PDA

View Full Version : Wapinzani wagongana Bungeni...

mwanakijiji
01-27-2009, 06:28 PM
Habari kutoka Dodoma zinadokeza kuwa ile damu mbaya ya wapinzani imezidi kujionesha Bungeni leo na hivyo kuashiria mara moja na daima kuwa wananchi hawa hawawezi kuwa pamoja tena katika ushirikiano wowote wenye maana.

Tunaendelea kufuatilia hasa ni nini kinaendelea.

Mpita Njia
01-27-2009, 06:50 PM
Mvurugano wa wapinzani linaweza kuonekana, na wka hakika linaweza kuwas jambo baya. Lakini pia, kama kuna kundi la wapinzani wenye 'akili' wanaweza kuitumia hali hii kujiimarisha. Yaliyotokea kwa upande wa wapinzani, yamedhihirisha kuwa hakukuwa na msingi mzuri wa ushirikiano au muungano. Hilo ni funzo ambalo linaweza kutumika kama moja ya misingi ya kujenga chama imara,

mwanakijiji
01-27-2009, 06:56 PM

unajua siamini kama ipo haja wala ulazima wa wapinzani kuungana. Wamepoteza muda mrefu sana (sasa miaka zaidi ya 15) kujaribu kitu ambacho wanajua hakiwezekani. Sasa sijui tatizo nini.. Ni bora kila mmoja aende kivyake vyake.

mfumwa
01-27-2009, 11:21 PM
Lakini kumbuka "umoja ni nguvu...". Kuiondoa CCM madarakani kunahitajika nguvu ya ziada, mojawapo ni hivi vyama vya upinzani kushirikiana. Kama wataendelea wenyewe kwa wenyewe kutengana, ni faida kubwa kwa CCM.

mfumwa
01-27-2009, 11:24 PM
Haya ndio maneno ya wapinzani, ila utekelezaji huwa mgumu...

Ushirikiano wa Upinzani bado upo
Halima Mlacha, Dodoma
Daily News; Tuesday,January 27, 2009 @20:00

KIONGOZI wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed ambaye ni Mbunge wa Wawi (CUF), amekanusha taarifa kwamba ushirikiano wa vyama vya upinzani katika masuala ya siasa umevunjika.

Akizungumza na gazeti hili jana, alisema taarifa hizo si za kweli na anatarajia kuitisha mkutano na vyombo vya habari ili pamoja na hoja nyingine, atoboe ukweli kuhusu suala hilo la ushirikiano.

?Si kweli eti vyama vya upinzani havishirikiani tena, ushirikiano uko pale pale, ila tu kama unataka kupata undani wa suala hili kesho (leo) nina mkutano na waandishi wa habari nitalizungumzia suala hili ukweli wake,? alisema Mohamed.

Alisema katika kikao chao cha upinzani ambacho kilifanyika jana, walijadili kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba wapinzani si wakweli pamoja na hoja binafsi za wapinzani ambazo zitawasilishwa katika mkutano wa 14 wa Bunge ulioanza jana mjini hapa.

Naye Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, alikiri kuwa suala la ushirikiano wa vyama vya upinzani lilijadiliwa kwenye kikao hicho, ila aliongeza kuwa anachokifahamu yeye, ushirikiano bado upo na ndiyo maana bado bungeni wanawakilishwa na msemaji mmoja wa kambi ya upinzani.

Msemaji huyo wa upinzani alisema hayo jana ikiwa ni wiki kadhaa sasa baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutoa kauli ya kuvunjika kwa ushirikiano wa vyama hivyo.

mwanakijiji
01-28-2009, 12:38 AM

anamaanisha ushirikiano kati ya CUF na UDP... na kuna weza kuwa na strategic partnership Bungeni, lakini hivi vyama haviwezi kuungana.

Mpita Njia
01-29-2009, 05:47 PM
Lakini kumbuka "umoja ni nguvu...". Kuiondoa CCM madarakani kunahitajika nguvu ya ziada, mojawapo ni hivi vyama vya upinzani kushirikiana. Kama wataendelea wenyewe kwa wenyewe kutengana, ni faida kubwa kwa CCM.

Kwani CCM imeungana na nani? Mbona ina nguvu za kuwashinda hao wanaohangaika kuungana?

mwanakijiji
01-29-2009, 06:45 PM
Kwani CCM imeungana na nani? Mbona ina nguvu za kuwashinda hao wanaohangaika kuungana?

hilo swali.. zuri; ndio maana siamini kama ili upinzani ufanikiwe ni lazima uungane.

mfumwa
01-30-2009, 11:26 AM
Kwani CCM imeungana na nani? Mbona ina nguvu za kuwashinda hao wanaohangaika kuungana?

Kuungana haimaanishi kuwa vyama hivi viungane kipatikane chama kimoja, sio hivyo, lakini ikiwezekana ni bora. Muungano hapa uwe shirikiano wa kweli, katika kudai yale yatakayoweza kuongeza idadi ya wapinzani kwa udiwani na ubunge, kuelekea kupata uRais. Hivi vyama kama vitakuwa na sauti moja kudai katiba, ili ipatikane tume huru kutakuwa na msukumo fulani. Wanaweza hata susia chaguzi ili kuisukuma serikali kuifanya tume kuwa huru.

Huwezi ingia kwauchaguzi kwa tume iliyochaguliwa na CCM ukasema kutakuwa na "fair play". Hivyo wakianza ungana katika mambo muhimu, ndio itakuwa rahisi kuiondoa CCM. Mpita njia unauliza CCM imeungana na nani?, unaweza linganisha rasilimali za CCM na chama chochote cha upinzani. CCM iko tangu lini?, hivyo umoja/ushirikiano ni muhimu kuiondoa CCM madarakani.

