PDA

View Full Version : Breaking News: Pinda aomba radhi



mwanakijiji
01-29-2009, 10:25 AM
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ameomba radhi kwa wale wote waliokwazika na kauli yake ya kutaka wauaji wa albino na wauawe papo hapo. Akizungumza Bungeni na hata kutoa machozi amesema alichokisema ni katika kuonesha kuwa serikali imechoshwa na mambo hayo ya kinyama.

Hata hivyo wabunge wa upinzani bado wanataka maelezo zaidi na ikibidi hatua zichukuliwe dhidi yake (aidha za kibunge) au za kisheria. Hata hivyo haijaonekana kama amefuta kauli hiyo na wanataka kusikia msimamo wake hasa ni nini.

Mpita Njia
01-29-2009, 12:52 PM
Ina maana kauli yake bado ip palepale! na yeye ni mwanashseria

dickabudi
01-29-2009, 02:01 PM
Kwa maoni yangu suala lisikuzwe kana kwamba kauli hiyo ni ya kwanza kwa Viongozi wawe wa Chama tawala au vyama vya upinzani kkumekuwa na maagizo mengi kwa Vijana wa vyama tofouti kusimamia haki hata kama gharama yake ni maisha, UVCCM wameagizwa hivyo, Green Guard wameagizwa na wengi wengineo

Maada iwe kuhakikisha kwa namna yoyote ile Albino na Vikongwe wana haki ya kuishi si malumbano ya kauli fulani iliamanisha nini na lengo ni ile tu Mh Mizengo aseme nimekosa nafikiri tunang'ang'ania kitu ambacho ni kidogo kuliko hao wanaozidi kuuwawa

Matigari
01-29-2009, 04:19 PM
Kosa moja halivunji ndoa. ( kosa moja haliachi mke)

Kabla ya yote tujiulize mzee pinda amefanya makosa mangapi katika uongozi wake. Pia tutahmini uongozi wake na uchapa kazi wake ukoje. Nadhani hii ni kasheshe ya kwanza kuisikia toka achukue uongozi, nisaidieni kama sivyo.

mwanakijiji
01-29-2009, 04:50 PM
Kosa moja halivunji ndoa. ( kosa moja haliachi mke)

Kabla ya yote tujiulize mzee pinda amefanya makosa mangapi katika uongozi wake. Pia tutahmini uongozi wake na uchapa kazi wake ukoje. Nadhani hii ni kasheshe ya kwanza kuisikia toka achukue uongozi, nisaidieni kama sivyo.

tatizo ni uzito wa kosa lenyewe. Mtu anayekuchapa kibao na mtu anayekudunga kisu kwa mara ya kwanza wote tunaweza kusema wamefanya "kosa moja". Uzito wake hata hivyo ni tofauti na matokeo yake yanaweza kuwa ni mazito yenyewe. HIvyo kosa moja linategemea uzito.

Alipotoa kauli yake wiki iliyopita wengi wetu tulisimamisha hukumu na kumpa kama alivyosema Dr. Mwakyembe "benefit of the doubt" ili asahihisha kauli yake. Aliporudia maneno hayo hayo jana kwenye "The Citizen" alikuwa amevuka mstari wa kosa "moja" na kuelekea na kuwa kile wenzetu wanakiita "repeat offender" kikwetu "sugu".

Hadi alipobanwa Bungeni ndiyo ametokea kujaribu kuhalalisha kauli hiyo bila kukubali uzito wake, kuitua n.k Anachojaribu kufanya ni kuelezea kuwa "nilikasirika sana ndiyo maana nilikuchoma kisu, kwa hiyo niwie radhi kwa kukufanya ukasirike kwa mimi kukuchoma kisu". Yaani hauna ubaya wa tendo la yeye kuchoma bali anasikitika umejisikia hasira!

Kutumia kisingizio kuwa "mimi ni mwanasheria" anaendelea kuthibitisha kuwa kuna sababu hata ya kumfutia leseni yake ya sheria (kama bado anayo) kwani Mwanasheria anayetangaza hadharani kuvunja sheria anapoteza sifa yake ya kuwa mwanasheria. Meya wetu hapa Detroit Kwame Kilpatrick leo anatumikia kifungo jela baada yakudanganya kwenye kizimba cha mahakama.

Wakati Jaji anatoa hukumu kama miezi mitatu iliyopita alizingatia ukweli mmoja kuwa Kwame ni Mwanasheria na hivyo kwa mwanasheria ambaye anajua uzito wa kusema kweli kwenye kiapo cha mahakama basi adhabu yake itakuwa kali na hatomuonea huruma.

