View Full Version : Wanakijiji mpoo??
Kavumvuli
01-27-2009, 10:36 AM
Kwa mara ya kwanza naingia kama mwanakijiji mpya!! miaka ile wageni walikuwa wakiingia kwenye mji wenyeji wanachacharika kutafuta kitoweo cha kumkaribisha mgeni, leo hii hayo bado yapo??? hebu tuone.............
ponda
01-27-2009, 11:48 AM
Nimekutumia kitoweo, anakileta mtoto, lakini sufuria langu lirudi na lisirudi TUPU.
Matigari
01-27-2009, 06:13 PM
I have sent a pie. Please enjoy.
mwanakijiji
01-27-2009, 06:26 PM
Kwa mara ya kwanza naingia kama mwanakijiji mpya!! miaka ile wageni walikuwa wakiingia kwenye mji wenyeji wanachacharika kutafuta kitoweo cha kumkaribisha mgeni, leo hii hayo bado yapo??? hebu tuone.............
karibu kabisa kavumvuli... kama unavyoona hapa kuna ukarimu wa kila namna. Miye ndiyo nimetoka kugema kidogo so kama ni mpenzi wa mnazi au ulanzi.. uchaguzi ni wako. Vinginevyo, mkuu atakupatia togwa.. karibu kijijini, mwanakijiji mwenzetu!
Karibu kavumvuli,humu hata nyama ya ulimi utapata..
Quemu
01-27-2009, 08:05 PM
Kwa mara ya kwanza naingia kama mwanakijiji mpya!! miaka ile wageni walikuwa wakiingia kwenye mji wenyeji wanachacharika kutafuta kitoweo cha kumkaribisha mgeni, leo hii hayo bado yapo??? hebu tuone.............
Kwa bahati mbaya leo nimechelewa kujihimu kwenda shambani. Ningalikuchumia mahindi japo machache. Lakini uzuri ni kwamba mwanangu Che' Junia jana jioni alirudi na samaki nchanga. Ntakuletea angalau fungu mbili....
Karibu sana.
mfumwa
01-27-2009, 11:27 PM
"Mgeni siku ya kwanza, mpe Ugali na Panzi, mtilie kifuuni, mkaribishe mgeni". Karibu sana Mwanawane.
My more
02-02-2009, 07:38 PM
Karibu kavumvuli,humu hata nyama ya ulimi utapata..
ohoooo hapo sasa
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.