Mpita Njia
01-30-2009, 01:10 PM
Ndio hapo sasa wapinzani, kila mmoja anatakiwa kujijenga na kuwa kama CCM. kama wanaanza kushambuliana tangu wakiwa wachanga hivi, hata hilo wazo la ushirikiano unalotoa halitawezekana, na kwa hakika wameshathibitisha kuwa haliwezekani

dickabudi
01-30-2009, 03:06 PM
Binafsi nataka kujua na kuungalia kwa kina upinzani ukiwa umeungana au haujaungana ukipewa dola utaleta mabadiliko yenye manufaa kwa umma au tutakuwa tunabadilisha jina la chama tawala tu kwangu mimi hiyo ndiyo hoja siyo kuleta mabadiliko ya nani watawala bali watawala wapya wana manufaa yapi kwa wazalendo

mfumwa
01-30-2009, 04:05 PM

Dickabudi, vyama vya siasa vinapigania kuwa madarakani ili kuongoza kwa sera walizojiwekea. Kubadilisha ni mojawapo ya vyanzo vya mabadiliko. Chama kikijua kuwa kikilikoroga uchaguzi unaofuata kitaondolewa kitajitahidi kupunguza madudu. Lakini kama chama kina fanya uchafu, na kikirudi kwa wananchi kinachaguliwa, unadhani kitakuwa na wazo la kuweka mambo sawa.

CCM ikiwekwa benchi, chama kitakachokuwa madarakani kitajitahidi ili kisijeondolewa tena madarakani. Na kujitahidi ni kufanya yale yenye maslahi ya Taifa. Ghana walijaribu, walikiondoa Chama tawala madarakani, sasa uchaguzi huu wa juzi wamekirudisha. Sasa hivi hichi chama cha Ghana nina hakika kitajitahidi kutofanya makosa.

dickabudi
01-30-2009, 05:17 PM
Ninachokiona ni kwamba Ghana wameadvance katika demokrasia wamediriki kuking'oa chama tawala na kukirejesha baada ya kupima na upande wa upinzani ambao wameona haukuwanufaisha ama kura zao za jazba ziliwasababishia kupata serikali legelege hivyo wamejutia makosa yao

ndiyo maana narudia tena lengo liwe ni kupata team ya kuongoza nchi yenye uchungu na nchi si kuwapa watu waunde serikali kwa sababu kwa sasa wapo kwenye upinzani

hivyo basi tutathmini sera za kila chama, profile ya kila kiongozi wa chama na kutafuta walio bora kwa mazingira yetu na wakati kabla ya kuhalalisha tu opposition wapewe waunde serikali

mfumwa
01-30-2009, 05:43 PM

Kubadilisha serikali sio kwamba Ghana walifanya jazba, ni kuamua kama walivyoamua Kenya, Zambia, Malawi nk. Hakuna mtu anawapa upinzani sababu tu ni wapinzani, kuna kupima. Na vyama vyenye muelekeo vya upinzani vipo TZ. Hakuna chama kitakachoingia, ama team ambayo itakuwa 100% perfect, hilo halipo, lakini tunataka japo kwa kiasi fulani mwananchi na Taifa liheshimiwe.

Mpita Njia
01-30-2009, 07:26 PM
CCM ikiwekwa benchi, chama kitakachokuwa madarakani kitajitahidi ili kisijeondolewa tena madarakani. Na kujitahidi ni kufanya yale yenye maslahi ya Taifa...

Tatizo ni kuwa hapa kwetu vyama havitegei kubakia madarakani kwa kutekeleza vema sera zake, bali kwa mizengwe ya kunua wapinzani, kutumia majeshi, kuharibu uchaguzi na hila nyingine nyingi

mfumwa
01-30-2009, 07:41 PM
Tatizo ni kuwa hapa kwetu vyama havitegei kubakia madarakani kwa kutekeleza vema sera zake, bali kwa mizengwe ya kunua wapinzani, kutumia majeshi, kuharibu uchaguzi na hila nyingine nyingi

Tunarudi kule kule kushirikiana ndio kutaweza kukiondoa chama tawala madarakani. Vishirikiane kudai katiba mpya, tupate tume huru ya uchaguzi, hayo yote ya mizengwe yatapungua.

Mpita Njia
01-31-2009, 09:52 AM
Tunarudi kule kule kushirikiana ndio kutaweza kukiondoa chama tawala madarakani. Vishirikiane kudai katiba mpya, tupate tume huru ya uchaguzi, hayo yote ya mizengwe yatapungua.

nadhani tutakuwa tuznazunguka hapohapo. Mimi naamini kuwa kushirikiana hakufai kwa sababu imeshajidhihirisha kwua ni suala lisiweza kuleta tija katika mazingira ya sasa. lakini upo uwezekano wa chama kimoja kimoja cha upinzani, kujijenga-mazingira ya sasa yanawezesha hilo.
Kujijenga kwao kusiwe kwa ghilba na mizengwe kama ambavyo chama tawala kimekuwa kikifanya ili kubakia madarakani. Kuna hoja nyingi za msingi hivi sasa ambazo zikijengwa kwa ustadi na kusimamiwa watu wanaojua propaganda na ushawishi wa kisiasa wanaweza kuwashawsihi watu wengi kukiunga mkono chama hicho, huku kikiwa na sera zentye kuonyesha matumaini ya ukombozi wa kweli.
Hili linawezekana ukizingatia kuwa maovu mengi yaliyofanywa na watawala yanajidhihirisha na wananchi wanaonekana kuwa w3amechoka kuka chini ya minyororo hii, wanachokosa na mtu wa kuwatoa utumwani tu. Hoja yangu ni chama fulani kijijengee uwezo wa kuwatoa watanzania katyika minyororo hiyo