View Full Version : Breaking News: Ajali nyingine Dar
mwanakijiji
01-30-2009, 09:24 AM
Habari kutoka JIjini Dar zinasema kuwa kuna ajali imetokea maeneo ya Kipawa karibu na uwanja wa ndege ambapo basi dogo la abiria limegongana na lori na watu kadhaa wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa. Tunaendelea kufuatilia habari hizo sasa hivi na tutawaletea taarifa zaidi kwa kadiri tunavyozipata (stay tuned).
Mpita Njia
01-30-2009, 09:55 AM
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema takriban watu sita wamepoteza maisha papo hapo
mfumwa
01-30-2009, 11:51 AM
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema takriban watu sita wamepoteza maisha papo hapo
Pole kwa wafiwa. Ajali zinazidi kuongezeka na kupoteza nguvu kazi ya Taifa, ama kuliongezea Taifa, ndugu na jamaa mzigo/gharama za kuwatunza majeruhi. Kweli sasa hili nalo ni janga kubwa kwa Taifa letu kama mauaji ya Albino. Serikali inatakiwa ikaze buti katika hili nasi wananchi tutoe ushirikiano.
Mpita Njia
01-30-2009, 12:36 PM
Kuna taarifa pia ajali nyingi, ikihusisha magari matati yakiwamo mabasi, imetokea leo asubuhi maeneo ya Mbezi
Mpita Njia
01-30-2009, 01:27 PM
Kamanda wa Polisi dar, bwana Kova amethibitisha kuwa watu tisa wamefariki na wengine 11 wamejeruhiwa
Angeris
01-30-2009, 02:36 PM
Mola awarehemu wapumzike kwa amani. Amen
January hii tumeomboleza vifo vingi vilivyotokana na ajali mbalimbali nchini.
Mpita Njia
01-30-2009, 04:26 PM
Kova ansema kuwa daladala lililohusika lilikuwa limefungiwa tangu 2007, lilikuwa likifanya kazi usiku tu.
Kilichotokea ni kuwa lori ya fuso, lililokuwa limebeba mchanga liligongana na semitrailer lililokuwa linatokea kando ya barabara. semitrailer likapinduka. Nusu saa baadaye (ilikuwa kama saa 10 usiku) ndipo lilipotokea hilo daladala lililokuwa limewabeba wauza nyama kutoka Pugu machinjioni na kulipamia semitrailer kwa nyuma. Ni ajali ya kutisha sana
mwanakijiji
01-30-2009, 05:03 PM
Duh.. sasa sijui tuseme vipi maana hata kutoa pole tu hakutoshi. Tusipoangalia mwaka huu utakuwa ni wa ajali sana. Sijui tufanye nini angala kupunguza madhara yake kama hatuwezi kupunguza wingi wa kutokea kwake.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.