PDA

View Full Version : Mada kuhusu TISS ziwe makini.

mkalipi
01-31-2009, 01:23 PM
Mengi yanasemwa kuhusu TISS, lakini hayatoshelezi kiu ya kutaka kufahamu zaidi. Mfano; je, ina maana miaka yote jamaa wa TISS walikuwa wamelala tu? Au kutokana na kazi yao ilivyo mema huwa hayasifiwi na mabaya tu ndio huonekana basi ndio wahukumiwe?

Kuhusu masuala kama KAGODA etc..Je, kitu kinachoitwa UNDERCOVER SECRET INTELLINCE OPERATIONS PROCEDURES (USIOP) kinajulikana kweli kwa watu wanaotoa mada zao mbalambali juu ya TISS? Katika USIOP kuna kitu kinaitwa FRONT COMPANY COVER. Kampuni inaanzishwa kwa malengo ya kulinda usiri wa operesheni za siri za kijasusi...(OPERATIONAL SECURITY COVER), hasa kwa zile operesheni ambazo utendaji wake na mtaji wa kuziendesha hautakiwi, kwa sababu za usalama, kujulikana na wanasiasa...wasije wakaleta zengwe...Kuna mambo ya vitu kama STRATEGICAL COUNTERTERORIST PROGRAMS, NATIONAL SECURITY OPERATIONS, n.k. Hivyo jamaa zetu wa siasa wakivijua, fumba fumbua, utawakuta majukwaani wanamwaga mambo hadharani oohh hivi ooh vile.

Kwahiyo ndugu zangu mkituma mambo fanyeni utafiti kwanza...msikurupuke!!
Mko hapo?

Mpita Njia
01-31-2009, 02:16 PM
Inaonekana kana kwamba kuna kitu umekiona mtu amekiandika halafu unaamua kumuonya. unaweza kutushiriksiha ni kitu gani hicho?

mwanakijiji
01-31-2009, 07:18 PM
Mengi yanasemwa kuhusu TISS, lakini hayatoshelezi kiu ya kutaka kufahamu zaidi. Mfano; je, ina maana miaka yote jamaa wa TISS walikuwa wamelala tu? Au kutokana na kazi yao ilivyo mema huwa hayasifiwi na mabaya tu ndio huonekana basi ndio wahukumiwe?

Kuhusu masuala kama KAGODA etc..Je, kitu kinachoitwa UNDERCOVER SECRET INTELLINCE OPERATIONS PROCEDURES (USIOP) kinajulikana kweli kwa watu wanaotoa mada zao mbalambali juu ya TISS? Katika USIOP kuna kitu kinaitwa FRONT COMPANY COVER. Kampuni inaanzishwa kwa malengo ya kulinda usiri wa operesheni za siri za kijasusi...(OPERATIONAL SECURITY COVER), hasa kwa zile operesheni ambazo utendaji wake na mtaji wa kuziendesha hautakiwi, kwa sababu za usalama, kujulikana na wanasiasa...wasije wakaleta zengwe...Kuna mambo ya vitu kama STRATEGICAL COUNTERTERORIST PROGRAMS, NATIONAL SECURITY OPERATIONS, n.k. Hivyo jamaa zetu wa siasa wakivijua, fumba fumbua, utawakuta majukwaani wanamwaga mambo hadharani oohh hivi ooh vile.

Kwahiyo ndugu zangu mkituma mambo fanyeni utafiti kwanza...msikurupuke!!
Mko hapo?

ulivyoandika ni kana kwamba ni wewe peke yako unajua mambo ya Intelligence. Jibu langu kwako ni fupi, hakuna watu wanaoweza kuabuse nafasi yao with impunity kama watu wa intelligence au wale wanaotumia kisingizio hicho.

Unachosema hapa unataka kiwe cover ya Ngowi lakini kama yeye ajuavyo na wengine tujuavyo, utetezi huo una matundu kuliko gunia. Yeye ni mmoja wa watu wanaotakiwa kutiwa pingu lakini kwa kisingizio hicho hapo juu anaendelea kupata na kujifanya kuwa sasa yeye shujaa.