PDA

View Full Version : Sisi ni watu wa ajabu duniani?



mwanakijiji
02-11-2009, 07:33 PM
Date::2/11/2009 (mwananchi)

Waziri Mkuu, wabunge waalikwa tamasha la albino Dar
Na Clara Alphonce

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la kupiga vita mauaji ya walemavu wa ngozi (albino) lililoandaliwa na Umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.

Katibu Mwenezi wa UV- CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara alisema kuwa tamasha hilo lililobeba ujumbe wa ' kila kijana ni mlinzi wa albino' litafanyika kesho kwenye Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam

Alisema nia ya tamasha hilo ni kuunga mkono hatua ya serikali ya kukemea mauaji ya albino yanayoendelea nchini kote.

Manara alisema mbali na Waziri Mkuu Pinda, pia kutakuwa na wabunge mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova ambao watatoa ujumbe wao kuhusu mauaji hayo.

Manara aliwataja wasanii mbalimbali watakao tumbuiza katika tamasha hilo kuwa ni TID, Prof. Jay, Soggy Doggy, Wanaume Halisi na Wanaume TMK wakati bendi zitakazotumbuiza ni Msondo Ngoma, FM Academia, Vibration Sound na kwa muziki wa taarab, East African Melody.

My Take:
what is wrong with this picture?

ponda
02-11-2009, 07:45 PM
Vijana wa CCM wanaunga mkono matamshi ya PM. na kuitikia wito kuwa "Vijana wa CCM wako wapi wakati haya yote yanatendeka?????

mwanakijiji
02-11-2009, 10:24 PM
Vijana wa CCM wanaunga mkono matamshi ya PM. na kuitikia wito kuwa "Vijana wa CCM wako wapi wakati haya yote yanatendeka?????

Lakini wanaunga mkono kwa burudani na muziki n.k lakini wao wanasema wanaunga mkono hatua ya serikali "kukemea".... kwa mtindo huu natumaini serikali itabidi iwe inatoa "makemeo" mengi tu..

Angeris
02-12-2009, 03:56 AM
Kinachouma zaidi unaweza kusikia baada ya hilo tamasha, albino mwingine kauawa au nusu akatwe kiungo kimojawapo mwilini.
Wasigeuze tu burudani,hao wenzetu wanahitaji ulinzi na kuhakikishiwa maisha yapo salama katika jamii waishiyo siyo kuwafanyia matamasha mara huku mara kule.