PDA

View Full Version : Exclusive: Dr. Mwakyembe on KLHN



mwanakijiji
01-25-2009, 03:14 AM
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/people/mwakyembe.jpg

Kesho siku ya Jumapili kuanzia majira ya saa saba za mchana (EST) sawa na saa tatu za usiku (Saa za Afrika ya Mashariki) tunatarajia kuwa na mahojiano na Dr. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kampuni ya Richmond. Ni matokeo ya Kamati hiyo ndiyo yaliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe. Edward Lowassa kujiuzulu na hatimaye Baraza la Mawaziri kuvunjika.

Tutazungumza na Dr. Mwakyembe karibu mwaka mmoja kamili tangu matukio yale ya Februari 2008, matukio ambayo yalikuwa ni ya kihistoria. Tutazungumza naye pia mambo mengine ya kitaifa saa na wakati huu ambapo Taifa letu linapitia katika mabadiliko makubwa ya kifikra.

Utaweza kusikiliza mahojitano yetu kupitia tovuti yako hii "live".

Matigari
01-25-2009, 05:03 PM
Tafadhali muulize ana mikakati gani ya kupunguza tatizo la ugonjwa wa AIDS katika jimbo lake la uchaguzi, maana takwimu zinaonyesha kuwa Kyela iko kati ya wilaya zinazoongoza kwa hili tatizo.

mwanakijiji
01-25-2009, 07:42 PM
Tafadhali muulize ana mikakati gani ya kupunguza tatizo la ugonjwa wa AIDS katika jimbo lake la uchaguzi, maana takwimu zinaonyesha kuwa Kyela iko kati ya wilaya zinazoongoza kwa hili tatizo.

takwimu gani?

omondi
01-28-2009, 04:19 PM
Link ya mahojiano hayo tafadhali!

mwanakijiji
01-28-2009, 04:58 PM
Link ya mahojiano hayo tafadhali!

Angalia kwenye Podcasts hapo juu au kwenye http://www.mwanakijiji.podomatic.com