Naamini kwa kadiri ya kwamba hataki kufuta kauli yake, kuomba radhi kwa kauli hiyo (siyo kwa kutukwaza bali kwa sababu ilikuwa na makosa) hastahili kuendelea na wadhifa wake. Kosa lake ni moja, lakini nikosa kubwa mno lenye matokeo ambayo yanazidi taamuli yetu.

Matigari
01-29-2009, 09:59 PM
Sawa mzee, naona una informnation nyingi kuliko nilizo nazo. Tusubiri tuone itakuwaje. najaribu tu kumuelewa kutokana na hasira tulizo nazo wote kuhusu mauaji ya zeruzeru ( I hope it is politically correct kuwaita zeruzeru if not forgive me) Binafsi naona aibu kwa niaba ya taifa langu kuwa tunaamini ujinga kama huo, tena mauaji ya hao ndugu zetu ni kitu kipya japo imani za kishirikina ni kitu cha siku nyingi.

Wakati mwingine tukiwa na jazba tunasema vitu vikali ambavyo hata hatufikirii kuvitimiza.

Kwa kifupi nimekuelewa na tuendelee kulitafakari hili. Have a good day.

QUTE
01-29-2009, 10:23 PM
MKJJ Heading yako inasema Pinda aomba radhi

Halafu hapa unasema,



Naamini kwa kadiri ya kwamba hataki kufuta kauli yake, kuomba radhi kwa kauli hiyo (siyo kwa kutukwaza bali kwa sababu ilikuwa na makosa) hastahili kuendelea na wadhifa wake. Kosa lake ni moja, lakini nikosa kubwa mno lenye matokeo ambayo yanazidi taamuli yetu.

mbona sijakuelewa?

Angeris
01-29-2009, 11:05 PM
Kufuatana na tukio lote la Mh. wazirii mkuu katika kupiga vita mauaji ya albino, ni kweli alikosea na kama ameomba radhi asamehewe kwasababu amekiri kutoa tamko ambalo lingeleta maafa nchini.

Lazima na yeye atakuwa ameona jinsi gani kauli yake imeifanya jamii kuzua maswali mengi. Muda mwingine mtu unapokuwa na jazba/hasira unaweza kutamka maneno ambayo yana madhara katika jamii/watu wanaokuzunguka. Tumsamehe kwakweli

Itakuwa imempa fundisho katika utendaji wake wa kazi. Next time, atakuwa mwangalifu anapotoa kauli zake.

mfumwa
01-30-2009, 11:17 AM
Kwa waungwana mtu akiomba radhi inabidi wakati fulani kumsamehe. Ila itategemea na uombaji wenyewe wa radhi. Pinda ni Waziri Mkuu, kauli ya Pinda ni kauli ya Serikali. Pinda akisema "anayeua Albino auawe", si sawa na Mfumwa akisema hilo. Hivyo Pinda alitakiwa kusema aliteleza katika kauli yake, manake yake yana athari kubwa sana kwa Taifa. Kumbuka si Albino tu wauawao TZ, kuna vikongwe na wengineo, jee watu wachukue sheria mkononi.

Nilikuwa nasikiliza BBC jana jioni, kweli kauli ya Pinda inatakiwa kusema aliteleza. Nasi kwa kuwa naye ni binadamu tutamsamehe.

mwanakijiji
01-30-2009, 05:43 PM
Unajua nimerudi tena kusikiliza hotuba ya Pinda jana.. na nimeona ametuchezea akili kweli!!

Mpita Njia
01-30-2009, 06:21 PM
Unajua nimerudi tena kusikiliza hotuba ya Pinda jana.. na nimeona ametuchezea akili kweli!!

Umegundua nini tena mkuu?

mwanakijiji
01-30-2009, 06:57 PM
Umegundua nini tena mkuu?

hajaomba msamaha kwa alichokisema!!! Sikiliza tena (kwenye podcast hapo). Yaani kazima hoja kiaina. Na zaidi ya yote hajasema kuwa watu wasiwauwe wanaotuhumiwa mauaji ya albino kuwa wawafikishwe kwenye vyombo vya usalama.

Mpita Njia
01-30-2009, 07:11 PM
hajaomba msamaha kwa alichokisema!!! Sikiliza tena (kwenye podcast hapo). Yaani kazima hoja kiaina. Na zaidi ya yote hajasema kuwa watu wasiwauwe wanaotuhumiwa mauaji ya albino kuwa wawafikishwe kwenye vyombo vya usalama.

Mi nilishaliona hilo tangu jana... cheki post number mbili nilishabainisha hivyo