PDA

View Full Version : Mwisho wa kisiasa wa Waziri Masha?



mwanakijiji
01-29-2009, 09:30 AM
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Lawrence Masha yuko kikaangoni tena. Safari hii hata hivyo ni kuhusiana na mkataba wa kampuni itakayochapisha vitambulisho vya uraia wa taifa, mradi ambao una thamani ya karibu Shs. Bilioni 200 katika kuanza kuutekeleza. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya kuaminika, Waziri Masha amejikuta katika kasheshe mpya baada ya kuingilia mchakato wa upatikanaji wa kampuni itakayoendesha mradi wa kuchapa vitambulisho hivyo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu hicho, Waziri Masha ameonesha kushangazwa kwa kampuni ambayo yeye aliipigia debe kutupwa pembeni na kampuni nyingine kupewa tenda hiyo. Kutokana na hilo Waziri Masha aliandika barua kwa Katibu Mkuu kiongozi Bw. Stephen Luhanjo akionesha kumlalamikia Katibu huyo mkuu kwa mawasiliano yako kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Patrick Rutabanzibwa bila ya kumshirikisha yeye.

Katika malalamiko yake Bw. Masha anaonesha kutoridhika kuwa kampuni x iliachwa wakati kwa imani yake ilipaswa kupewa tenda hiyo. Hata hivyo, wataalamu mbalimbali na watu wa bodi ya tenda ya wizara walikataa kampuni hiyo licha ya kupigiwa debe sana na Waziri. Tetesi ambazo inadaiwa zina uzito mkubwa zinasema kuwa Bw. Masha ana maslahi yaliyofungamana na kampuni hiyo na kwa muda mrefu alitarajia ingepata tenda hiyo.

Mpango wa kuchapisha vitambulisho vya uraia umekuwa ukizungushwa kwa muda mrefu na kuna tuhuma za ufisadi ambao umechelewesha kuanza kwa mradi huu. Miaka karibu kumi iliyopita kampuni kutoka Malaysia ?ilishinda? tenda ya kuchapa vitambulisho hivyo katika mazingira ambayo hayakueleweka.

Mojawapo ya mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa ni uamuzi wa kuchukua teknolojia ya ?Smart Card? ambayo ni ya kisasa sana duniani yenye kuhisisha vipimo vinavyojulikana kama ?biometric? kama macho, vinasaba n.k Malalamiko mengine ni pamoja na kuundwa kwa ofisi ya kusimamia mjadala na maafisa wake kuteuliwa wakati tenda ya mradi ilikuwa haijatangazwa. Hilo inadaiwa lilifanywa kinyume na sheria ya Udhibiti wa Manunuzi ya serikali.

Habari mbalimbali zinasema kuwa hadi sasa mradi huo umezidi kuonekana kupanuka na kukua zaidi huku ukifikia gharama ya karibu bilioni 250 huku baadhi ya watumishi wa wizara ya mambo ya nje na wa taasisi nyingine wakiwa ni washauri katika makampuni yaliyokuwa yanaomba tenda hiyo. Wengine inadaiwa wameshalipwa. Habari za uhakika zinasema kuwa hata baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa wizara na wenyewe wanadaiwa kuwa na maslahi katika makampuni hiyo ilimradi kila mmoja mwisho wake alipwe.

Chanzo chetu kilitukumbushia sakata la ununuzi wa rada ambapo maafisa mbalimbali wa serikali akiwemo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu na Gavana wa Benki Kuu wanatuhumiwa kupewa malipo ya karibu Shs. Bilioni moja ili kufanikisha mradi huo. ?Mradi huu una kila aina ya ulaji kwa baadhi ya watu? kimesema chanzo chetu.

Hata hivyo, msimamo wa Katibu Patrick Rutabanzibwa unaonekana kuwa kikwazo kikubwa kwa wakubwa wengi hasa baada ya kujikuta anahusishwa na orodha ya ufisadi wakati katika sakata la mkataba wa IPTL alionekana ni shujaa. ?Huu ni wakati wake kujisafisha. Badala ya kutumia vyombo vya habari au kwenda mahakamani, Ruta anataka kuonesha kuwa yeye ni mwadilifu na yuko tayari kugongana na yoyote katika mradi huu? alisema afisa mmoja toka wizarani ambaye alikataa kutajwa jina kwa sababu si msemaji wa Wizara.

Kutokana na sakata hilo maafisa wa wizara wanaangalia ishara yoyote kutoka Bungeni leo kuhusu mwelekeo wa mradi huu na hasa nafasi ya Waziri Masha kwani endapo itathibitika kuwa amejaribu kwa namna yoyote kujinufaisha kwa kutumia mradi huu au kupinda taratibu za ununuzi wa umma kama alivyofanya aliyekuwa Waziri Mkuu Lowassa, inatabiriwa kuwa huu waweza kuwa ndiyo mwisho wake kisiasa katika wakati huu.

mwanakijiji
01-30-2009, 05:51 PM
Kampuni anayoibeba Masha ni balaa tupu

2009-01-30 10:49:51
Na Waandishi Wetu

Kampuni ya Sagem Securite ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha anadaiwa kuibeba katika mchakato wa kupata mzabuni wa kutekeleza Mradi wa Vitambulisho vya Taifa ambao utaigharimu serikali kiasi cha Sh. bilioni 200, kama ni sawa na iliyoomba kazi ya aina hiyo nchini Nigeria mwaka 2003 ni ya hatari.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, kampuni hiyo, ikijiita Sagem Securite iliwatia matatani mawaziri watatu wa serikali ya Nigeria wakati huo ikiongozwa na Rais Olusegun Obasanjo, kutokana na kudaiwa kuwahonga mawaziri hao kiasi cha Dola za Marekani milioni 2.

Hongo hiyo ilidaiwa kutolewa kama kishawishi kwa viongozi hao ili waibebe katika zabuni ya kutengeneza vitambulisho vya kitaifa vilivyokuwa viliigharimu nchi hiyo kiasi cha Dola za Marekani milioni 214.

Mradi huo unafanana na ambao serikali ya Tanzania inataka kuanzisha wa kutengeneza vitambulisho vya taifa ambao utagharimu taifa Sh. bilioni 200 (sawa na Dola za Marekani milioni 150).

Rais Obasanjo kwa kukasirishwa na uroho wa wasaidizi wake, alimfuta kazi Waziri wa Kazi na Uzalishaji wa nchi hiyo, Hussaini Akwanga.

Akwanga alidaiwa kutenda kosa hilo akishikilia wadhifa wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Nchi ya Nigeria.

