PDA

View Full Version : Unachukuliaje kuchwapa kwa walimu?



mwanakijiji
02-15-2009, 01:37 AM
Hivi kama DC anaagiza Polisi wakutie viboko mbele ya wanafunzi utakubali? Kwanini?

Mpita Njia
02-16-2009, 10:58 AM
Nitakubali tu kama ni sehemu ya adhabu ninayostahili kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria zilizopo na kama nitaridhika kuwa kweli nimetenda kosa nililoshtakiwa nalo

jatropha
02-16-2009, 12:57 PM
Hivi kama DC anaagiza Polisi wakutie viboko mbele ya wanafunzi utakubali? Kwanini?
Utaratibu huosafi sana kwamafisadi wa nchi hii.Inatakiwa Jakaya aige mfano huo siku moja katika kikao cha baraza laMawaziri afunge mlango na amuite Mwema atembeze viboko,wa kwanza kuchapwa awe Masha.Pia Spika aige mtindo huo kwa wabunge wasindikizaji wasiosema chochote bungen,wanaolala na wanaochelewa, Wa kuchapwa awe mbungw wa Jimbo la Ubungo Keenja kwa kutowatenbelea wananchi wake hata mara moja.

DC huyo anastahili kupatiwa uwaziri mkuu kwa kuonyesha kuthubutu kuondoa usugu a watumishi wasiowajibika

Mpita Njia
02-16-2009, 02:40 PM
Kwa hiyo jatropha wewe ungekubali kutiwa mboko mbele ya wanafunzi?

Angeris
02-16-2009, 09:35 PM
Nikijiweka nafasi ya mwalimu, sitakubali kuchapwa viboko tena siyo tu mbele ya watoto hata ofisini kwa DC.

Kama shule ina matatizo hiyo siyo jinsi ya kutatua matatizo. Sana sana unadhalilisha watu wazima tu kwa kujiona wewe ni mtendaji mzuri. Hata kama walimu wana makosa,DC angetafuta utaratibu mwingine wa kupambana nao ili akomboe maendeleo ya elimu huko wilayani mwake.

Yaani kabisa kula bakora,jamani sisi tuna vituko!

paulp
02-18-2009, 01:44 PM
adhabu ya viboko ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kinyume cha sheria. chombo chenye mamlaka ya utoaji wa adhabu na kutoa haki ni mahakama pekee. Nalaani kitendo cha mkuu wa wilaya kuwachapa viboko walimu

Mpita Njia
02-18-2009, 03:09 PM
Lakini wapo pia wanaodai kuwa walimu (hao)m walistahili kuchapwa kwa sababu hawajali wajibu wao

kurutamatata
02-18-2009, 04:19 PM
Mwalimu mtu mzima mwajiriwa na haki zake zote apigwe viboko mbele ya wanafunzi wake,huu sasa umekuwa utawala wa ki Nazi au vipi?Huyu DC ashukuru Mungu amefukuzwa kazi tu.Vinginevyo,ilikuwa afikishwe mbele ya vyombo vya sheria ashikishwe adabu! Hivi hapa nchini nafasi za MaDC nchini kote zimetengewa Wanajeshi tu?Na Wakuu wa Mikoa je,wako wanajeshi wangapi?This Tanzania's Strategic Economic Planning! "Put them in the Regions and Districts for conveniences sake,why not?"Wewe unajali maendeleo,maendeleo gani?Bora liende.

mwanakijiji
02-18-2009, 04:49 PM
Lakini wapo pia wanaodai kuwa walimu (hao)m walistahili kuchapwa kwa sababu hawajali wajibu wao

Mpita Njia, walimu wanaokubali kuchapwa viboko na mtu mwingine yeyote regardless ya reason hawastahili kuwa walimu!

dRU
02-18-2009, 05:40 PM
Hivi kama DC anaagiza Polisi wakutie viboko mbele ya wanafunzi utakubali? Kwanini?

Inaposemekana kwamba mtu anatumikia adhabu, basi wazi ujue kwamba hapo pana maumivu ya aina fulani ambayo mpewa adhabu atayasibu. Katika hili sakata la walimu, hivi viboko vilikuwa adhabu na hakika si waalimu tu ambao wameguswa na adhabu hii bali watu wengi hasa kwa jinsi swala zima lilivyochangiwa na wadau mbali mbali ikijumuika na Serikali kumtupa chini DC.

