si kweli wana matatizo mengi wana hasara kubwa na wana mikataba mibovu sana haina manufaa kwa nchi

Ni wale waliofukuzwa na Mwalim kwa kununua ndege mbovu za George Hallack mpalestina tapeli duniani Mzee

Mpita Njia
03-03-2009, 02:07 PM

Ndio maana nikazungumzia clean deal, si hayo mazabemazabe.

dickabudi
03-03-2009, 02:33 PM
Mpitianjia kweli unaweza kufanya clean deal na mtu aliyezoea dirty deals?

Cheblack Mpingo
03-03-2009, 04:15 PM
Hawa lashapewa fedha za walipa kodi hapo awali sasa mtu anapowapangua saa hizi sijui tumuelewe je? sialitakiwa awapangue kabala ya kuchezea hizo fedha za walipa kodi wa tanzania?

dickabudi
03-04-2009, 02:27 PM
Mimi naomba kutafakari yafuatayo

Mh Mataka alifukuzwa kazi na Rais Benjamin Mkapa, je Mkapa alimwonea au ni kweli alikuwa na makosa makubwa na adhabu aliyopewa na Rais Mkapa ilimstahili?

Baada ya hapo amerudije kuongoza shirika jingine la umma, nani kampendekeza kwa Mh Rais Kikwete? Kwa nini Rais Kikwete amemteua mtu aliyefukuzwa kazi na Rais aliyetangulia

Kijijni kitafakari haya kwa mapana na marefu tutaona kwamba ama anastahili kuwa Mkuu wa Shirika au amebebwa

Mpita Njia
03-04-2009, 04:33 PM
Mpitianjia kweli unaweza kufanya clean deal na mtu aliyezoea dirty deals?

Hatuwezi kuwabana wakafanya mambo yanavyotakiwa? Kama tutashindwa kuwabana, kwa nini tusionyeshe kuwa tunakerwa kwa kuwashughulikia kisawasawa watu hawa.

dickabudi
03-04-2009, 04:49 PM
Tujadili haya Mpitanjia tuachane na ATCL na PW maana wakati ATC inaingia ubia na SA nao walibid wakashindwa

Mh Mataka alifukuzwa kazi na Rais Benjamin Mkapa, je Mkapa alimwonea au ni kweli alikuwa na makosa makubwa na adhabu aliyopewa na Rais Mkapa ilimstahili?

Baada ya hapo amerudije kuongoza shirika jingine la umma, nani kampendekeza kwa Mh Rais Kikwete? Kwa nini Rais Kikwete amemteua mtu aliyefukuzwa kazi na Rais aliyetangulia

Kijijni kitafakari haya kwa mapana na marefu tutaona kwamba ama anastahili kuwa Mkuu wa Shirika au amebebwa na si kiongozi mwema wa kupewa dhamana hiyo