Chanzo hicho kilisema kuwa Rais Obasanjo alichukua hatua hiyo wakati uchunguzi wa kashfa hiyo ukiendelea, lengo likiwa ni kupiga vita rushwa kwa watumishi wa umma.
Wakati akimfukuza kazi Akwanga, Rais Obasanjo alisema Waziri huyo, alilidhalilisha taifa.

Waziri huyo na wenzake watano walifunguliwa mashtaka mahakamani kwa makosa 16 yanayohusiana na sakata hilo, linalokadiriwa kusababisha hasara ya Dola za Marekani milioni 214 sawa na Sh. 300 bilioni. Waliofikishwa kortini walidaiwa kula rushwa ya Dola za Marekani milioni mbili.

Walioshtakiwa pamoja na Akwanga, na nyadhifa walizokuwa nazo kwenye mabano ni Turi Akerele (Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani), Dk. Okwesilieze Nwodo (Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Peoples Democratic Party), Dk. Mohammed Shatta (Waziri wa Nchi wa Mambo ya Ndani) na Sunday Afolabi aliyweahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini humo.

Afolab alishtakiwa kwa kupokea Dola za Marekani 330,000, Akwanga alimuwezesha binti yake kupokea Dola za Marekani 30,000 kwa niaba yake.

Mwakilishi wa kampuni hiyo nchini Nigeria ndiye aliyedaiwa kutoa rushwa hiyo akishirikiana na Nwodo na Akerele alipokea Dola za Marekani 500,000.

Kampuni hiyo ikielezwa kuhusika na kashfa hiyo kuhusu vitambulisho vya taifa nchini Nigeria, jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alithibitishia Bunge kwamba Waziri Masha alimwandikia barua pamoja na mambo mengine akimtuhumu Katibu Mkuu Kiongozi kuingilia wizara yake bila kumuhusisha katika mchakato wa zabuni ya vitambulisho hivyo.

Akijibu mwaswali ya papo kwa papo bungeni, Pinda alisema taarifa hizo ni kweli kwa kuwa kuna nyaraka zimenyofolewa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.

``Hilo ni kweli kabisa, maana kuna watu wamenyofoa folio pale Wizara ya Mambo ya Ndani,`` alisema Pinda alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, aliyetaka kujua sababu za Waziri Masha kuingilia mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya taifa kinyume cha sheria ya Manunuzi ya Umma (PPRA).

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwataka watu wavute subira ili mchakato huo ukamilike kwanza ndipo mwenye kutaka kuhoji afanye hivyo.

``Mheshimiwa Slaa umetuwahi, lakini jambo hili linafanyiwa kazi. Ingekuwa ni vizuri ukasubiri mpaka mchakato umalize ulete madai kama haya ingesaidia sana,`` alisema Pinda, na kuongeza:

``Mchakato huu haujafika mwisho. Tusubiri halafu tutamhukumu Waziri ukikamilika.``

Hata hivyo, ilibidi Spika, Samuel Sitta, alilazimika kuingilia kati kwa kuyakataa baadhi ya maswali yaliyoelekezwa kwa Waziri Mkuu na Dk Slaa kutokana na kuonekana kwamba baadhi ya wabunge walionekana kuleta malumbano na Pinda.

``Nadhani tukitumia kipindi hiki kulumbana na Waziri Mkuu, si sahihi Ukipata `facts` na we uliza ufafanuliwe `facts` na siyo kuleta malumbano na kung`ang`ani kile unachodhani wewe ni sahihi,`` alisema Spika Sitta.

Alimshauri Dk. Slaa kutumia njia nyingine ya kuwasilisha bungeni hoja binafsi kama hakuridhika na majibu aliyopewa na Waziri Mkuu ili kutoa fursa ya kujadiliwa na wabunge wengi zaidi.

Naye Joseph Mwendapole anaripoti kuwa Dk Slaa, amesema anaandaa hoja binafsi kwa ajili ya kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, awajibishwe kwa kuingilia mchakato wa kumpata mzabuni wa kutengeneza vitambulisho vya taifa.

Akizungumza na Nipashe jana, Dk. Slaa alisema anashangaa kuona Waziri Masha akiingilia shughuli ambayo anajua fika kuwa hana mamlaka nayo kisheria.

Alisema anashangazwa na hatua ya Waziri Masha kuandika barua ya malalamiko kwa Waziri Mkuu kutetea kampuni ya Sagem Securite iliyoomba zabuni ya kutengeneza vitambulisho hivyo.

Waziri Masha anadaiwa kuitetea kampuni hiyo baada ya Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo kuiengua katika mchakato wa kuwania zabuni hiyo.

Dk. Slaa alisema Masha kama angeona kuna taratibu zimekiukwa alipaswa kumwelekeza mlalamikaji (Sagem Securite), hatua za kuchukua kuwasilisha malalamiko badala ya yeye (Masha) kulalamika kwa niaba ya kampuni hiyo.

``Mchakato wa zabuni hii una usiri na mashaka sana...na mashaka haya yanadhihirishwa na waziri ndani ya serikali kulalamika kwa niaba ya kampuni iliyoomba zabuni,`` alisema na kuongeza kuwa Waziri hana mamlaka ya kuingilia mamlaka zinazoshughulikia masuala ya zabuni.

Aidha, alisema kama Waziri alikuwa na mashaka na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya zabuni, alipaswa kuielekeza kampuni ya Sagem kwenda kulalamika kwenye Mamlaka ya Usimamizi wa Zabuni (PPRA) na si yeye kulalamika.

``Kama kulikuwa na malalamiko, PPRA ndiyo ilipaswa kuchunguza na kutoa jibu kama kuna sheria au taratibu imekiukwa au la, sasa yeye anakimbilia kwa Waziri Mkuu kufanya nini na ana maslahi gani na kampuni hiyo?`` alihoji Dk. Slaa na kuongeza kuwa Masha ni mwanasheria na alijua fika kuwa anachokifanya ni kinyume cha sheria.

Alisema atakapokamilisha hoja yake hiyo ataiwasilisha kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ambayo ndiyo ina mamlaka ya kupanga siku ya kusikilizwa kwa hoja hiyo.

Alisema inashangaza kuona mabilioni ya fedha za umma zikizidi kuyeyuka katika mchakato usio na mwisho, lakini hakuna anayewajibishwa.

Dk. Slaa alipinga kauli ya Waziri Mkuu aliyoitoa jana bungeni kuwa mchakato wa zabuni hiyo unaendelea kwa kuwa sasa umesimama.

``Nitaomba kama haya yanayosemwa juu ya Masha ni kweli basi awajibishwe kwa kuwa kila anayekiuka Sheria lazima achukuliwe hatua za kisheria,`` alisema.

