PDA

View Full Version : Yanayojiri Bungeni

Mpita Njia
01-27-2009, 10:14 AM
Bunge ndio limeanza leo. Tunatarajia kuwa mambo kadhaa nyeti yatafikishwa wka ajili ya kujadiliwa. yapo masuala ya Richmond na jinsi serikali ilivyotekeleza mapndekezo ya Bunge, masuala ya ATCL, Kiwira, TICTS na mengine kadhaa. naomba tutumie jamvi hili kupeana yanayojiri huko.
Moja ya mambo yatakayotokea ni kuwa serikali itapeleka ombi la kuziingiza zile Bil 60 za EPA kwenye bajeti ya serikali ili ziweze kutumika kama ambavyo Kikwete aliseleza-kukopesha wakulima. lakini suala lenyewe limefichwea sana mana hata kwenye ratiba ya Bunge halijaonyeshwa wazi kuwa serikali itafanya hivyo-inaandikwa tu kwua serikali iawasilisha mpango wake. KWA NINI WANAFICHA?

mwanakijiji
01-27-2009, 10:19 AM

haya mzee tunatarajia mengi kutoka upande wenu. Hivi walisema hizo fedha zimewekwa wapi hivi sasa?

Mpita Njia
01-27-2009, 10:52 AM
haya mzee tunatarajia mengi kutoka upande wenu. Hivi walisema hizo fedha zimewekwa wapi hivi sasa?

Wala hawajasema walipoziweka, walichokuwa wameeleza tu ni kuwa zitaingizwa TIB ili zitumike kwa ajili ya wakulima

Mpita Njia
01-28-2009, 12:52 PM
Leo hii wapinzani wamefanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza nia yao ya kuyavalia njuga masuala mawili. La kwanza ni kushinikiza waziri Mkuu ajiuzulu kutokana na kauli zake dhidi ya watu wanaoua albino. Na la pili na hoja ya kudai katiba mpya. hawakutaka kufafanua kwa undani mikakati watakayoitumia wakidai kuwa kufanya hivyo ni sawa na askari anayefichua mbinu za medani vitani. lakini lililo dhahiri ni kuwa wanapanga kuwasilisha hoja Bungeni kuhusiana na masuala hayo.
Pia nadhani wamefanya mkutano huu wa pamoja kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa kambi yao haijasambaratika kama ambavyo inahisiwa.

Mpita Njia
01-30-2009, 11:26 AM
Leo hii Mzindakaya kamshukia waziri wa maliasili na utalii kwa kukiuka mazimio ya Bunge yaliyoitaka serikali kusitisha muda wa umiliki wa vitalu vya uwindaji mwaka huu. Waziri ameongeza muda huo had 2012. Mzindakaya ametoa azimio kuwa Bunge likee hilo na kuitaka serikali isitishe extension ya umiliki wa vitalu. Pia ameilaumu wizara ywa kukikumbatia chama cha wawindaji ambacho mesema kinamilikiwa na wazungu na extension ilitolewa kwa shinikizo la wazungu hao

mfumwa
01-30-2009, 11:31 AM
Leo hii wapinzani wamefanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza nia yao ya kuyavalia njuga masuala mawili. La kwanza ni kushinikiza waziri Mkuu ajiuzulu kutokana na kauli zake dhidi ya watu wanaoua albino. Na la pili na hoja ya kudai katiba mpya. hawakutaka kufafanua kwa undani mikakati watakayoitumia wakidai kuwa kufanya hivyo ni sawa na askari anayefichua mbinu za medani vitani. lakini lililo dhahiri ni kuwa wanapanga kuwasilisha hoja Bungeni kuhusiana na masuala hayo.
Pia nadhani wamefanya mkutano huu wa pamoja kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa kambi yao haijasambaratika kama ambavyo inahisiwa.

hapo katika kudai katiba ndio huwa nasema hawa jamaa wanatakiwa kuungana kuweka nguvu zao zote. Wakifanikiwa hilo mengi yatabadilika hadi tume ya uchaguzi. Na kama tume ikiwa huru, uwezekano wa wapinzani kuongezeka kwa kushinda katika chaguzi utazidi.

