PDA

View Full Version : Spika Sitta: Umechagua CCM kuliko Taifa?



mwanakijiji
02-12-2009, 07:41 AM
Hii ibara ya 15:1 ya Katiba ya CCM ni lazima ifutwe kama hawa CCM wanaweza kujadili mambo kwa uhuru. Vinginevyo kwa mtindo huu tutafika pabaya sana. Inasikitisha kuona kana kwamba Spika Sitta ameanza kulewa sifa zisizo na maana na matokeo yake ni kuanza kuliburuza Bunge na papo hapo kuliburuza Taifa.

Kuna jaribio la kulifanya Bunge liwe juu ya Urais na Mahakama:
Mara ya kwanza alisifiwa pale alipompasha Rais Kikwete na kumtaka awe "mkali kidogo" na watu wakampongeza kwa kuweza kusema/kuelekeza ukweli kwa Rais na watu waliona kuwa ni kitu ambacho hakikuwahi kufikiriwa.

Hivi majuzi amegongana na Mahakama na kimsingi kampiga mkwara Jaji Mkuu kitu ambacho ninakipinga kabisa.

Chochote anachopanga kufanya, hivi sivyo jinsi ya kwenda kwani it will backfire!

kishazi
02-12-2009, 11:15 AM
Tatizo la viongozi wetu hawawezi kutofautisha siasa(chama)na utaifa kama taifa sasa yeye anaweza akawa ametoa kauli ya kisiasa bila kufikiria utaifa kwanza na madhara ya kauli kwa taifa hapo mbeleni .

mwanakijiji
02-12-2009, 06:48 PM
Nadhani baada ya matukio ya mwaka jana kule Bungeni hadi kuanguka kwa Waziri Mkuu Lowassa wabunge wa CCM wamejikuta hawana jinsi isipokuwa kubanana mumo kwa mumo.

Mpita Njia
02-14-2009, 12:07 PM
Tatizo la viongozi wetu hawawezi kutofautisha siasa(chama)na utaifa kama taifa sasa yeye anaweza akawa ametoa kauli ya kisiasa bila kufikiria utaifa kwanza na madhara ya kauli kwa taifa hapo mbeleni .

Tatizo si viongozi, mfumo wetuw a uongozi an utawala hauzingatii mgawanyo huo

Japhet
02-15-2009, 01:14 AM
Kama Spika anaongoza Bunge kwa misingi ya kanuni za Bunge, tatizo liko wapi???? ubaya ni kukiuka kanuni pamoja na Katiba ya nchi. Pia Katiba ya Tanzania itabadilishwa au kurekebishwa mara ngapi??? Kwani siku hizi naona "marekebisho ya katiba umekuwa wimbo mitaani"....Kwa maoni yangu, nadhani katiba inabidi irekebishwe kwa misingi ya Maslahi ya taifa na wala si kwa ajili ya watu wachache wenye maslahi binafsi.