Masha anadaiwa kufanya hivyo akidai kutoridhishwa na hali halisi ya mchakato huo kabla hata matokeo ya kupatikana mzabuni hayajatangazwa.

Kampuni hiyo, ni kati ya makampuni 54 yaliyoomba kupewa zabuni hiyo. Ilienguliwa katika mchujo wa tatu, baada ya mchujo wa kwanza kuyaengua makampuni 33 na kubaki 21 na mchujo wa pili, kuyaengua makampuni 13 na kubaki manane.

Wajumbe wanaounda bodi hiyo, ni wanatoka Magereza, Uhamiaji, Jeshi la Polisi, Zimamoto na Uokoaji, Usalama wa Taifa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru).

mwanakijiji
01-30-2009, 06:00 PM
Maswali 10 kwa Masha

2009-01-30 10:46:38
Na Boniface Luhanga, Dodoma

1.Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, majibu ya wazabuni walioingia hatua ya pili ya mchakato wa kupata kazi ya kutengeneza vitambulisho vya taifa hayajatolewa kwa wahusika Je, kampuni ya Sagem Securite ilijua vipi imeenguliwa hadi kulalamika kwa Waziri Masha?

2.Hadi sasa taarifa zinasema si Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wala Bodi ya Zabuni, waliopewa nakala ya barua ya malalamiko ya Sagem Securite, kwa hali hii ni Waziri pekee mwenye barua hiyo, Je, ni halali kukalia barua na kulalamika tu bila kuonyesha vyombo husika?

3.Kwa nini Sagem Securite walilalamika kwa Waziri tu na si kwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani na nakala ya malalamiko kupelekwa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) kama maelekezo ya zabuni yalivyoonyesha?

4. Kwa nini hata pale Waziri Masha ambaye ni mwanasheria mahiri alipopata malalamiko ya Sagem Securite hakuwaelekeza pa kwenda kwa mujibu wa sheria ya PPRA, badala yake aliamua kuchukua jukumu hilo kwa niaba ya mzabuni?

5.Sheria ya PPRA haitoi fursa ya kulalamika kuhusu zabuni kama vyombo vyote vinavyohusika katika kupitia mchakato wa zabuni ya umma vitakubaliana kwa mujibu wa sheria je, ni kwa nini Waziri Masha alijitokeza na kumtaka Katibu Mkuu wake aombe maelekezo PPRA wakati bodi ya zabuni hakutofautina?

6.Uchunguzi wetu umeonyesha wazi kwamba vyombo kadhaa vya usalama wa nchi vilishiriki katika mchakato wa zabuni hiyo ambavyo ni Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) tangu hatua ya awali, je, malalamiko ya Masha ya kutokukubalina na maamuzi ya bodi ni kielelezo cha kukosa imani na vyombo hivyo na kwamba yeye peke yake ndiye anayeona hitilafu katika mchakato huu?

7.Waziri Masha anadai kulalamikiwa na Sergen Securite, inakuwaje anataka hata makampuni ambayo hayajalalamika rasmi kwake yarejeshwe kwenye mchakato wa zabuni?

8. Kwa nini Waziri Masha hakumweleza Waziri Mkuu ukweli wote kuhusu kampuni ya Sagem Securite hata baada ya kuelezwa na bodi ya zabuni, ni kwa nini pia hakuwa na ujasiri wa kumwona Katibu Mkuu Kiongozi kujua sababu za kumwagiza Katibu Mkuu wake aendelee na mchakato wa zabuni, ni nguvu gani inamsukuma kushindwa kuona yote haya?

9. Kwa nini Waziri Masha ameamua kumpuuza Katibu Mkuu wake, kwa nini hataki afanye kazi kama mtendaji na anamshinikiza kisiasa, je, anataka kuwa msimamizi wa sera na mtendaji kwa wakati mmoja?

10.Waziri Masha anataka kuwaambia Watanzania kwamba mchakato mzima wa zabuni ya vitambulisho vya taifa una utapeli, rushwa na kwa maana hiyo ufutwe kwa sababu tu kampuni ya Sagem Securite imeenguliwa kwenye zabuni?

Watanzania wangependa kusikia majibu ya Masha ingawa amekwisha kusema kwamba hawezi kuzungumzia barua aliyomwandikia Waziri Mkuu wala uingiliaji wake mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya taifa kwa sababu anatekeleza kazi za Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

bulesi
01-30-2009, 06:28 PM
Kampuni hii ya kifaransa ilianza kufukuzia tenda hii toka enzi za Joseph Mungai akiwa waziri wa mambo ya ndani, na inasemekana Mungai alikwishakatiwa advance pochi kama kawaida yake; alipokuwaanaondoka akamuachia wosia Masha juu ya ulaji wa tenda hiyo na kama kawaida ya kampuni hii ya kifaransa inasemekan Masha nae kisha kula advance na ndio maana anakuwa mbogo Kampuni yao inapotolewa nje!! HAWA MAFISADI LAZIMA TUWATOKOMEZE KAMA VILE TUTAKAVYOWATOKOMEZA WAUAJI WA NDUGU ZETU ALBINO!!

mwanakijiji
02-03-2009, 06:21 PM
Sakata la Masha na vitambulisho presha...

2009-02-03 10:24:20
Na Waandishi Wetu Dar na Dodoma

Hoja binafsi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Dk. Willibrod Slaa ya kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, awajibishwe kwa kuingilia mchakato wa kumpata mzabuni wa Mradi wa Vitambulisho vya Taifa, imepelekwa kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na huenda ikajadiliwa na kamati hiyo muda wowote kuanzia leo.

Habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati ya Uongozi wa Bunge zilizothibitishwa na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, zinaeleza kuwa hoja hiyo imepelekwa kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ambako inatarajiwa kujadiliwa muda wowote leo kabla ya maamuzi kuwasilishwa bungeni.

Imeelezwa kuwa uamuzi wa kupelekwa hoja hiyo kwenye kamati hiyo, umefikiwa na Kamati ya Uongozi wa Bunge, ambayo Mwenyekiti wake ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta, katika kika kilichofanyika mjini Dodoma jana.

``Kamati ya Uongozi ya Bunge ilikutana leo (jana) mchana, baada ya kikao cha Bunge cha asubuhi, ikafikia uamuzi kwamba, hoja ya Dk. Slaa ipelekwe kwenye Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na huenda kesho (leo) kamati hiyo ikaijadili,`` chanzo chetu kutoka ndani ya kamati hiyo kilieleza.

Uamuzi huo umefikiwa na kamati hiyo zikiwa zimesalia siku tatu, kufika siku ambayo Dk. Slaa, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kuwasilisha hoja hiyo katika Mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.

