PDA

View Full Version : Waziri Mkuu alimaanisha hatua kama hizi? (Picha)

mwanakijiji
02-05-2009, 04:08 PM
Global Publishers

Mauaji ya kutisha yaliyofanywa na wananchi wenye hasira dhidi ya kijana aliyejulikana kwa jina moja la Idd aliyetuhumiwa kutaka kuiba mbuzi kwenye banda eneo la Kigogo jijini Dar es Salaam, yamelaaniwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo.

http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1233817141_mwizi3.jpg

Licha ya kijana huyo kufumwa akiiba, wananchi hao walisikitishwa na namna kijana huyo alivyoteswa hadi kuuawa.
Ilielezwa na mwanamke mmoja mkazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Omari kuwa, mtuhumiwa akiwa na wenzake wawili walinaswa na wananchi majira ya alfajiri wakifanya jaribio la kuiba mbuzi kwenye banda la mzee mmoja (jina halikutajwa).

http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1233817141_mwizi2.jpg

Alisema mama huyo aliyeshuhudia unyama aliofanyiwa Idd kwamba, wakiwa kwenye harakati za kumtwaa mbuzi huyo, mwenye mali aliwaona na kuwapigia kelele za mwizi ambapo wananchi walijitokeza na kumnasa kijana huyo, huku wengine wakifanikiwa kukimbia.

?Walipomkamata walimvua nguo, wakaanza kumkata na viwembe, kumpiga kwa mawe huku wakimtaka atubu dhambi zake kabla ya kumtoa uhai.

Baadaye walimchoma moto hadi ngozi ikatoka akawa anahangaika, watu hawakujali wakaendelea kumtesa hadi alipokata roho,? alisema mama huyo kwa masikitiko.

Mwananchi mmoja mkazi wa Kigogo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kuwa, kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi kinatokana na watu kuchoshwa na vitendo vya kihalifu.

?Kwa mfano eneo letu vibaka ni wengi sana, watu wanaibiwa kila siku na wahusika wanakamatwa lakini siku mbili wanaonekana tena mitaani, ndiyo maana watu wanajichukulia sheria mkononi,? alisema Hamis Juma.

Hata hivyo, msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda Abdallah Msika amekuwa akiwaomba wananchi kutochukua sheria mkononi na kuwataka wawe wavumilivu wakati jeshi lake likiendelea kuweka mikakati ya kukomesha vitendo vya uhalifu nchini.

NB:
Naamini Waziri Mkuu alimaanisha kitu kama hiki. Ingawa kwenye kesi za wizi wa "mbuzi" adhabu ya kifo namna hii ni kitu cha kulaaniwa, nina uhakika kama jamii tuko tayari kuona wauaji wa albino wakipewa kibano namna hii na kuuawa papo hapo.

Kwa vile serikali imetoa kinga kwa wananchi kuchukua sheria mikononi, tusishangae kuona picha za namna hii zikidai kuwa "x ni muuaji wa albino". Waziri Mkuu ambaye alilia kuona mauaji ya albino sijui anaweza kujisikia vipi watu wakianza kutiwa moto, kupata kipigo namna hii kwa kisingizio cha "kutekeleza agizo la serikali".

outlier
02-05-2009, 04:26 PM
Duh! Watu ni wanyama eehhh!
Hii adhabu naona ni "disproportionate" kwa mwizi wa mbuzi! Lakini kwa wauaji wa albino- ukiacha mambo ya sheria na haki za binadamu, naona adhabu kama hii INAWAFAA SANA.

Angeris
02-05-2009, 09:45 PM
Ukijiweka kwenye nafasi ya huyo kijana hata kwa bahati mbaya inahuzunisha japokuwa alitaka kuiba. Inaonekana kabla hajafa aliteseka sana,ona ile ngozi ilivyobabuka kwa moto inasikitisha sana kwakweli.

Kuhusu wauaji wa albino, wafanywe lolote hata kunyongwa maana nao wanaua!
Nadhani Pinda tumeshamsamehe ila akiona hizo picha,kumbukumbu ya kauli yake itamjia na kujutia zaidi.

mwanakijiji
02-05-2009, 11:32 PM

Sasa kama wale wanaoua albino kinyama nao wauawe (kinyama bila ya shaka) na wale wanaoua wanaouua walioua albino na wafanywe nini na nani?

outlier
02-05-2009, 11:43 PM
Sasa kama wale wanaoua albino kinyama nao wauawe (kinyama bila ya shaka) na wale wanaoua wanaouua walioua albino na wafanywe nini na nani?

Wanaoua mbona zimekuwa nyingi mpaka zanachanganya! Wanaoua albino wauawe kinyama, SAWA. Wanaoua wanaoua albino wasifanywe kitu, kwa maana wataacha kuwaua wanaoua albino kama wanaoua albino wataacha kuwaua albino ama kwa kuwa watakuwa wamekwisha (kwa kuuawa kinyama) ama wataogopa!

Angeris
02-06-2009, 12:41 AM
Mwanakijiji,
Hatuwezi kukataa kuwa kauli ya PM ilituchanganya sana watanzania. Ili maisha yasonge vizuri tufanye kama hakusema yale maneno maana kila mtu alitoka na mtazamo wake juu ya yale maneno. Watu wangeuana sana tu, kwa vile kaomba msamaha basi amefuta kauli yake kwa maana nyingine.

kama ni wewe, uamuzi upi wa busara ungeutoa juu ya watu wanaoua albino na kuchukua viungo vyako kwa sababu mbalimbali?

