PDA

View Full Version : Kwanini Maharamia ya kisomali hayakamatwi?



Ditto
02-16-2009, 11:14 AM
Naskia huwa yanaivamia meli ikiwa katikati ya bahari..Je hizo meli haziwezi kuwa na vifaa maalum vya kuwaona tokea mbali na ikiwezekana wawashambulie kabla hawajaingia humo ndani?

Naskia pia huwa yakishaingia ndani wengine hubaki humo na wengine huwachukua mateka baadhi kuwapeleka nchi kavu mpaka hapo hela itakapo toka..baadae huwaachia mateka hao..Je kweli Marekani inavyojisifu kuwa na mashirika makubwa ya kijasusi wameshindwa kabisa kufuatilia nyendo zao mpaka kujua hasa ni akina nani hasa wanaohusika na shughuli hiyo?Mbona naona kama kuwafuatilia ni rahisi sana ukizingatia lazima wanataka kukabidhiwa hicho kitita kwa cash, kwaiyo lazima watamuona mmoja wapo wa wahusika akija kuzichukua..

Bado hainiingii akili kwamba dunia nzima imeshindwa kuwatuliza hao maharamia ya kisomali wakati inavyoonekana yanatumia mbinu za kizamani kabisa za utekaji nyara (Pirates style). Labda kama kuna mtu ana uwezo wa kuelewa kiundani kwanini hawa watu wanashindwa kukamatwa naomba anisaidie..

Mpita Njia
02-16-2009, 12:22 PM
Nimeangalia picha chake naona viboti wanavyotumia hao maharamia ni vidogo sana na ninashangaa wanaweza kuteka meli kubwa. Hivyo viboto vyao sidhani kama vinakuwa na makombora makubwa ya kuweza kutishia meli hizo wanazoziteka. Wanafanikiwaje?