Dk. Slaa, ambaye pia ni Mbunge wa Karatu (Chadema), alitarajiwa kuwasilisha hoja hiyo bungeni Ijumaa ya wiki hii.

Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah, alilithibitishia Nipashe kwa njia ya simu jana kuwa tayari Dk. Slaa alikwishatoa notisi kwa ofisi za Bunge kuhusu nia yake ya kutaka kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

``Notisi imeshatolewa, nimeiona, imepokelewa kwa mujibu wa taratibu, kinachobaki ni maelezo ya hoja,`` alisema Kashililah alipozungumza na Nipashe jana.

Nipashe ilipowasiliana na Mwenyekiti wa Kamati ya hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Wilson Masilingi, alisema mpaka sasa anachojua ni kwamba kesho Waziri Masha pamoja na maafisa wa zabuni wameitwa kwenye kamati yake.

``Suala la Masha litajadiliwa Jumatano. Masha anatakiwa kuja mbele ya Kamati akiwa na wataalam mbalimbali wakiwamo wale wa zabuni,`` alisema Masilingi huku akikataa kuingia kwa undani.

Dk. Slaa Alhamisi iliyopita wakati wa maswali ya papo kwa hapo bungeni kwa Waziri Mkuu, alimtaka alieleze Bunge kuhusiana na hatua ya Waziri Masha kuingilia kati mchakato huo kinyume cha sheria ya Manunuzi ya Umma.

Hata hivyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema kuwa Dk. Slaa ameiwahi serikali kabla haijalizungumzia suala hilo, lakini athibitisha kuwapo taarifa za kunyofolewa kwa nyaraka za siri zinazohusu suala hilo katika jalada moja, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Hata hivyo, Spika Sitta alimshauri Dk. Slaa kuandaa hoja binafsi kuhusu suala hilo na kuiwasilisha bungeni.

Spika alifikia hatua hiyo baada ya kumkatiza Dk. Slaa aliyekuwa anaendelea kumuuliza maswali Waziri Mkuu kwa kumweleza kwamba kama alikuwa hakubaliani na ukweli ulioelezwa, basi aandae hoja binafsi ili ijadiliwe na wabunge.

Awali, Dk. Slaa aliliripotiwa na Nipashe akishangaa kuona Waziri Masha akiingilia shughuli ambayo anajua fika kuwa hana mamlaka nayo kisheria.

Dk. Slaa alisema anashangazwa na hatua ya Waziri Masha kuandika barua ya malalamiko kwa Waziri Mkuu kutetea kampuni ya Sagem Securite iliyoomba zabuni ya kutengeneza vitambulisho hivyo.

Waziri Masha anadaiwa kuitetea kampuni hiyo baada ya Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo kuiengua katika hatua za awali za mchakato wa kuwania zabuni hiyo.

Dk. Slaa alisema kama Masha angeona kuna taratibu zimekiukwa alipaswa kumwelekeza mlalamikaji (Sagem Securite), hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasilisha malalamiko badala ya yeye (Masha) kulalamika kwa niaba ya kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Nipashe wiki iliyopita, wajumbe wanaounda Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo, ni pamoja na wajumbe kutoka Magereza, Uhamiaji, Jeshi la Polisi, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na mchakato wa zabuni hiyo uliwahusisha pia maofisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) na Usalama wa Taifa.

Inasemekana pia kuwa Waziri Masha aliandika barua kwa Waziri Mkuu, akimlalamikia Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kwa madai kuwa hakumhusisha yeye (Masha) kama waziri mwenye dhamana na Wizara ya Mambo ya Ndani katika kuwasilisha kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri taarifa za utekelezaji wa mchakato wa mradi huo.

Katibu Mkuu Kiongozi anadaiwa kumwagiza kufanya hivyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo peke yake.

Imegundulika pia kuwa kampuni ya Sagem Securite ilipata kuwaletea matata mawaziri watatu nchini Nigeria, ambao walifukuzwa kazi na kushitakiwa mahakamani kutokana na tuhuma za kupokea rushwa kutoka kampuni hiyo ili ipate zabuni ya kutengeneza vitambulisho vya taifa.

Mawaziri hao walifukuzwa wakati wa utawala wa Rais Olusegun Obasanjo.

Habari hizo ziliripotiwa na gazeti hili Alhamisi iliyopita, ikidaiwa kuwa Waziri Masha alifanya hivyo akidai kutoridhishwa na hali halisi ya mchakato huo kabla hata matokeo ya kupatikana kwa mzabuni hayajatangazwa.

Mradi huo unakadiriwa kwamba utaigharimu serikali Sh. bilioni 200.

mwanakijiji
02-04-2009, 05:36 PM
Masha sasa ni majaliwa

2009-02-04 17:12:19
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Wakati Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ilitarajia kuketi leo kujadili sakata linalomkabili Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Lawrence Masha, kuna taarifa kuwa kibarua cha mheshimiwa huyo kiko mashakani kutokana na baadhi ya wabunge kuandaa nondo kibao za kumtia hatiani kiongozi huyo.

Nondo hizo inadaiwa zina ushahidi kadhaa unaobainisha kuwa Mheshimiwa Masha alitaka kuibeba kampuni moja ili ipate tenda ya kutengeneza vitambulisho vya taifa, mradi utakaogharimu takribani shilingi bilioni 200 za Kitanzania.

Chanzo kimoja cha gazeti hili kimedai kuwa kikundi hicho cha wabunge waliokomalia sakata hilo, kimeapa kuwa kitaendelea kulivalia njuga sakata hilo hadi Mhe. Masha aachie ngazi ama kwa kujiuzulu au kwa kuwajibishwa na Rais Jakaya Kikwete aliyemteua.

Habari zaidi zinadai kuwa miongoni mwa wabunge hao, yumo Dk. Wilbroad Slaa wa Jimbo la Karatu (CHADEMA).

Vyombo vya habari mbalimbali vimesema kuwa, Dk. Slaa tayari ameandaa hoja binafsi kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni akitaka sakata hilo lijadiliwe kwa kina na uamuzi kutolewa.

Habari zaidi zinasema hoja ilishatua kwa Spika wa Bunge ambaye aliipeleka kwenye kamati hiyo ya mambo ya nje, ambayo inaketi leo.

Imeelezwa kuwa Waziri Masha na Dk. Slaa wameitwa kwenye kamati hiyo ambapo kila mmoja atatoa hoja zake.

Alasiri ilipojaribu kuwasiliana na Dk. Slaa kupata maelezo yake kuhusiana na sakata hilo alisema, ingawa ameitwa kwenye kamati hiyo, hadhanii kuwa atasitisha dhamira yake ya kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

Amesema anachofahamu yeye ni kwamba,kamati hiyo haina uwezo wa kuzuia hoja, isipokuwa inao uwezo wa kuichelewesha endapo itakuwa haijakamilisha uchunguzi wake.

