PDA

View Full Version : Kuku wa Limao



mwanakijiji
11-10-2008, 06:58 AM
Bibi Aziza wa Gumzo alitoa maelekezo yafuatayo:

Mahitaji:

Nyama ya kuku ,
maji juisi ya limao ,
nyanya,
chumvi,
mvinyo wa kupikia ,
vitunguu maji ,
tangawizi.

Maelekezo
Osha nyama ya kuku halafu uikate iwe vipande, koroga pamoja na chumvi, mvinyo wa kupikia, pilipili manga, tangawizi na vitunguu maji. Koroga maji juisi ya limao pamoja na unga, chumvi, pilipili manga, yai na mafuta.

Washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria, weka vipande vya nyama ya kuku kwenye unga uliokorogwa, halafu weka ndani ya sufuria vikaange, halafu vipakue.

Washa moto tena, mimina maji kwenye sufuria, halafu tia chumvi, sukari, maji juisi ya limao, korogakoroga halafu mimina maji ya wanga, korogakoroga, tia vipande vya nyama ya kuku korogakoroga vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Razz Razz Razz Razz Razz Razz Razz Razz

ukimaliza kula futa mdomo. Very Happy

My more
11-30-2008, 02:07 AM
Bibi Aziza wa Gumzo alitoa maelekezo yafuatayo:

Razz Razz Razz Razz Razz Razz Razz Razz

ukimaliza kula futa mdomo. Very Happy

Hallo hallo:):):)

duru langu
11-30-2008, 02:23 AM
ungali liokorogwa kivipi? na maji pekee au na maji na vikorombwezo vingine?

mmmh huu msosi utakuwa wa aina yake maana yake, pilipili, sukari, chumvi, mvinyo,
juisi n.k. vyote kwa mpigo! ama kweli mapishi ni ubunifu :)

Kepa
12-07-2008, 11:50 PM
ungali liokorogwa kivipi? na maji pekee au na maji na vikorombwezo vingine?

mmmh huu msosi utakuwa wa aina yake maana yake, pilipili, sukari, chumvi, mvinyo,
juisi n.k. vyote kwa mpigo! ama kweli mapishi ni ubunifu :)

Ndio maana wabunifu hutuwekea mapishi hapa ili na siye wengine tufaidi utamu.

MEGZ
12-12-2008, 12:00 PM
naomba niulize, huo unga wa kukoregea unakuwa wa ngano au wa sembe?