View Full Version : Mkuchika alikuwa wapi?
mwanakijiji
02-13-2009, 09:50 AM
Kuna msomaji wetu mmoja kauliza swali zuri sana na lenye mantiki kufuatia maagizo ya Waziri wa Habari Kapt. Mkuchika kutoa siku saba kwa magazeti matatu kuelezea kwanini wasichukuliwe hatua.
msema kweli: ...
Mwanakijiji nimesoma habari hapo juu na kuona kuwa serikali imekosa mwelekeo hasa katika maamuzi mengi mazito. Kama ulivyoainisha kuwa yamekuwa yakitoakea mangi juu ya taaluma ya uandishi wa habari na maadili yake kwa ujumla lakini serikali imekuwa ikikaa kimya. leo mwenyekiti wa MOAT ameguswa pabaya serikali yaangaza jicho lake. Je wanataka maadili yafuatwe kwa kuwa MENGI ameguswa pabaya? Ni watu wangapi tumewaona wakidhalilishwa katika vyombo vya habari wakiguswa mambo yao binafsi na Mengi kupitia MOAT hawakugusia au kwakuwa akina WEMA SEPETU, JOKETI na wengine wengi kama hao hatujaona wala kusikia serikali ikitaka kutoa maamuzi juu ya maadili ya uandishi wa habari
Kwanini baada ya kuandikwa kina Karamagi, Mengi, na "Waziri Mkuu wa zamani" imekuwa kana kwamba mbingu zimeguswa? Wanapoandikwa kina Nsia na vijana na mabinti wengi, watu wanapopigwa mapicha wakiwa wamelewa na kuwekwa magazetini, mtu anapopigwa picha kakaa vibaya na kufanywa kituko kwanini magazeti "yale" yanaendelea kuwepo.?
Yawezekana kuwa mkuki kwa nguruwe ni kweli mtamu...kwa binadamu ndiyo mchungu..?
l
Steve Dii
02-13-2009, 01:30 PM
Kuna msomaji wetu mmoja kauliza swali zuri sana na lenye mantiki kufuatia maagizo ya Waziri wa Habari Kapt. Mkuchika kutoa siku saba kwa magazeti matatu kuelezea kwanini wasichukuliwe hatua.
Kwanini baada ya kuandikwa kina Karamagi, Mengi, na "Waziri Mkuu wa zamani" imekuwa kana kwamba mbingu zimeguswa? Wanapoandikwa kina Nsia na vijana na mabinti wengi, watu wanapopigwa mapicha wakiwa wamelewa na kuwekwa magazetini, mtu anapopigwa picha kakaa vibaya na kufanywa kituko kwanini magazeti "yale" yanaendelea kuwepo.?
Yawezekana kuwa mkuki kwa nguruwe ni kweli mtamu...kwa binadamu ndiyo mchungu..?
l
Kiwango cha uchungu waupatao watu kwa kuandikwa kwenye magazeti kwa mambo yao ya ndani hakika ni wao tu wanaweza kuuelezea. Jamii yetu imeharibika kutokana na kuongezeka kwa wimbi la aina hii ya uandishi. Mambo ya ndani yataendelea kuandikwa na hata huko nchi zilizoendelea haya mambo yanaandikwa kwenye magazeti, ila wanaustaarab wao katika kuyaandika. Sisi naona tumerukia hii market segment bila ya mwongozo kuwepo. Wenzetu kuna sheria zinazowalinda walioandikwa, fine kubwa hutolewa kwa ma-victims pale wanaposhitaki, sisi sheria hizi wala hazieleweki. Ni pale tu wakubwa wanapoandikwa ndipo tunapoona viongozi wanakurupuka kuleta vitisho.
Tumeyaona pale Mwanahalisi lilipofungiwa kwa makosa ambayo magazeti mengine hayakufungiwa. Ni ukurupukaji katika ku-deal na situation ndiyo unaotuangusha sisi. You know sometimes what matters is not the problem (since is already with you) but how someone deals with that problem.
Sasa kama unavyosema, akina Jokate na ma-miss wengine kibao wameandikwa kwa kejeli na stori nyingi tu za kutungwa, viongozi wetu wamekuwa kimya muda wote huo, lakini leo hii wameamua kulivalia njuga na ku-single out some few tabloids. They should look at the root of all these na siyo juu juu kwa stori moja au mbili. Market ya udaku itaendelea kuwepo na iko nasi, kujifanya tunaizima ghafla kwa imla si suluhisho hata kidogo.
Walevi, picha za ajabu ajabu na mengine ya aibu wafanyayo binadamu yataendelea kuwepo kwani yalikuwepo; na kwa jinsi teknolojia inavyokua, basi yataendelea kunaswa na kuwekwa kama vielelezo. Challenge iliyopo ni ugumu wa kujua uwiano thabiti wa kuyaelezea mambo haya bila nia ya kuaibisha walionaswa na kati ya nia ya kuleta fundisho/adhabu kwa wahusika (walionaswa na walionasa).
Elimu, sheria/miongozo na matangazo kupinga aina ya uandishi huu na haja ya jamii kujitumbukiza ndani yake ya weza kuwa solution ya muda mrefu na yenye manufaa zaidi kuliko watu kufungwa na kufungiwa kwa magazeti pekee. Maana kawaida ya vitu ambavyo vinaongozwa na market demands ni kuwa - ukivizuia, hutafuta njia zake za mpenyo kujiendeleza. Na ikitokea hivyo ndipo suluhisho katika kutatua tatizo linalotukumba litakapokuwa gumu zaidi kulipata.
SteveD.
Mpita Njia
02-13-2009, 06:33 PM
Kuhusu sheria, Mkuu Steve sijui kama wengi (hasa walioko kwenye media) watakuelewa. Hiyo sheria iliyopo wanaipinga, wanataka uhuru zaidi. sasa hiy o reference ya wenzetu walivyo na sheria kali inaweza kuwafanya waanze kudhani kuwa unapendekeza na sheria zetu ziongezwe ukali pia-hautakuwa rafiki yao.
Tatizo linalojitokeza kwa mujibu wa maoni yangu ni kuwa hivi ni vita ambavyo media imejikuta ikitumika kama silaha bila ya yenyewe aidha kujua au kupenda. Haya ndiyo matokeo ya commercialisation ya media na kinachonisikitisha ni kuwa inazidi kumong'onyoa ile dhana kuwa media ni mhimili wa nne. I for one would not like to have a pillr which can be manipulated so easily by people who have power or money
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.