PDA

View Full Version : Mpambano IPP na Mh. Masha!!??

dRU
02-17-2009, 06:36 PM
Wanakijiji, nimekanyofoa haka ka taarifa kwenye IPPMEDIA.
Ni hapa tuu kwenye mtanange wa maneno, ninanukuu

"Hata hivyo, baada ya shutuma na vitisho hivyo, Masha alibadilika na kuwataka waandishi wa habari wamuulize maswali mwandishi wa magazeti ya IPP aliinua mkono kwa nia ya kupinga suala hilo, lakini Masha akamzuia kwa kusema: ``Wewe wa IPP sitaki uulize kwa sababu sikukualika.``

Mwandishi alitii amri hiyo, lakini akamkumbusha Waziri huyo kuwa yeye (Masha) ndiye aliahidi kuwa angemuuliza mwandishi. Iweje sasa anageuka na kuwaambia waandishi wa habari ndio wamuulize (mwandishi wa magazeti ya IPP)?.

Hadi mkutano huo unakwisha Masha hakumruhusu mwandishi kutoka IPP kuuliza swali, badala yake aliwaruhusu waandishi wa habari kutoka vyombo vingine vya habari peke yake kufanya hivyo."

Mwisho wa kunukuu.

Hivi kweli kuna mambo ya maslahi ya nchi hapa ama ya ubinafsi??? Ninaomba kuelemishwa:mad:

Baija Bolobi
02-21-2009, 06:53 PM
Hakuna maslahi yoyote ila Masha anatumiwa na mafisadi kumdhoofisha Mengi.
JK anachelekelea kuwa acha masha afe mwenyewe maana anajua yaliyomkuta Masilingi.

mwanakijiji
02-21-2009, 09:33 PM
Hakuna maslahi yoyote ila Masha anatumiwa na mafisadi kumdhoofisha Mengi.
JK anachelekelea kuwa acha masha afe mwenyewe maana anajua yaliyomkuta Masilingi.

wakati mwingine naijiuliza kama tumepoteza utimamu wa akili zetu, au akilii zetu zimetupoteza sisi.

Baija Bolobi
02-21-2009, 09:37 PM
Mwana Kijiji, hatujarogwa na usaliti uliopindukia na kuzama katika medani za familia, kabila, dini na itikadi. Ebu niambie, hivi kweli mtu anayemficha mtu kama Liyumba unadhani anafanya kwa urafiki, au ushirika katika wizi wake? Ni wangapi humu kijijini wako tayari kuwaripoti ndugu zao mafisadi na kuwatolea ushahidi wa kuwazamisha. Ni nani yuko tayari kusimama kugombe ubunge akipingana na baba yake au kaka yake aliye fisadi? Namtaka na nitamuunga hata kama atakuwa kinyume na chama changu.

911
02-22-2009, 07:33 PM
Rushwa,ufisadi,'tamaa' na madudu mengine yanayoendana na hayo huwa na uwezo wa kupofusha si macho peke yake,bali pia akili na uwezo wa kufikiri na kuchanganua mambo.Thatz y huwa shishtuki sana mara nisikiapo kuwa wale wenye dhamana ya kulinda mali zetu wakituingiza katika mikataba isiyo na manufaa kabisa kwa taifa...Huwa muda mwingine najiuliza kuwa je watu hawa(wengi wao wakiwa ni 'wasomi'!) wanatumia ubongo wao au uti wa mgongo????

Mpita Njia
02-23-2009, 11:03 AM
Nadhani hata hii vita dhidi ya ufisadi nayo imetupofusha macho

dickabudi
02-23-2009, 11:39 AM
Nikionacho Mimi ni biasness ya magazeti ya IPP kwa Mh Masha, magazeti haya yamepotosha sana ukweli wa masuala ya Masha kwa kuona ana mvutano na Mwenye Mali

Angalia uandikaji wa habari wa Majira huwezi amini Marehemu Nyaulawa na Idd Simba ni wakurugenzi wa gazeti hili

Angalia Mwananchi ulikuwa huwezi jua kama Rostam ni Mkurugenzi lakini si vyombo hivi vya IPP, tuvikemee, tuwatake waandishi na wahariri wawe fair

Tuwe makini ama sivyo tutasujudia watu na sio fikra zenye kujenga

Mpita Njia
02-23-2009, 12:31 PM

Nakuunga mkono kuwa waandishi wanatakiwa kuwa fair. lakini marekebisho kidogo, Rostam si mkurugenzi wa Mwananchi, na wala si mwanahisa kwa sababu alishauza hisa zake zamani

Baija Bolobi
02-23-2009, 01:24 PM
Sasa angalia Rai na Mtanzania yanasemaje juu ya Rostam? Pamoja na kukuunga mkono juu ya upendeleo wa waandishi, nachelea kusema hakuna mwandishi awezaye kumwandika mwenye gazeti vibaya. Dawa ni kuwa na magezeti yanayomilikiwa na waandishi wenyewe. Ndiyo maana gazeti kama Raia Mwema linajitahidi hata kama lina chuki na serikali iliyopita.