Maana sasa unanichanganya. Au wewe hujamsamehe pinda? na kuona lile suala limepita?

mwanakijiji
02-06-2009, 01:37 AM
Wanaoua mbona zimekuwa nyingi mpaka zanachanganya! Wanaoua albino wauawe kinyama, SAWA. Wanaoua wanaoua albino wasifanywe kitu, kwa maana wataacha kuwaua wanaoua albino kama wanaoua albino wataacha kuwaua albino ama kwa kuwa watakuwa wamekwisha (kwa kuuawa kinyama) ama wataogopa!

sasa tukiwaacha wauaji kwa sababu wanaua wengine kwanini tusiwaache basi wauaji wale wanaoua wengine pia? Hatuwezi kuhalalisha mauaji ya kihololea ili kuzua mauaji ya kiholela. Kama tunataka kuwaua tuwaue ndani ya sheria!

mwanakijiji
02-06-2009, 01:39 AM
kama ni wewe, uamuzi upi wa busara ungeutoa juu ya watu wanaoua albino na kuchukua viungo vyako kwa sababu mbalimbali?

Wapelekwe mahakamani, ushahidi uoneshwe, wapewe nafasi ya kujitetea, ushahidi wa utetezi wao upimwe, mashahidi waletwe, wahojiwe, kisha baada ya kupima ushahidi wa pande zote mbili hukumu ifikiwe kwa kadiri ya uwezo wa mwanadamu.

Hukumu hiyo ikisema jamaa wameua kwa kukusudia (first degree) basi adhabu yao ni kifo (kwa sheria ya sasa). Hivyo basi adhabu hiyo iende kutekelezwa.

Maana sasa unanichanganya. Au wewe hujamsamehe pinda? na kuona lile suala limepita?

Hajaomba msamaha sasa tutamsamehe kwa vipi. Alilia tu.

outlier
02-06-2009, 06:50 AM
sasa tukiwaacha wauaji kwa sababu wanaua wengine kwanini tusiwaache basi wauaji wale wanaoua wengine pia? Hatuwezi kuhalalisha mauaji ya kihololea ili kuzua mauaji ya kiholela. Kama tunataka kuwaua tuwaue ndani ya sheria!

kuwapeleka mahakamani - wafungwe kisha wanyongwe itachukua muda mrefu, na mauaji maalbino watamalizwa, shortcut ni kuwaua nao kinyama. Wakishafanyiziwa kama watu ama watano watafyata wenyewe. Au sio!

dickabudi
02-06-2009, 12:14 PM
Mimi nimefurahi kuona picha ya kijana mwenyekosa dogo la kuiba mbuzi anavyokumbana na adhabu kubwa kama kuchomwa moto kwa maamuzi ya jazbz ya wananchi kweli ni adhabu kubwa inastahili kulaaniwa, pia mleta picha angetuletea picha ya wananchi wasio na hatia kuona pia wanavyoteseka kwa kupigwa nondo, roba za mbao kule mwananyamala, risasi zilizopoteza maisha hata ya Maprofessa kama Nicas Mahinda, ukiwa wanaoachiwa wajane na watoto wa raia wema wakivamiwa na makundi ya hao vibaka nako apime uzito wake, angetuwekea pia picha ya yule mtoto albino aliyepoteza mkono na sasa anauguzwa hospitalini tuuone uzuri wa kutokuchukua sheria mkononi, Pinda hahitaji kusamehewa wala kuomba msamahama, muuaji wa Albino atakapokamatwa itategemea mazingira aliyokamatwa nayo akipata wa kumfikisha Polisi anabahati, akipata wa kumhukumu ni sawa kabisa

Angeris
02-06-2009, 12:49 PM
Mwanakijiji,
Nahisi hili suala ni gumu kwa watu wengine kama wewe kuliko lilivyokuwa. Tumsubiri pinda aombe msamaha kama kule bungeni alilia tu,kwa jinsi ulivyosema.
Unajua sisi ni binadamu,muda mwingine kuna watu tunawaudhi na wanatuudhi sana hata kudiriki kukwambia atakuua halafu akaomba msamaha yakaisha. Ila lazima hiyo kauli ibaki akilini mwako,nikimaanisha hutasahau kuwa mtu alikwambia atakuua.
Nilikubali na bado nakubali kuwa PM alikosea sana na binafsi nimemsamehe kilio chake kimeidhinisha ujumbe fulani kwa jamii. Zaidi ya hapo siwezi kusema kitu, Sheria siijui vizuri sana.
Ila nakusalut mwkjj.

Mpita Njia
02-12-2009, 03:41 PM
hatimaye Pinda amesema jana alipokuwa anahojwia an TBC kuwa hakuwa anaulilia uwaziri mkuu kwa sababu huo ni mzigo ambao anatami kuutua

mwanakijiji
02-12-2009, 03:58 PM
hatimaye Pinda amesema jana alipokuwa anahojwia an TBC kuwa hakuwa anaulilia uwaziri mkuu kwa sababu huo ni mzigo ambao anatami kuutua

sasa si atafanya vizuri tu akiamua kuutua.. ?

Angeris
02-14-2009, 12:58 PM
halafu akiachia,nani amrithi??
Mwacheni Pinda jamani!