mfumwa
01-30-2009, 11:35 AM
Leo hii Mzuindakaya kamshukia waziriw a maliasili na utalii kwa kukiuka mazimio ya Bunge yaliyoitaka serikali kusitisha muda wa umiliki wa vitalu vya uwindaji mwaka huu. Waziri ameongeza muda huo had 2012. Mzindakaya ametoa azimio kuwa Bunge likee hilo na kuitaka serikali isitishe extension ya umiliki wa vitalu. Pia ameilaumu wizara ywa kukikumbatia chama cha wawindaji ambacho mesema kinamilikiwa na wazungu na extension ilitolewa kwa shinikizo la wazungu hao

Kama Bunge lilishapitisha kusitisha muda wa umiliki mwaka huu, Waziri anapata wapi nguvu kuongeza mpaka 2012. Huu ugawaji wa vitalu umepigiwa sana kelele, kuanzia kupewa kipaumbele wazungu, pia bei za kuwinda zilikuwa chini sana kulinganisha na mataifa mengine ya Afrika. Sasa walitakiwa kusitisha ili kuja na sera mpya ya kulina rasilimali zetu wakati tukiingiza mapato.

Mpita Njia
01-31-2009, 10:05 AM

Hii wizara sasa imegeuzwa kuwa shamba la bibi, kila mmoja anakuja anajichotea anakwenda zake

Mpita Njia
01-31-2009, 10:07 AM
Mzindakaya amlipua Waziri Mwangunga
Ni kwa kukiuka agizo la bunge kufuta vibali vya uwindaji

Leon Bahati, Dodoma

MBUNGE wa Kwela (CCM), Dk Christant Mzindaka, maarufu kama "mzee wa mabomu", ameibuka bungeni na kueleza kusikitishwa na uzembe uliofanywa na Waziri wa Maliasili, Shamsa Mwangunga kwa kuwaongezea muda wamiliki wa vitalu vya uwinfaji katika hifadhi za taifa kinyume na maagizo ya bunge.

Mzindakaya alitoa maelezo hayo kupitia hoja yake binafsi aliyoiwasilisha jana bungeni na kuungwa mkono na wabunge wengi

Wakati Dk Mzindakaya akisema hayo, bunge lilimkemea Waziri Mwangunga kwa kuonyesha dharau dhidi ya maazimio ya bunge yaliyomtaka kusitisha umiliki wa vitalu vya uwindaji wa kitalii mwishoni mwa mwaka jana na badala yake akawaongezea muda wawindaji hadi mwaka 2012.

Hoja ya Dk Mzindakaya, ambayo iliungwa mkono na wabunge wengi, ilikuwa inaweka wazi kuwa bunge liliamuru vibali vilivyokuwa vinatumika viishie 2009 ili kuanzia 2010 taratibu mpya zisizo za kuiba mapato ya serikali zitumike.

Mzindakaya alilieleza bunge kuwa kwa Waziri Mwangunga alipuuza maazimio ya bunge na kusikiliza ushawishi wa matajiri hao wa kigeni wanaofanya biashara na raslimali za nchi, kupitia vitalu walivyomilikishwa na hatimaye akawaongezea miaka miwili hadi 2012.

Alifafanua kuwa kulingana na taratibu za awali, Tanzania ilikuwa hainufaiki na biashara hiyo ya utalii bali wageni wanaomiliki vitalu na ndio maana bunge liliona hilo likataka hali hiyo irekebishwe.

Mwangunga aliamriwa kusimamisha vibali vilivyotolewa na wizara yake kwa wawindaji badala ya kuisha mwaka 2012 vifikie ukomo 2010, ili kuanzia hapotaratibu mpya za uwindaji zianze kutekelezwa.

