mwanakijiji
11-10-2008, 07:00 AM
Bi. Aziza alitufundisha jinsi ya kupika kisamvu:
MAHITAJI
kisamvu kilichopondwa vizuri(kiasi waweza kadiria kama vikombe vinne vya chai)
-karanga za kusaga kiasi 3/4 ya kikombe cha chai,kama ni peanut butter tumia vijiko 4 vya chakula.(angalia isiwe nyingi)
-1-nyanya 4 kubwa.
-2-vitunguu maji,saumu.
-3-mafuta ya maji vjk 3vya chakula.
-4-tui la nazi kikombe kimoja cha chai.
-5-chumvi
-6-karoti,pilipili hoho(option).
UANDAAJI
1 Pika kisamvu chako mpaka kiive pamoja na vitunguu saumu vilivyopondwana chumvi ya kutosha(kama hukuchemsha na chumvi kitakuwa kichungu).
2 kisha tia karanga(zikoroge kwanza kwenye maji ya uvuguvugu)acha ziive.kama ni butter haihitaji kupikwa sana.
Vikisha kuwa tayari,
3 Kwenye sufuria safi na kavu kaanga vitunguu maji vilainike visifike brown.
4 weka nyanya koroga kiasi,usisubiri mpaka ziwe rojo,weka karoti na hoho(zikate staili unayopenda)kiasi sec 30.kisha tia mboga yako changaya vizuri tia tui lako la nazi,onja chumvi,pika mpaka liive.
Tayari kwa kuliwa Laughing