Mwanakijiji, hapa hakuna atakayekubali kwa sababu adhabu ni maumivu. Lakini sasa, na turudi nyuma, mimi ninasema ama kukubali adhabu hii ama kutokubali ingetemea sana na mazingira ya swala zima mpaka kufikia adhabu!!! :mad: Kuna awakati mtu akakubali adhabu ama tu kwa sababu mtoa adhabu kamzidi - ki madaraka, ki sheria ama kwa mabavu ama vingine kwa kukubali nusu ya shari.. maana Wapemba husema "ntu kugombana nkutaka" .. hivyo ay nini shari kamili!!!:D.
Mwanakijiji, nina hakika kwamba ndani ya sakata hili yapo ambayo wengi hatuja yapata vizuri maana si kawaida itokee mtu aje na askari Polisi na kuamrisha watu walale na kupigwa bakora nao watu hao wakawa "tayari" kupokea adhabu hiyo ambayo kwa namna yeyote ile haukiwa na (ya) busara.

Ilikuwaje mpaka DC akawasawishi, ama kuwaamuru watu (POLISI) ambao wangetegemewa kuwa washauri wazuri kisheria kwa DC na hata raia wengine... Unapotumia Polisi kutenda jambo basi ni lazima nao Polisi wamekiri kwamba kitendo wanachokifanya ni cha haki maana sidhani kama DC angewaamrisha waje na Bunduki kuwapiga risasi Waalimu hao kwa makosa hayo hayo basi Polisi wangefanya tu hivyo eti kutimiza amri (Mambo ya ZOMBE haya mhhhh!!!).

Lipo jambo ambalo litafichuka tu hapo mbeleni na tutapata kujua zaidi yote haya yalijiri kwa namna gani.. maana hukumu si kwa DC tuu kama ilivyotolewa na Serikali bali wanatakiwa wote ndani ya mtanange huu wapate haki zao.....

Sishabikii waalimu kupigwa bakora mbele ya wanafunzi na wala sishabikii DC kuachishwa kazi na hata Polisi wachapa viboko!!! :eek:

Steve Dii
02-19-2009, 05:57 AM
....sijui sheria na mizengwe mbalimbali inayoizunguka sheria kuhusiana na watu kuchapwa viboko hadharani!!

....nijuacho ni kwamba; bila viboko (sisi) tusingelikuwa na leli ya kati hivi sasa!!!

....you be the judge!!

Mpita Njia
02-19-2009, 10:43 AM
Mpita Njia, walimu wanaokubali kuchapwa viboko na mtu mwingine yeyote regardless ya reason hawastahili kuwa walimu!

hata mimi naamini hivyo. lakini kuna watu niliowasikia wakizungumza, hasa kutoka katika eneo hilohilo la tukio ambao wanaamini kuwa walimu hao walistahili viboko (nadhani wanamaanisha adhabu). kwa hiyo, hapa inatakiwa tuelewane mapema kuwa tunapozungumzia kuchapwa viboko ni kwa mantiki ya dhabu au tunazungumzia kitendo hicho cha kuchapwa. kwa sababu kama ni adhabu, walimu wasiotekeleza majukumu yao wanastahili adhabu, lakini kuchapwa kiboko si moja kati ya adhabu zilizoainishwa

Matigari
02-19-2009, 08:47 PM
Lakini wapo pia wanaodai kuwa walimu (hao)m walistahili kuchapwa kwa sababu hawajali wajibu wao



Hakuna mtu yeyote anayestahili kuchapwa hata kama kuna kosa lililofanyoika. Taratibu za ajira huwa zinaeleza aina za adhabu ya kupewa mtu endapo ataonekana hakutimiza wajibu wake. Halafu kutathmini kufanikiwa au kutofanikiwa kwa elimu ya shule ya msingi ni vigumu maana kuna wadau wengi wanaohusika. Kuna taasisi ya elimu ( yaani shule na ofisi ya elimu ya wilaya au mkoa, kuina wazazi kuna waalimu na wananci. Ni lazima tujiulize hao wengine walichangiaje katika jitihada za kuwasaidia hawa vijana wafaulu au waelewe wanachokisoma huko shuleni. Je walimu walikuwa na vifaa vya kutosha? Kama la, taasisi zinazohusika zilifanya nini? Je wazazi walichangiaje? Walifuatiliaje maendeleo ya wanafunzi, Je mama au baba alikuwa akimkimbusha kijana au binti kujisomea jioni na kumalizia homework? Wananchi kwa ujumla hawakujua kuwa vijana hawaelewi wanachofundishwa? Wananchi walifanya nini kutatua hilo? Walimshirikisha mbunge wao? Kuna maswali mengi maana kufeli mtihani hakuji mara moja dalili za kufeli au kupasi huwa zinaonekana toka mwanzo wa mwaka.

Wasalaam