Mpita Njia
02-23-2009, 02:18 PM

Mkuu, hakuna mtu anaweza kuukata mkono unaomlisha, I think this is natural. Hata hilo rais Mwema sidhani kama linaweza kumwandika vibaya Jenerali Ulimwengu

dickabudi
02-23-2009, 02:20 PM
Mpita Njia nakubali kuwa kwa sasa Rostam si mwanahisa wala Mkurugenzi Mwananchi lakini uliona reporting yao hata siku za nyuma akiwa mwanahisa na mkurugenzi hazikumlinda wla kumnadi kwa wabaya wake

Hata saga la Mtikila na Rostam umeona Mtanzania wasivyolalia upande mmoja

Hata leo umesikia Mhariri wa Mtanzania akizungumza Channel Ten na kuisifia CUF hata kama mwenye mali ni mwana CCM?

Mpita Njia
02-23-2009, 02:55 PM

Ni kweli, lakini hata huyo mhariri wa mtanzania, sidhani kama anaweza kumlima Rostam. hata hao mwananchi, lazima kuna mtu ambaye hawawezi kumwandika vibaya, ni kawaida tu. lakini katika mazingira kama hayo, nadhani ni vema kuamua kunyamaza kimya inapotokea habari inamhusu bosi wako kuliko kuonyesha kuwa unaegemea upande fulani kama wanavyofanya IPP

mwanakijiji
02-23-2009, 05:22 PM
Unajua ndiyo maana mara nyingi kwa wenzetu huku wanapoandika au kutaarifu jambo lolote ambalo linahusu mmiliko wao au mahusiano basi wanafanya kile kinachoitwa "full disclosure". Manake ni kuwa IPP wakiandika kuhusu Mengi katika shughuli za Mazingira ni muhimu waongeze kuwa 'Bw. Mengi ni mmiliki wa makampuni ya IPP wachapashaji wa magazetei ya Nipashe".

Hii full disclosure ni muhimu sana katika kulifanya gazeti au chombo cha habari kuwa huru.

Baija Bolobi
02-23-2009, 07:17 PM
Uzuri wa Jenerali Ulimwengu, yeye mwenyewe ni mmoja wa waandishi wa gazeti hilo. Kwa hiyo hata wewe unajua kuwa hiyo haiwezekani. Tatizo ni hawa wanaoanzisha magazeti kwa kificho hawataki hata kujulikana wazi, lakini wanawashinikiza wahariri kuandika wanayotaka wao. Kijiji chetu hiki ni mfano hasa pale watu wanapoamua kumrudi mwana kijiji na yeye asifanye lolote juu yao. Ukweli tuuseme, Jenerali amejijengea jina hata kama ni Mnyamulenge.

ponda
02-24-2009, 10:06 AM
Nadhani hata hii vita dhidi ya ufisadi nayo imetupofusha macho

itafikia mahali mtu anakosana na mpenzi wake ala lawama wanatupiwa hao mafisadi, tehee teheee

dickabudi
02-24-2009, 11:58 AM
Jadili

Mengi na Lowassa hadi Marehemu Dr. Omary Ally Juma akaingilia kati
Mengi na Wakurugenzi wa Habari Corporation(Jenerali, Dr. Shoo, Salva Rweyemamu, Marehemu John Rutayisingwa, Mbwambo Johnson)
Mengi na Manji
Mengi na WanaYanga
Mengi na Masilingi ni kweli kutokuwepo kwake kwenye Baraza la Mawaziri ni kwa sababu aligombana na Mengi??
Mengi na Masha
Mengi na TBC
Mengi na Malima (Mtoto wa Kighoma Malima) baadae Adam Malima na Samwel Sitta, pia jadili uteuzi wa JK kwa Adam Malima, uone kama tofauti ya Kiongozi yeyote na Mengi ndiyo kaburi lake kisiasa?

Actual Environment ndani ya IPP yaani mahusiano ndani ya kampuni ni ya kidemokrasia au kumsujudia mwenye nacho?

Engagement criteria ni transparency and fairness

Masha anaposema hakuwaalika wanahabari IPP ni kwa sababu ni fisadi au ni kwasababu ya wao kuonekana wamelalia upande mmoja????