``Kwa mujibu wa mamlaka ya bunge, kamati haina uwezo wa kuzuia hoja, isipokuwa inaweza kuchelewesha tu endapo itasema haijakamilisha uchunguzi wake,`` Dk. Slaa aliliambia gazeti hili.

Ameongeza kuwa endapo atahisi kuwa inafanyika mbinu yoyote ya kumnyamazisha au kuzuia hoja yake, wahusika wa suala hilo wataumbuka zaidi kwa sababu mahakama kuu ya suala hilo itakuwa ni umma wa Watanzania.

Wakati tukienda mitamboni, kamati ya mambo ya nje ambayo mwenyekiti wake ni Mbunge wa Muleba Kaskazini, Mhe. Wilson Masilingi, ilitarajiwa kukutana na kujadili suala hilo.

Hivi karibuni, Mhe. Masha alidaiwa kuingilia mchakato wa mradi wa vitambulisho vya taifa, jambo ambalo Dk. Slaa aliliibua bungeni Alhamisi iliyopita wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Mhe.Mizengo Pinda.

Hata hivyo, Spika aliingilia kati suala hilo na kumtaka Slaa, kama ana hoja ya msingi kuhusiana na suala hilo, basi aiwasilishe ili ijadiliwe.

ipn
02-05-2009, 08:33 AM
ni vizuri masha abanwe tumechoka kuwa na mawaziri wababaishaji

dickabudi
02-05-2009, 10:24 AM
Mwanakijiji hapa ndipo unatakiwa upachimbe na kuona CCm wana quality gani, fanya yafuatato:

1. Tafuta nini jana kamati ya wabunge wa CCM imetafakari, wamemhoji vipi kada wao na wana msimamo gani kuhusiana na tuhuma hizi yaani wamepata ukweli gani na wakawa na msimamo gani wa pamoja uwe wa kulindana au wa kumtema muovu
2. Tafakari Mh Spika kwa nini alitaka iwe hoja binafsi, je ni kumsafisha Masha au kumuwajibisha

3. Tafakari na tupe nyepesinyepesi kutoka kwa kamati ya Masilingi uone dhambi ya Waziri mwenye dhamana ya Wizara fulani kutokuwa na taarifa kuhusu mchakato fulani wa watalaam wa wizara yake na anapoandika kwa Boss wake kuonyesha amekuwa by passed ni kosa la kujiuzulu, kuonywa, kufukuzwa kazi ama kupandishwa cheo maana watu wanasahau kuwa adhabu ni pamoja na kupandishwa cheo

dickabudi
02-05-2009, 10:31 AM
Pia nionavyo Mimi taarifa za gazeti la Nipashe zinaunazi na kuendeleza tofauti za Masha na Mengi ni hatari gazeti linapotumika kama ofisa habari wa mwenye gazeti na si kuwapasha wananchi uhalisia wa jambo fulani
Mimi naona wako biased na wajiondoe kweye issue za Masha kwa kuwa wanaandika kumfurahisha Mkurugenzi wao Mtendaji na si kuwapa kile kitu fair wasomaji wao

dickabudi
02-05-2009, 11:50 AM
Mwanakijiji unaposema baadhi ya wabunge nilitegemea kupata majina ya wabunge kama 15 hivi na maoni yao kwa ratio ya uwingi kutokana na vyama vyao kwa mfano slaa na mbunge wa kike wa CHADEMA, CUF mbunge kutoka Unguja wa kuchaguliwa na wawili wa kike kutoka bara na visiwani etc, hapo ningeona habari imechimbwa na kutafitiwa lakini unaposema wabunge halafu tukawa na hoja za Dr Slaa pekee unasababisha tusitafakari kwa kina, usimfanye Dr. Slaa ni Mlalamikaji, Mwendesha Mashtaka, Hakimu na Askari Magereza lets be broad katika utafiti

Mpita Njia
02-05-2009, 01:55 PM
Kwa mwenye uwezo asome rai la leo, nadhani anaweza kuona picha tofauti na kile ambacho tumekuwa tukielezwa siku zote

dickabudi
02-05-2009, 02:15 PM
Hayo ndiyo yanayoonekana maudhui ya Barua ya Waziri Masha

Tujiulize nia ya barua hiyo ni njema au ni mbaya au tunataka tu kuweka historia

Kwa nini tusipate copy ya hii barua kama tulivyo na copy za SFO na EPA ripoti kumaliza mzizi wa fitina


"Kwa mujibu wa chanzo chetu hicho, Waziri Masha ameonesha kushangazwa kwa kampuni ambayo yeye aliipigia debe kutupwa pembeni na kampuni nyingine kupewa tenda hiyo. Kutokana na hilo Waziri Masha aliandika barua kwa Katibu Mkuu kiongozi Bw. Stephen Luhanjo akionesha kumlalamikia Katibu huyo mkuu kwa mawasiliano yako kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Patrick Rutabanzibwa bila ya kumshirikisha yeye.

Katika malalamiko yake Bw. Masha anaonesha kutoridhika kuwa kampuni x iliachwa wakati kwa imani yake ilipaswa kupewa tenda hiyo. Hata hivyo, wataalamu mbalimbali na watu wa bodi ya tenda ya wizara walikataa kampuni hiyo licha ya kupigiwa debe sana na Waziri. Tetesi ambazo inadaiwa zina uzito mkubwa zinasema kuwa Bw. Masha ana maslahi yaliyofungamana na kampuni hiyo na kwa muda mrefu alitarajia ingepata tenda hiyo." hii ni kwa mujibu wa gazeti la Nipashe je ni kweli hayo ndiyo maudhui ya barua ya Waziri Masha???????????

