mwanakijiji
02-06-2009, 12:05 AM
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/national/klhnsiren.gif
KLHN/JF Exclusive:
Na. Mwandishi Wetu
Wabunge wawili wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dr. Wilbroad Slaa na Dr. Ali Tarab Ali wamekuta vyumba vyao vimetegeshwa vyombo ambavyo vinaamini kuwa kuwa ni vya kunasa mawasiliano bila ya wao wenyewe kujua. Habari kutoka Dodoma ambazo zimethibitishwa na Dr. Slaa zimesema kuwa ugunduzi huo umefuatia taarifa za kijasusi ambazo zilipenyezwa kwa waheshimiwa hao kutoka "vyanzo vya kuaminika" kuwa vyumba vyao vimetegeshwa vyombo hivyo na watu ambao KLHN inasita kuwataja kwa sasa.
Taarifa hizo ambazo zilipenyezwa mapema leo zilidokeza kuwa vyumba vya wabunge hao na bila ya shaka baadhi yao wengine viko katika uchunguzi katika jitihada ya kupata taarifa za nini waheshimiwa hao wanapanga, nani wanakutana nao na wanazungumza nini. Vyanzo vya udokezi huo wa habari za kijasusi ambavyo vimezungumza na KLHN kwa masharti ya kutotajwa jina, wadhifa au idara vinasema kuwa vifaa hivyo vya kielektroniki viliingizwa humo kwa njia za kiufundi wa hali ya juu na ilikuwa ni vigumu kugundulika.
Baada ya kupata taarifa hizo Dr. Slaa (Karatu- CHADEMA) hakuzipa uzito mkubwa sana hadi aliporudi hotelini (Hotel 56 iliyoko upande wa Mashariki wa Bunge - Geti la wageni) majira ya saa 12:30 za jioni. Baada ya kufuatilia na kuulizia wahudumu Dr. Slaa aliomba msaada wa kupekua pekua chumba hicho ili kuona kama taarifa alizopewa zina ukweli wowote. Hata hivyo wakiwa wamekata tamaa waliamua kuangalia chini ya godoro/kitanda na kwa sekunde chache walishangazwa na kukuta kifaa ambacho hawakukitambua kikiwa kinamulikamulika taa nyekundu.
Mara moja taarifa ilitolewa kwa Katibu wa Bunge, Polisi, na waandishi wa habari ambao waliwahi kufika hotelini hapo. Wakati hilo linafanyika Dr. Slaa alitaka kuona kama kati ya wabunge wanne waliopo pale ambao wako karibu naye kama wengine nao wamekabiriwa na kitu kama hicho. Wabunge wawili wa CCM ambao majina yao hayajafahimika hawakukuta kitu kama hicho isipokuwa Dr. Ali Talib Ali (CUF - Konde) anayepakana chumba na Dr. Slaa. Hivyo taarifa hizo nazo zilizidi kuwashtua wabunge hao na hasa lengo na madhumuni ya vitu hivyo.
Hadi hivi sasa vyombo mbalimbali vya usalama vilikuwa vinasubiriwa kufika hotelini hapo ili kuhakikisha kuwa vifaa hivyo ni vitu gani, vya nani, na vimewekwa kwa madhumuni gani.
Endapo itagundulika na kuthibitishwa kuwa vifaa hivyo ni vya kunasia sauti au kunasa mawasiliano itakuwa ni mara ya kwanza kwa kugundulika hadharani kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametegeshwa namna hiyo na zaidi ya yote itatishia uhuru wa wao kuzungumza, kukutana, au kuwasiliana na mtu yeyote kama raia huru. Zaidi ya yote wataalamu wa kisheria wameidokeza KLHN kuwa endapo hilo ni kweli "basi yeyote atakayekuwa amefanya hivyo atakuwa amevunja Katiba Ibara 18:1" inayotambua uhuru wa mtu binafsi na kukataza mawasiliano yake kuingiliwa nje ya sheria.
Kwa muda mrefu hata hivyo Dr. Slaa amekuwa akilalamikiwa kuvujisha siri za serikali na amewahi kutishiwa kukamatwa na Polisi kutokana na kudai kuwa anazo nyaraka mbalimbali za serikali. Hivi juzi baadhi ya viongozi wa serikali wameoneshwa kuchukizwa na kukerwa na Dr. Slaa kupata taarifa ya barua ya Waziri wa Mambo ya Ndani (anayesimamia Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji, Uokoaji) kwenda kwa Waziri Mkuu kuhusiana na suala la mradi wa Vitambulisho.
Hata hivyo haijulikani kama vifaa hivi vinahusiana kwa namna yeyote na shughuli za Dr. Slaa katika kuibua kashfa mbalimbali za ufisadi. Ikumbukwe kuwa ni Dr. Slaa na viongozi wengine wa upinzani walioibua ile orodha maarufu ya vitendo vya Aibu ambayo hadi hivi sasa baadhi ya walioatajwa wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na kashfa mbalimbali.
Katika kijarida chetu cha Cheche toleo la wiki hii na katika Mtandao wa JamiiForum, Dr. Slaa aliandika kuwapiga mkwara wale wote watakaojaribu kuficha au kuvuruga masuala mbalimbali ambayo wamekuwa wakiyafanyia kazi.
Juhudi za kupata uongozi wa Polisi zinaendelea na tutawapa taarifa pindi tukijua nini kinachoendelea mjini Dodoma.