PDA

View Full Version : Serikali kufungia magazeti leo au kutoa matamko?



mwanakijiji
02-12-2009, 09:40 AM
Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kupitia idara ya Maelezo leo inatarajiwa kutoa tamko kuhusu mwelekeo wa uandishi wa vyombo vya habari kufuatia malumbano na migongano ya maneno yenye kuashiria kuvunjika kwa maadili ya kiundishi hususan kuingilia habari za kibinafsi za maisha ya watu jambo ambalo linaonekana kuanza kuwakera viongozi mbalimbali. Pamoja na serikali baraza la vyombo vya habari nchini (MCT) nalo linatarajiwa kutoa tamko katika kile kinachoonekana kuitikia wito wa mmiliki wa vyombo vya IPP aliotoa juzi kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu madai ya kuzushiwa habari mbalimbali za uongo.

Matamshi hayo ambayo yanatarajiwa kutolewa muda si mrefu ujao yanatarajiwa kutoa maangalizo kuhusu haja ya vyombo vya habari kuheshimu uhuru wa watu na maadili ya jamii yetu.

Msimamo wa KLHN ni kuwa uamuzi huo wa kutoa matamko umechelewa na inaonekana unakuja baada ya moto wa malumbano hayo kuanza kuunguza pabaya. Siku za hivi karibuni magazeti mbalimbali ambayo yanadaiwa kuwa na watu wakubwa nyuma yake yamekuwa yakitumika kurushiana madongo, kashfa, uzushi na madai ambayo kwa mtu yeyote mwenye akili timamu ataona kuwa yana walakini.

Kwa muda mrefu tumeandika na kupiga kelele kuhusu suala hili na hata katika kijarida chetu cha Cheche tumelitolea maoni jambo hili tena. Tunasikitishwa kuwa kwa muda mrefu serikali imekaa kimya ikiangalia na kukodolewa uchafuzi wa hewa ya habari nchini ambapo watu wachache wenye nguvu za kisiasa na kiuchumi wamewageuza watanzania kuwa vikaragosi vyao kwa kuwatupia kila aina ya habari huko wao wenyewe wakitengeneza mamilioni ya fedha. Tunasikitika kuwa kwa muda mrefu baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kinyume na kundi moja huku vikiamini kuwa vina kinga na baraka ya watawala.

Licha ya kutambua mabadiliko yaliyotokea siku chache zilizopita ambapo vyombo vingine vimeibuka kuanza kujibu mapigo, tunasikitika kuwa kuna watu wameona kuwa jambo hilo ni la lazima baada ya serikali kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuchukua hatua. Wakati serikali haikuweza kuvumilia mara tatu suala la MwanaHalisi na habari ya kumng'oa Rais Kikwete, kwenye masuala haya ya vitandani mwa watu na kwenye vyumba vya watu yamevumiliwa kwa muda mrefu kana kwamba hakuna utawala wa sheria nchini.

Wito wetu leo siyo tu kwenye masuala haya ya watu binafsi wanaogombana kupitia vyombo vya habari bali pia vyombo vile ambavyo vinatumika kutangaza habari za kingono na mambo ya ufuska kama kwa kuyatukuza huku vikiweka picha mbalimbali ambazo ni wazi zinavunja kanuni za Adhabu na sheria mbalimbal zinazohusiana na masuala ya uchapishaji, utangazaji n.k

Haitoshi kwa serikali leo kutoa matamko ya kumuonya mtu au kukemea, tunachotarajia ni kuona serikali ikichukua hatua madhubuti ya kufungia vyombo vyote vya habari ambavyo vimevuka mpaka wa maoni huru na kuwa katika eneo la kukashfiana na kuharibu maadili ya watoto (deliquency of minors). Tunatumaini kama serikali inaona kuwa mambo yanayofanywa ni sehemu ya uhuru wa maoni au habari, basi wakati umefika kwa serikali kuanzisha sera na hatimaye sera itakayoratibu habari za kingono, filamu, na vitu kama hivyo kwa watu wazima ili vipatikane katika mazingira yanayotakiwa, vikiratibiwa na kusimaiwa kisheria kuliko ilivyo sasa ambapo badala ya kuita kuwa ni mambo ya kingono (pornography) tumeamua kuvipatia jina la "udaku".

Hata katika nchi ambazo wengi wetu tunaonekana kuziiga mambo ya kingono yanaongozwa na sheria sawia na majarida au magazeti yenye habari za namna hiyo hayapatikana kiurahisi au waziwazi kama ilivyo nchini. Tunarajia serikali itahakikisha kuwa watu wazima wanapata uhuru wa kuona na kusoma kile wanachotaka kwa mujibu wa sheria na ya kuwa watoto wetu na public square or airwaves haviharibiwi kwa kuacha kundi la watu wachache kutawala hadi kwenye macho na masikio yetu.

