View Full Version : Kuwafichua mafisadi wa ngono - Mjadala
mwanakijiji
02-09-2009, 04:46 PM
Kichwa cha Mjadala: Viongozi wa umma ambao wanamahusiano ya kingono na watumishi walio chini yao, au ambao wanamahusiano ya kingono nje ya ndoa zao ni lazima waumbuliwe, na wao wenyewe kuondolewa kazini au kuhamishwa ili kulinda maadili na nidhamu kazini. Watumishi wa ngazi za chini wanaohusishwa na vitendo vya ngono ni wahanga tu (victims) na hivyo wanastahili ulinzi wa kisheria na kinga pale wanapofichua advances za mabosi wao kwa mujibu wa SOSPA ya 1998!
Jadili: Je unakubaliana na hoja hii au la, na kwanini?
Kasharu
02-09-2009, 05:58 PM
Mimi naona ni sawa kabisa, lakini kitu kimoja naona siyo sahihi ni kwamba ingesomeka hivi, mtu yeyote anayejihusisha na ngono kazini lazima achukuliwe hatua za kinidhamu bila ya kujali cheo cha mtu. Aliyetongoza na aliyetongozwa akakubali wote lao moja.
Na kama kuna mtu anatumia cheo chake kutongoza, wamkatalie na kutoa taarifa panapohusika ili sheria itumike. Hayo ndo maoni yangu
mwanakijiji
02-09-2009, 06:49 PM

Kasharu, mara nyingi sheria inamlinda mtu aliye chini kwa sababu ya nafasi yake hawezi kuathiri moja kwa moja ajira ya aliye juu. Hivyo utaona kuwa sexual harrasment mara nyingi inadaiwa kufanywa na aliyejuu dhidi ya aliyechini (no pun intended).
Ni kwa sababu hiyo basi utaona mzigo wa kuwajibika unabebeshwa bosi kuliko tarishi au mhudumu kwa sababu wakati mwingine (kama siyo mara zote) yule mfanyakazi wa chini anajikuta anakubaliana na sexual advances za kiongozi wake kwa sababu ya kulindda ajira yake, mlo wake, n.k
Ni kwa sababu hiyo utaona kuwa inapogundulika kuwa kuna improper sexual relations, ni kiongozi anayetakiwa kujiuzulu au kuhamishwa na siyo mfanyakazi wa chini.
outlier
02-10-2009, 12:30 AM
Mimi naona ni sawa kabisa, lakini kitu kimoja naona siyo sahihi ni kwamba ingesomeka hivi, mtu yeyote anayejihusisha na ngono kazini lazima achukuliwe hatua za kinidhamu bila ya kujali cheo cha mtu. Aliyetongoza na aliyetongozwa akakubali wote lao moja.
Na kama kuna mtu anatumia cheo chake kutongoza, wamkatalie na kutoa taarifa panapohusika ili sheria itumike. Hayo ndo maoni yangu Mimi naona hii haijatulia sana. Chukulia scenario ya mtu anayefanya kazi katika idara fulani na hana exposure sehemu nyingine, yeye triangle yake ni kazini, nyumbani na sokoni/dukani- uhusiano wa kazini, kuanzia kwenye u-geli/boyi-frendi hatimaye ngono no baadaye uchumba na ndoa ndio chance yake. Sasa itakuwaje kama utamuadhibu mtu kama huyo. Na kuna watu kibao tu wameoana kwa kukutana kazini!! Na kuhusu mahusiano ya kingono kati ya bosi na mfanyakazi wa chini, kuna incidents ambapo mfanyakazi wa chini ndio anayemtega bosi mpaka bosi anaingia 'kingi' kwa hiyo kama kutakuwa na kuwaadhibu (kama wana ndoa zao) basi iwe adhabu kwa wote
ponda
02-10-2009, 10:28 AM
Kichwa cha Mjadala: Viongozi wa umma ambao wanamahusiano ya kingono na watumishi walio chini yao, au ambao wanamahusiano ya kingono nje ya ndoa zao ni lazima waumbuliwe, na wao wenyewe kuondolewa kazini au kuhamishwa ili kulinda maadili na nidhamu kazini. Watumishi wa ngazi za chini wanaohusishwa na vitendo vya ngono ni wahanga tu (victims) na hivyo wanastahili ulinzi wa kisheria na kinga pale wanapofichua advances za mabosi wao kwa mujibu wa SOSPA ya 1998!
Jadili: Je unakubaliana na hoja hii au la, na kwanini?
M.M.M. Naona umeamua nimekuona umepost hata kwenye ze utamu. mimi najiuliza kwanini umeegemea kwenye viongozi tu? suala la mtu na mahusiano ya ndoa naona limekaa kibinafsi zaidi na kama ni kuumbuana isiwe kwa viongozi tu iwe kwa WATU WOTE?
Hata hao watumishishi unaowasema wa chini umejaribu kuangalia ni kiasi gani wanachangia kuwarubuni maboss wao wakitegemea kupata favour fulani fulani?
mimi nadhani kama ni uharifu wa ngono tuangalie unyanyasaji wa maofisini lakini mambo ya mahusiano nje ya ndoa tunaenda mbali na kama tukiamua hivyo basi iwe kwa wote na sio kuwaengua wale uliowatetea kwenye ze utamu.
NB. Nitaomba radhi endapo jina nilili liona kwenye ze utamu halihusiani na wewe moja kwa moja na pia nasisitiza tuangalie tusijegeuza mtandao huu ukawa wa UDAKU kwa kujikita kwenye issues binafsi zaidi kuliko matatatizo yetu na THE TANZANIA WE WANT.