Mpita Njia
02-05-2009, 02:37 PM
Nilivyoelewa mimi, barua ya Masha ilikuwa na masuala mengi ambayo hayaelezwi an hao walioiona hiyo barua-kwa nini wameamua kueleza baadhi ya kuyaacha mengine, hilo mimi sijui. Pia, habari ya rai inaonyesha kuwa masha hakuitetea kampuni ya Sagem specifically bali alionya dhidi ya taratibu zisizofaa za kuteua mshindi. Inavyoonekana hii ngoma ililazimishwa na ministerial tenmder board wakati Kikwetevalishazuia kuendelea na mchakato wa tenda za kuficha, akataka kuwe na tenda ya wazi. Kama ndivyo hivi ilivyo, naona kuna mengi ambayomtunapaswa kuambia kabla hatujaamua nani ni mkosa

dickabudi
02-06-2009, 12:19 PM
Mimi nakuunga mkono Bwana Mpita Njia maana taarifa zinakanganya na inavyoelekea tusiingie kwenye mtego wa kudanganywa kuwa fisadi ni Mawaziri tu.
Nilivyosoma Rai, Mtanzania na hata Mwananchi zote zinaonyesha Masha kuwa kwenye right track ya kutokomeza ufisadi, kinyume na taarifa zinazobebwa na Nipashe

Tuepuke kutumiwa kufurahisha watu fulani kwa sababu tunapakuandika tunafedhehesha taaluma, rushwa si kupokea mabilioni tu rushwa pia ni kuwakingia kufua wahalifu kwa sababu tuna mahala pa kudanganya umma
kwa mkanganyiko huu taarifa tunayoitegemea ni ya kamati ya Masilingi maana tayari magezrti yetu yameondoa naturarity ya sakata hili kwa kuheshimu wanaowaajiri hapo ndipo naamini msemo wa Kaka yangu Dr. Gideon Shoo kuwa 'huwezi kufuga Mbwa ukabweka mwenyewe.'

mwanakijiji
02-06-2009, 05:20 PM
Barua tumeishaitundika kwenye "Vielelezo na Ushahidi". Hivyo tusiandikie mate tena.

dickabudi
02-07-2009, 10:50 AM
Mwanakijiji ....!!!! Congratuation umefanya kazi nazipitia barua zote hizo kutathmini na kupata uhalisia wa hili sakata

Ila nilichogundua Waziri Masha ni jasiri na hazina yetu ya baadae na vema Dr. Slaa akawakilisha hoja yake mapema ili wale waliompotosha akawataja na wakachuliwa hatua

Kifupi tujumuishe watalaam wa sheria na ugavi utakuta kwamba kamati nzima ya tenda ya wizara ya mambo ya ndani ni ya kuvunjwa na kuwajibishwa

Narudi palepale Fisadi si Waziri tu jamani angaliani humo kwenye mawizara kuna mamessenger wana magorofa eti kwa shughuli za kifisadi tusing'ang'anie kutoa kafara mawaziri wakati watendaji wa chini ndiyo wenye michezo michafu

dickabudi
02-17-2009, 09:52 AM
Taarifa hii ni kama ilivyoandikwa na Habari Leo imekopiwa tu


Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, ametangaza kuyafikisha baadhi ya magazeti mahakamani, kwa kile alichosema ni kutokana na kuandika habari zinazomhusu zenye lengo la kumchafua kwa kumhusisha na vitendo vya rushwa.

Masha aliwaambia waandishi wa habari leo, Dar es Salaam, kwamba amemwagiza mwanasheria wake, Imma Consult kutafuta ushahidi wa kutosha kufungua kesi mahakamani dhidi ya kampuni ya IPP Media, magazeti ya Nipashe na Sema Usikike na waandishi ambao wamekuwa wakiandika habari hizo.

Licha ya kuishitaki kampuni hiyo, waandishi wa habari hizo na kampuni iliyochapisha magazeti hayo, pia atakifikisha mahakamani kikundi ambacho kitabainika kutumia vyombo hivyo vya habari, kumchafua kwa madai kuwa imeonekana kuwa habari hizo zililenga kujenga hoja dhidi yake.

Waziri huyo alisema habari hizo zilimhusisha kuingilia mchakato wa kumpata mzabuni atakayetengeneza mfumo wa vitambulisho vya Taifa, kwa nia ya kuwezesha kampuni ya Sagem Securite anayodaiwa kuitaka ipate zabuni hiyo.
"Magazeti ya IPP Media yamekuwa yakishabikia sana, tujiulize, kulikoni?

Watanzania wanajiuliza Masha kafanya nini?...Nimeona niseme ili nisiache wengine wanisemee," alisema Masha. Kwa mujibu wa Masha, magazeti hayo yaliandika kuwa alikwenda Uswisi Oktoba mosi mwaka jana, ambako pamoja na mambo mengine, alikutana na kampuni hiyo, jambo alilosema si kweli na hata viza yake ya kuingia nchini humo, inaonyesha kuwa alitakiwa kuingia nchini humo Oktoba 4.

Alikiri kwenda nchini humo na kusema alifika Oktoba 5 kuhudhuria mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi (UNHCR) uliokuwa uanze Oktoba 6, lakini kwa mujibu wake, hakuwahi kukutana na kampuni hiyo kwa kipindi hicho.

Akielezea kilichotokea, Masha alisema wakati mchakato huo ambao ni wa siri ulipokuwa ukiendelea, kuna kampuni zilizokuwa zimeomba zabuni hiyo ambazo zilituma wawakilishi wao kwake na kudai kuwa zinatendewa isivyo katika mchakato na yeye alipuuza madai hayo na kuwashauri wafuate utaratibu wa kutoa malalamiko, ambao unawataka wafanye hivyo baada ya kukamilika kwa mchakato.

Masha alisema baada ya kukabidhiwa ripoti ya mchakato huku akiionyesha ripoti hiyo, aliona dosari kwenye ripoti hiyo, yakiwamo baadhi ya mambo aliyoelezwa awali na kampuni zilizodai kutendewa isivyo halali, ambayo aliyapuuza na kuona kuwa kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikivuja wakati mchakato ukiendelea.

Kutokana na dosari hizo, alimshauri Katibu Mkuu wa Wizara ambaye alikuwa akihusika katika mchakato huo, aombe ushauri kutoka Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) na Mamlaka hiyo ikajibu kuwa kweli kulikuwa na dosari.

Baadaye aliandika barua ambayo ni siri kwenda kwa Waziri Mkuu, ambaye ni bosi wake, kuelezea hali ya mchakato huo ilivyo, lakini kwa bahati mbaya barua hiyo ilinyofolewa katika nyaraka za Serikali na kuwekwa kwenye mtandao. Kwa mujibu wa Masha, alishangaa kuona ikiandikwa kuwa alikutana na kampuni hiyo Novemba Uswisi huku ikitajwa kuwa ina kesi ya rushwa nchini Nigeria na kuona kuwa alikuwa akihusishwa kwa namna moja au nyingine na rushwa.