Vile vile, alikemewa vikali kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuigonganisha mihimili miwili, bunge na serikali kwa maana kwamba, akiwa na madaraka ya kiserikali iliyowekwa madarakani na wananchi alipuuzia maagizo ya bunge, ambalo ni mwakilishi wa wananchi katika kutunga sheria za nchi.

Katika utetezi wake, Mwangunga aliomba radhi kwa hatua yake hiyo na kufafanua kwamba, aliona kuwa kusimamisha ghafla kwa shughuli za uwindaji, kungesababisha hasara kwa taifa na hata kuathiri biashara hiyo, hivyo akanona ipo haja ya kuwaongezea muda wafanyabiashara hao ili baada ya hapo miongozo hiyo ianze kutumika.

Alidai kuwa utoaji wa vitalu hupaswa kufanywa miaka miwili kabla ya kuanza biashara, ili kutoa nafasi ya mmiliki kutafuta wawindaji hivyo utekelezaji wa maazimio ya bunge ungeweza kulisababishia taifa hasara.

Akiomba radhi kuhusu kosa hilo, Waziri Mwangunga alijitetea kuwa hakufanya hivyo kwa kulidharau bunge bali kwa utashi wake pamoja na ushauri wa wataalamu wake.

Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa vikali na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) kwa maelezo kuwa historia inaonyesha kuwa Tanzania imekuwa ikipata hasara kubwa kupitia biashara ya utoaji wa vitalu.

Zitto alisema kumbukumbu za serikali zinaonyesha kuwa mwaka 2006, walikuwa wametarajia kukusanya Sh15 bilioni lakini walikusanya Sh7 bilioni tu.

Alikemea vikali tabia hiyo na kutaka iwe fundisho kwa wengine na kwamba, atakayefanya kosa kama hilo afike bungeni akiwa na barua ya kujiuzulu la sivyo sheria itumike ambayo ni kumfunga jela kwa siku saba.

"Kama hapa tungetekeleza kanuni kisawasawa hivi sasa waziri (Mwangunga) angepelekwa Keko (gerezani) akakae huko siku saba," alionya Zitto.

Baada ya bunge kusikiliza hoja ya Dk Mzindakaya, utetezi wa Waziri Mwanguna pamoja na mchango wa wabunge wawili, Spika wa Bunge, Samweli Sitta alilisimamisha msururu wa wabunge wengine waliokuwa wameomba kuchangia na kutaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atoe ufafanuzi.

Pinda alisema kuwa haoni sababu za wabunge kuendelea kuchangia kwa sababu kimsingi, Mwanguna aliomba bunge msamaha, ingawa kulikuwa na kasoro katika kumalizia maelezo yake.

Kwa ujumla hoja zote za Dk Mzindakaya ziliungwa mkono na katika kuhitimisha alifuta pendekeo za pili, ambacho kilikuwa kinalitaka bunge limwadhibu Mangunga.

Spika alisema kuwa barua ya wizara ya kuwaongezea muda wamiliki wa vitalu muda wake umepunguzwa badala ya kuisha 2012, utaisha 2010.

Bunge hadi jana jioni lilikuwa linajadili muswada wa sheria ya wanyamapori ambao ulipingwa vikali na wabunge wa upinzani, kwa maelezo kuwa baadhi ya vifungu viko vinawanyima haki wazawa.

Miongoni mwa kasoro hizo ni zinazokataza wananchi kuingia kwenye maeneo ya hifadhi, jambo ambalo lilielezewa kuwa ni kuzuia haki ya wakazi wa maeneo karibu na hifadhi kutofanya shughuli zozote ikiwemo kutafuta kuni au majani.

Kipengele kingine kilichoonekana kuwakera wapinzani ni cha kumtaka mtuhumiwa aliyekamatwa ndani ya hifadhi kuwa ndiye anayepaswa kuithibitishia mahakama kuwa hakutenda kosa, badala ya mpango wa kawaida ambao mlalalmikaji ndiye anayepaswa kuthibitisha katika kiwango cha kuiondolea mashaka mahakama kwamba, mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

SOURCE: Mwananchi