Angeris
02-10-2009, 02:35 PM
Hii hoja ni nzito sana kuipatia ufumbuzi pindi tunapoijadili.
mwanakijiji
02-10-2009, 06:18 PM
M.M.M. Naona umeamua nimekuona umepost hata kwenye ze utamu. mimi najiuliza kwanini umeegemea kwenye viongozi tu? suala la mtu na mahusiano ya ndoa naona limekaa kibinafsi zaidi na kama ni kuumbuana isiwe kwa viongozi tu iwe kwa WATU WOTE?
Kanuni yangu ni kuwa watu wote hawatuhusu! Unalofanya wewe na mke wako au na mpenzi wako mimi halinihusu halimradi alihusiani na kuvunja sheria au fedha za walipa kodi. Viongozi wa umma ni fair game kwa sababu aidha waliomba kura, au wanalipwa kutoka kodi zetu! So mambo wanayoyafanya jamii inahaki kuyatambua na kuyaumbua.
Hata hao watumishishi unaowasema wa chini umejaribu kuangalia ni kiasi gani wanachangia kuwarubuni maboss wao wakitegemea kupata favour fulani fulani?
Hiyo siyo defense; katika sheria za maadili ya kazi burden of proof iko kwa Bosi, kama bosi anaona anategwa na mfanyakazi wa chini, anamsimamisha kazi, anamshtaki kwa mtu mwingine au anamtimua. Hatakiwi kukubaliana naye. Mara nyingi tunachofanya wakati mwingine ni kumuita huyo dada na kumuambia mbele ya shahidi kuwa hizo advances zake hazitakiwi kazini na kama hawezi kujizuia atatimuliwa kwani there is no tolerance linapokuja suala la sexual harassment.
mimi nadhani kama ni uharifu wa ngono tuangalie unyanyasaji wa maofisini lakini mambo ya mahusiano nje ya ndoa tunaenda mbali na kama tukiamua hivyo basi iwe kwa wote na sio kuwaengua wale uliowatetea kwenye ze utamu.
Mahusiano ya nje ya ndoa au ya wapenzi wawili bado yanabakia ni kwa watu wenye ndoa zao. Hadi pale tutakapotengeneza molarity policy wa kuangalia mtu anafanya nini chumbani kwake hatuna business ya kuingilia maisha ya watu binafsi! Period.
NB. Nitaomba radhi endapo jina nilili liona kwenye ze utamu halihusiani na wewe moja kwa moja na pia nasisitiza tuangalie tusijegeuza mtandao huu ukawa wa UDAKU kwa kujikita kwenye issues binafsi zaidi kuliko matatatizo yetu na THE TANZANIA WE WANT.
Hapana uliyeona kwenye utamu ni mimi ndiyo nimewaandikia. Ukweli utabakia vile vile kuwa tulipofika sasa tumevuka mpaka wa kufichua ufisadi wa ngono na kufikia kuharibu maisha ya watu kwa kuwatukana hadharani tukijua kuwa hawawezi kutujua. Mtu hadi unaogopa kupiga picha kwa sababu hujui picha yako itaishia wapi.
ponda
02-11-2009, 04:03 PM
[QUOTE=mwanakijiji;2403]Kanuni yangu ni kuwa watu wote hawatuhusu! Unalofanya wewe na mke wako au na mpenzi wako mimi halinihusu halimradi alihusiani na kuvunja sheria au fedha za walipa kodi. Viongozi wa umma ni fair game kwa sababu aidha waliomba kura, au wanalipwa kutoka kodi zetu! So mambo wanayoyafanya jamii inahaki kuyatambua na kuyaumbua.
SASA WEWE UNA UHAKIKA GANI KAMA WANATUMIA PESA YA WALIPAKODI KUFANYA NGONO??????
KAMA KAVUNJA SHERIA YA KIAPO KATI YAKE NA MKE WAKO WEWE INAKUHUSU NINI WAKATI UMESEMA YANAYOHUSU MTU NA MKE WAKE HAYAKUHUSU WEWE?
mwanakijiji
02-11-2009, 07:29 PM

unaona sasa hapo ndipo lililo la msingi.. sheria ya maadili ya viongozi inawahusu viongozi na ni wao wenyewe waliipitisha. So, kwa kukubali kuandika sheria hiyo, ni wao wenyewe wametulazimisha kufuatilia mambo yao. Hata sheria ya makosa ya kujamiiana nayo ni hivyo hivyo. Kama hawataki wafuatilie mambo yao kwa vile wao ni viongozi wanachotakiwa kufanya ni kuzifuta tu sheria hizo. So, ni wao wamefanya mambo yao binafsi kuwa our business!
Mpita Njia
02-12-2009, 10:49 AM
Sioni kama kuna ubaya wowote kwa kiongozi kuwa na mahusiano ya kingono na mtumishi aliye chini yake iwapo tu; walikubaliana; mahusiano yao hayaingilii kazi zao; mahusiano yao hayana madhara kwa kazi zao. Mimi naona mahusiano kama haya ni masuala binafsi. Kama mtu umetokea kumpenda, awe kiwete, tajiri, mfupi, ana kazi hana kazi, bosi wako, junior wako-utampenda tu kwa sababu moyo ndio unasukuma hilo pendo,. kama mtu atapenda kwa sababu ya kitu fulani, mfano maumbile au fedha, hapo kuna tatizo.
Kuna sababu gani ya kumkata mtu kwua na mahusiano ya kingono na junior wake kama mahusiano hayo hayaathiri kazi zao?
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.