Baada ya hapo aliwasiliana na Balozi wa Nigeria nchini, ambaye alimjibu kuwa jambo hilo linashughulikiwa kwa tahadhari, kwa kuwa kampuni hiyo ilifunguliwa kesi hiyo mwaka 2003 lakini mwaka 2004 kesi hiyo iliondolewa mahakamani na sasa inatekeleza miradi mikubwa nchini humo, na kuhoji kwa nini taarifa zote za kampuni hizo zisichapishwe. Mpaka sasa kampuni zilizo katika mchujo ni Unisys ya Afrika Kusini; Giesecke & Devrient Fze ya Dubai; Iris Corporation Berhad ya Malaysia; Madras Security Printers ya India; ushirikiano wa Maruben Corporation, Zetes na Nec ya Japan; ushirikiano wa Tata Consultancy Services na Ontrack Innovations Limited ya India.

ponda
02-17-2009, 02:23 PM
Pia nionavyo Mimi taarifa za gazeti la Nipashe zinaunazi na kuendeleza tofauti za Masha na Mengi ni hatari gazeti linapotumika kama ofisa habari wa mwenye gazeti na si kuwapasha wananchi uhalisia wa jambo fulani
Mimi naona wako biased na wajiondoe kweye issue za Masha kwa kuwa wanaandika kumfurahisha Mkurugenzi wao Mtendaji na si kuwapa kile kitu fair wasomaji wao

This is a point TUJIHADHARI tusijekuwa VIBARAKA wa MASHA na MENGI kama ambavyo dalili zinajionyesha wazi kweny bahadhi ya mitandao na magazeti, ugomvi wao sisi tutaishia kuwa washangiliaji wakati hata hatujui HASA wanagombania nini. TAFAKARI

mwanakijiji
02-17-2009, 04:38 PM
Mimi nadhani watu wana akili timamu:

a. Masha amekiri kuwa alikwenda Uswisi kwa mkutano wa UNHCR kama ilivyoripotiwa.
b. Masha amekiri kuwa ni kweli alipokea malalamiko. Imeandikiwa hivi "kuna kampuni zilizokuwa zimeomba zabuni hiyo ambazo zilituma wawakilishi wao kwake na kudai kuwa zinatendewa isivyo katika mchakato" - Anakiri kukutana na wawakilishi wa makampuni ya SAGEM na mengine (hataji walikutana lini, wapi na kwa namna gani na hao wawakilishi?
c. Katika kukiri kuwa alikutana na hao "wawakilishi" hatuambii uwezo huo wa kisheria yeye aliutoa wapi wa kuklutana nao? Je yeye ni sehemu ya watu wanaopokea malalamiko ya tenda kwa mujibu wa sheria!?

Inawezekana hawakukutana Uswisi au mbinguni, lakini kwa mujibu wa taarifa hii Masha alikutana na wawakilishi wa makampuni yaliyolalamika. Aseme lini na wapi?

mwanakijiji
02-17-2009, 05:19 PM
Hebu tuangalie hii habari inachosema hasa. Kumbuka nimesema hapo nyuma kuwa maneno nayo ni fani, ni wa wachache tunaimudu, Masha si mmojawao. Kama ilivyoandikwa na gazeti la The Citizen



Mr Masha told the press conference that in fact three bidders, and not one company as widely known, [B]informally raised concerns about vetting information that was not meant to be revealed before the pre-qualification process was complete.[/quote]

What does this "informally raised" means? Could it be during lunch, breakfast, or dinner, or something that we would consider to be "unofficial"? But even more interesting is "how did they informally raised" these issues. To me it sounds that the concern were not raised through a letter because that will make it official!

My interpretation is confirmed by how Habari Leo reported the same news conference concerning the same issue "Akielezea kilichotokea, Masha alisema wakati mchakato huo ambao ni wa siri ulipokuwa ukiendelea, kuna kampuni zilizokuwa zimeomba zabuni hiyo ambazo zilituma wawakilishi wao kwake na kudai kuwa zinatendewa isivyo katika mchakato"

What do you read here? According to Habari Leo Masha admitted that he met the representatives of some companies! Otherwise, how can you explain the statement "zilituma wawakilishi wake kwake"? This removes any doubt that the concerns were not raised through regular channels.

But more interesting is the question, where and when did he meet the representatives of these "four" different companies. Was it at the IA offices in Dar where I would supposed there is a guest book that these might have signed.


Mr Masha explained that he had himself advised his permanent secretary, Mr Patrick Rutabanzibwa, who is legally mandated to intervene to liaise with PPRA over the information raised by the four firms.

This is where Masha keeps entangling himself in the web of deception he is trying very hard to weave! If a: Patrick is the one "legally mandated to intervene to liaise with PPRA" when then did the four companies complain to the Minister who is not "legally mandated to intervene"? And why this complaints were given in an informal way through unnamed and undated channels? Masha knows the answers.


"I gave this advice as the minister who carries political responsibility here knowing that the leaked information immediately raised questions about the motives of those leaking it. I wanted to ensure the credibility of the entire process was safeguarded,"

This is very interesting. At face value one can sense a patriotic spirit, a desire to safeguard the welfare and interests of the nation. But looked closely we can see that Masha did not try to oppose this white elephant project! We at Cheche will explore this in our next issue. To us it doesn't matter who is the Minister of Internal Affairs, we stand opposing this misuse and abuse of public funds for this unnecessary, highly expensive and unneeded ID project!

If Masha wanted to be a hero, he should have opposed it through Cabinet meetings where he has powers like any other minister or even quit in opposition. By his continued support and defense of this ill-thought project Masha has shown lack of clear judgment of issues and an obvious weakness of persuasive skills.


Mr Masha said adding it would be hypocritical of those equating this move to manipulation.

If what he did was not manipulation of the first order, then manipulation has lost its meaning! Remember when one try to manipulates somebody its not because for wrong reasons, sometimes they will present very good reasons to justify such moves. I would argue that is what Masha did.



The minister said it was because of the PPRA�s advise that the final list of six firms that have been approved by the ministry to enter the bidding process was made from eight that were cleared by the tender evaluation committee.

Is he trying to suggest that without his intervention the tender board would have not reached the conclusions that it did reach? I think he does!



The list, he noted, does not include all the four firms that complained earlier and among them, Sagem Securite that a section of the media has linked his name with. He said another firm that was also left out had been cleared despite exhibiting similar weaknesses that saw others struck out and which could successfully be challenged ion court.

What about the six firms that are left? does he or his close associates have any vested interests in them that Mr. Masha need to disclose?


The minister, however said, any of the firms that feels aggrieved was free to seek justice in court as required. �But for now the law forbids them to participate in the process,� he said.

I'll bet a nickel that I know what companies will be the first one to challenge their denial in court. And I can even bet you a dollar that I know what law firm will represent them!


He said he was not acting on anyone�s behalf when he wrote the letter whose leakage from the ministry, he said, was being investigated by an internal committee to establish who was behind it and seal the loopholes.

This is sad, I hope he remembers what he wrote in the letter!


