mwanakijiji
11-05-2008, 09:51 AM
Habari Leo
Wafanyakazi sita wa Benki ya Barclays jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa tuhuma za wizi wa dola za Marekani milioni 1.8 (takriban Sh bilioni 2.16).
Mwendesha Mashitaka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyella, mbele ya Hakimu Mkazi Euphamia Mingi aliwataja watuhumiwa kuwa ni Winford Mwamonda (34), Shubira Mutungi (24), Neema Salia (26), Upendo Mushi (30), Margareth Longway (33) na Emmanul Mukono (40).
Kenyella alidai watuhumiwa wote wanakabiliwa na mashitaka tisa; la kwanza likiwa ni kula njama za kudanganya Oktoba 29, mwaka huu Dar es Salaam, wote waliiba dola za Marekani milioni 1.8. Katika shitaka la pili, washitakiwa wote Agosti 28, mwaka huu, wanadaiwa kughushi ujumbe wa kasi wa kibenki kuonyesha kwamba ujumbe huo ni halisi uliokuwa umetumwa kwenda Kigamboni Oil Limited kwa akaunti namba 0018001993 kuhamisha dola 299,974.000.
Shitaka la tatu ni kwa watuhumiwa wote kuwa Oktoba 27, mwaka huu Dar es Salaam kwa udanganyifu, walighushi ujumbe wa kasi wa kibenki wenye namba 000356 wa Oktoba 27, kuwa umetumwa kwa Ramadhani Hamisi kupitia akaunti 015701698 kwa dola za Marekani 80,500.
Shitaka la nne ni kwa watuhumiwa wote kuwa Oktoba 27, mwaka huu, walighushi ujumbe wa kasi wa kibenki wenye namba 00305 kuonyesha kwa ujumbe huo ni halisi ulikuwa umetumwa kwa Kigamboni Oil Limited kwa akaunti namba 0018001993 kwa dola 700,769.
Shitaka la tano kwa mtuhumiwa wa kwanza hadi wa tano ni kumwezesha mtu kutenda kosa la wizi, wakiwa waajiriwa wa Barclays Dar es Salaam, wakijua kuwa kuna maingizo ya uongo kwa akaunti 0008001993 kwa ajili ya Kigamboni Oil Limited na kupata dola 700,769 na 299,974.00, walikaa kimya bila kufanya chochote na kusababisha kampuni hiyo kuendelea na wizi wa dola 1,000 mali ya Barclays.
Shitaka la sita ni kwa mtuhumiwa wa kwanza hadi wa tano kuingiza maingizo yasiyo sahihi kwa Ramadhani Hamisi na kukaa kimya na matokeo yake Hamisi aliendelea na wizi huo wa dola 80,500 na shitaka la saba ni kwa mtuhumiwa wa pili, Oktoba 28, mwaka huu akiwa muingiza taarifa kwa udanganyifu, alifanya maingizo ya uongo kwa kutuma dola 299,974.00 wakati si kweli.
Shitaka la nane ni kwa mtuhumiwa wa pili kwa udanganyifu, alituma dola 80,500 kwenye akaunti 0157001698 ya Hamisi wakati ni uongo na shitaka la tisa ni kwa mshitakiwa wa sita kujaribu kuiba Novemba 3, mwaka huu makao makuu ya Benki ya Stanbic bila dai lolote halali, aliwasilisha hundi namba 0000002 na kuiba Sh milioni 60 na dola 40,000 kwa kutoa fedha hizo kutoka Gralic Inter Trader.
Kenyella alidai upelelezi wa kesi hiyo unaendelea kwa sababu washitakiwa wengine hawajakamatwa na pia fedha hazijakamatwa na kuomba kuwasilisha hati ya kiapo kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Charles Mkumbo, kuwa washitakiwa wote walikamatwa Barclays usiku na mshitakiwa wa sita, alikamatwa juzi Benki ya Stanbic Kinondoni.
Kenyella alidai washitakiwa wote walikamatwa kutokana na taarifa kutoka kwa viongozi wa benki za Barclays na Stanbic, na kushitakiwa kwa mashitaka hayo. Washitakiwa wote walikana mashitaka hayo na Hakimu Mingi alisema na uamuzi wa dhamana kwa washitakiwa atautoa kesho.
My Take:
Je hawa waambiwe warudishe tu hizo fedha yaishe?