Tunachotarajia leo siyo maneno matupu, bali hatua kali na za mfano, ili hatimaye kwa kutumia sheria kulazimisha kina cha uandishi, habari za kuvutia, na maadili yanazingatiwa katika fani hii. Vinginevyo, kama wanachotaka ni kukemea "tabia iliyojitokeza" tumeona kuwa sisi tutanguliwe kuwakemea kwa uzembe na kufumbia macho uposhaji mkubwa wa maadili.

Mpita Njia
02-12-2009, 10:08 AM
Wizara na Idara zimejiingiza kwenye siasa kiasi kwamba hata wakitoa hilo tamko, hata liwe na maneno makali ya aina gani, wananchi watayaona kama kichekesho tu. Mkuchika kila anapozungumza watu wanamuona kama anazungumza kuhusu propaganda za CCM.
Kwa maoni yangu-ni kweli wamechelewa , si kutoa kauli bali kuchukua hatua. Sheria zipo, zimeshawahi kutumika kuadabisha wengine huko nyuma, sasa kinachoogopwa ni nini? wala hawatakiwi kutoa kauli, bali kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Mpita Njia
02-12-2009, 05:28 PM
Mkuchika kamaliza press conference sasa hivi-ametoa siku saba wka magazeti ya Taifa Letu, Sema Usikike na Taifa Tanzania kutoa maelezo kwa nini yasichukuliwe hatua kutokana na kukiuka maadili ya uandishi

mwanakijiji
02-12-2009, 06:43 PM
Michuzi

Magazeti ya Taifa Tanzania, Taifa Letu na Sema Usikike yamepewa siku saba yajieleze kwa nini yasichukuliwe hatua za kisheria kwa kuandika habari za kukashifiana, uzushi, uchochezi na uongo. Na yametakiwa kuwa yamefanya hivyo ifikapo Februari 19 mwaka huu saa 10 jioni.

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, amesema hayo leo alipokuwa akitoa tamko la Serikali kuhusu mwenendo wa vyombo vya habari nchini.
Amesema Serikali imesikitishwa na mwenendo wa magazeti hayo na hairidhiki na mwenendo huo, kwani yanakiuka Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, ambayo alisistiza kuwa itaendelea kutumika hadi itungwe nyingine.
Akifafanua, Mkuchika alitolea mfano wa Taifa Tanzania toleo la Februari 6-12 mwaka huu, lililomshambulia Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi kwa kuandika kuwa harusi yake imezua utata na la Taifa Letu la Februari 9 mwaka huu, lililoandika kuwa Karamagi (Nazir) anadaiwa kudandia wake za vigogo wenzake.

Pia Waziri alizungumzia Sema Usikike toleo la Februari 10 mwaka huu lililoandika kuwa Waziri "Mkuu wa zamani amweka kimada shoga...".

Kutokana na hali hiyo, Waziri aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuacha mara moja kutumia vyombo vyao kwa maslahi binafsi yanayoweza kuhatarisha amani na utulivu.

Pia aliwataka wahariri wa habari kuacha kuandika na kushabikia habari za watu binafsi ambazo hazina maslahi kwa Taifa.

Waziri aliwataka wamiliki na wahariri hao kuzingatia kifungu cha 30(1)(2) cha Katiba ya nchi kisemacho: "...kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma, haviathiriwi na matumizi mabaya ya Uhuru na Haki za Watu Binafsi."

Mpita Njia
02-13-2009, 07:28 PM
Prince Bagenda (mwenyekiti wa bodi ya uhariri ya Taifa Tanzania) amesema wamepokea barua ya serikali leo asubuhi na wanajiandaa kuijibu lakini anaonyesha kutetea habari ya Mengi kuoa waliyoichapisha kwa maelezo kwua ni mtu maarufu ambaye mambo anayoyafanya yana public interest

Dua
02-18-2009, 01:18 AM
Public interest of stupidity? How much money do they fleece from the government? It?s all there to be seen even by a blind person.

When teachers are canned the power that may be can act decisively but when scandals from EPA, Richmond et al the culprits should wait for the courts to decide. Stupidity of the highest degree.

cute
02-18-2009, 01:26 PM
Public interest of stupidity? How much money do they fleece from the government? It?s all there to be seen even by a blind person.

When teachers are canned the power that may be can act decisively but when scandals from EPA, Richmond et al the culprits should wait for the courts to decide. Stupidity of the highest degree.

I like this Dua.