The minister also denied that he has ever met representatives of Sagem Securite in Switzerland or anywhere else as claimed and challenged those with evidence to produce it.

He already admitted that he did! I hope he doesn't have some memory problem!


He said reports have said he was in Switzerland on wrong dates and also failed to verify reports that Sagem Securite had been involved in corruption and banned from Nigeria. Mr Masha produced a letter from the Nigerian high commission in Dar es Salaam to show that the firm was still operating in Nigeria.

The Nigeria angle is irrelevant and immaterial!

People are missing some telling contradictions!

dickabudi
02-18-2009, 11:29 AM
Mwanakijiji

Masha asked why those who have a story of Sagem Securite malpractised does not go futher to explain that the firm was cleared on 2004 and is still working with Nigeria Government

Second as a Minister, entrusted by the President, he can either by writting or orally receive claims from various Stakeholder and he ellaborates that, at the first occassion he took the claim lightly, but when he still saw that there are shortcomings from the evaluation report which he was given by the Permanent Secretary its where he suggested for PPRA Consults ofwhich yielded a good result

He goes further to elaborate that the leaked letter was communication to his Superior which is self expalinatory, insisting on the full awareness of such decision because later on any shortcoming will be his 'baby'

mwanakijiji
02-18-2009, 04:51 PM
Mwanakijiji

Masha asked why those who have a story of Sagem Securite malpractised does not go futher to explain that the firm was cleared on 2004 and is still working with Nigeria Government

Second as a Minister, entrusted by the President, he can either by writting or orally receive claims from various Stakeholder and he ellaborates that, at the first occassion he took the claim lightly, but when he still saw that there are shortcomings from the evaluation report which he was given by the Permanent Secretary its where he suggested for PPRA Consults ofwhich yielded a good result

He goes further to elaborate that the leaked letter was communication to his Superior which is self expalinatory, insisting on the full awareness of such decision because later on any shortcoming will be his 'baby'

dickabudi, isome tena barua ya Masha kwa Waziri Mkuu uone jinsi ambavyo ilikuwa ni ya makusudi kupotosha. So far, nilichokisikia hadi hivi sasa ni kuwa Masha mwenyewe amekubali kukutana na hao wawakilishi kinyume na ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi.

dRU
02-18-2009, 06:44 PM
Inakuwa ni jambo la kushangaza kuona malumbano ya namna hii ya kiendelea wakati wao wahusika wanajua haswa nini kimetokea .. hakika hii ni ajabu ya shingo kukataa kulalia mto!!!! Wanatakiwa viongozi ambao wapo tayari kukubali mapungufu yao na hasa pale wanapokwenda mrama ni lazima wakumbuke kwamba mtu hujifunga kwa ulimi wake iwapo hutazungumza kwa hadhari...

mwanakijiji
02-18-2009, 06:50 PM
Inakuwa ni jambo la kushangaza kuona malumbano ya namna hii ya kiendelea wakati wao wahusika wanajua haswa nini kimetokea .. hakika hii ni ajabu ya shingo kukataa kulalia mto!!!! Wanatakiwa viongozi ambao wapo tayari kukubali mapungufu yao na hasa pale wanapokwenda mrama ni lazima wakumbuke kwamba mtu hujifunga kwa ulimi wake iwapo hutazungumza kwa hadhari...

Unajua ni almost impossible kwa mwanasiasa wa Tanzania kuomba msamaha akimaanisha kuwa amekosea kweli! Hata Waziri Mkuu mwenyewe alishindwa kuomba msamaha na badala yake akabakia kulia!

Baija Bolobi
02-19-2009, 01:20 AM
Aisee huyu utoto ndo unaommaliza.

dickabudi
02-19-2009, 11:44 AM
Mwanakijij nimeisoma tena barua ya Mh Masha na bado nikaona kuwa alichosisitiza kwa boss wake ni kwamba yeye kama Cheif Executive wa Wizara anaona ana umuhimu wa kuwa na taarifa na kujiridhisha kuwa taarifa ipo kwenye right track kabla haijaenda kwenye Baraza la Mawaziri kwani yakiharibika yeye ndiye wakuwajibishwa na hiyo imewatokea kina 'Mzee Ruksa' wakiwa kwenye wizara hiyo hiyo

Pia mwanakijiji nimewahi kuwa mwajiriwa katika serikali za mitaa (Halmashauri ya jiji) enzi za nyuma uendeshaji wa shughuli za kiserikali wanasiasa wanahoja za majungu majungu tu hivyo kwa mtizamo wa haraka haraka huwezi jua mpaka kitu kipite minutes sheets hujaa malumbano mengi yenye tija na yasiyo na tija, hoja za ajabu huanzishwa na wanasiasa na ndo mtindo wa kuendesha serikali

unaweza kuwa na maamuzi ya busara yakakwama kwa sababu kama hizo

Pili kupokea wawakilishi kwa aina yoyote si kosa, pia kuwasikiliza si kosa na kutoa dukuduku lako iwe ni lako binafsi au ni baada ya kupata mawazo ya wadau si kosa kwani hizo ndiyo kazi za mwanasiasia to work beyond the boarder for the interest of the ruling government

Mwanakijiji naomba nipe CODE OF CONDUCT ya wanasiasa tuone alichokiuka Masha kwenye kukutana na wawakilishi wa baadhi ya makampuni yanayowania tenda ya Kutengeneza vitambulisho vya Uraia Tanzania

Pili lets have the latest information je as per worldwide records SAGEM SECURITE ni among corrupt instittution? Are they working in Nigeria at this time? what was the outcome of their 2003 saga in Nigeria? how it ended? they were cleaned?
Latest information on other bidders, their history, their perfomance, their stand on corruption ili tulisaidie taifa kupata bidders clean, tukumbuke jukumu hili si la tender committe pekee ni letu sote, due deligence from any one itaokoa taifa

Pili nipe ushiriki wa IGP, Boss wa Immigration, Boss wa Fire Brigade na TAKUKURU tija yake ni nini? Na maamuzi yao yakipitiwa na wataaluma waliopo PPRA kwa uidhinisho au masahihisho nini kinapungua katika kuhakikisha fairness and transparency?

Kwa mtizami wangu atokee mtu ndani ya Tender Board au PPRA athibitisha kuwa Waziri Masha alishinikiza SAGEM wapewe tender kwa kuwashawishi ama kwa ahadi ya hela au hela kama zilivyo chaguzi nyingi za vyama vyote vya siasa yaani CCM, CHADEMA, CUF, TLP nk nitamwelewa lakini tafsiri ya barua ya Masha kwa Boss wake haijawa hoja maana kila mtu atatafsiri anavyotaka yeye iwe