PDA

View Full Version : News Alert: Mengi awashukia wabaya wake tena!



mwanakijiji
02-10-2009, 04:49 PM
TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa muda mrefu sasa, magazeti yanayofadhiliwa na watuhumiwa wa ufisadi yamekuwa yakiandika mambo mengi yaliyojaa fitina na uongo dhidi yangu na familia yangu. Kwa mfano:-

• Mengi anataka kumng'oa JK 2010?
• Mengi hatari kama Hitler
• Ndoa ya Reginald Mengi na CHADEMA yabainika
• Mengi na kashfa ya ufisadi – Tume ichunguze bilioni 40 za ukimwi.
• Mengi aoa tena – harusi yafungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kanali Fabian Massawe

Taarifa zote hizi ni za uongo mtupu.

Kama nilivyokwishasema awali, mafisadi wanaotuhumiwa kuiba fedha za umma ambazo zingetumika kwa kujengea shule na kupiga vita maradhi na umaskini wamekuwa wanazitumia fedha hizo kwa maslahi yao binafsi kwa kujijengea majumba ya kifahari huko Dubai, Uswisi na Afrika ya Kusini, na kubwa zaidi, sasa wanazitumia kudhoofisha nguvu zinazopiga vita ufisadi.

Mafisadi hawa wameanzisha magazeti zaidi ya 15 ambayo yanasambaza fitina na uongo uliotungwa. Nia na madhumuni ya mafisadi kutunga na kusambaza fitina na uongo ni kuufanya umma uelekeze nguvu na mawazo yao katika fitina na uongo huo na kuacha kufikiria na kuzungumzia tatizo kubwa la ufisadi.

Fitina na uongo wa mafisadi hawa ni sumu inayosambazwa ndani ya jamii na inaweza kujenga chuki, kuwagawa wananchi na kuvuruga amani. Iwapo vurugu zitatokea, basi mafisadi hao wataanza hata biashara mpya ya kuuza silaha ili Watanzania wazitumie kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Wengi wa mafisadi wanaishi maisha machafu mno. Hadi hapo Baraza la Habari Tanzania (MCT) litakapotoa msimamo wake juu ya uandishi wa mambo ya faragha (privacy) endapo waandishi wa habari wanaoheshimu taaluma yao ya kuandika ukweli wataandika uchafu wa maisha hayo, wasilalamike.

Ninarudia tena kusema kwamba ni lazima mafisadi waelewe kwamba kutapatapa kwao ni jitihada za wafamaji kwa sababu moto wa vita dhidi yao umekwishawaka na hawawezi kuuzima au kuukwepa. Hautazimika kamwe, na jitihada zao za kudhoofisha nguvu za vita dhidi ya ufisadi zitageuka kuwa kichocheo cha moto huo hata kama watafanikiwa kuwatokomeza watu wanaopiga vita ufisadi.
____________________
Reginald A. Mengi
Mwenyekiti Mtendaji
IPP Limited
10 Februari,2009

ponda
02-10-2009, 05:15 PM
Huyu naye mzee wa kulia lia hachoki??? Kazi kutafuta sympath kwa watu, kila akisemwa yeye analia na mafisadi is he untouchable?

mwanakijiji
02-10-2009, 06:11 PM
Huyu naye mzee wa kulia lia hachoki??? Kazi kutafuta sympath kwa watu, kila akisemwa yeye analia na mafisadi is he untouchable?

yawezekana una point lakini kama hivyo vichwa vya habari hapo juu ni vya kweli, wewe huoni tatizo au kwa vile ni Mengi basi anatakiwa kunyamaza?