dRU
02-18-2009, 11:38 AM
Wajameni, nimeifumua hii article kwenye mtandao wa eThinkTankTz na nikaona vyema niileta kijijini tuweze changia mawazo..... haya tena wanakijiji shime shime hoja hii hapa :-
Dear Mzalendo,
Kwanza pole sana kwa kuzinduka saa hizi. Kama kufa wengi tulikufa na kufufuka tayari. Mbona tangu enzi za Mwalimu taaluma ilikufa ikabaki siasa? Kwani hujui? Mfano, pita mikoa na wilaya zote utakuta vigingi vya saraji - miradi iliyo anzishwa kisiasa mpaka leo imekwama? Uliza kwanini wana-taaluma wengi mpaka leo wanakimbilia siasa? Mzee Sarungi (samahani kama utaudhika mzee au ndugu ndio mifano hai)anazeeka na ubinngwa wake wa mifupa wakati angekuwa anaendesha taasisi yake ya "Mifupa", Prof. Kapuya anatija gani katika taifa ukilinganisha na "taaluma" yake maskini. Nasikia ni mkemia wa kutupa! Mifano mingi ndugu yangu! Mpaka leo hatuna kiwanda cha sindano ya kushonea viraka, nashukuru MITUMBA imeficha hilo, bei poa hunahaja ya kushona viraka! Wenyetu tunaowakimbilia na kuwahusudu kama Wachina, Wahindi (India & Pakistani), Malasia, Singapura, Vietinamu na wengine wanaendelezwa na wana"Taaluma" wake na sio wanasiasa. Wanasiasa wananafasi zao na wana taaluma
zao. Jiulize mfano wa karibuni, wapi suluhu ya msongamano wa magari Dar! Rafiki yangu Edward aliongoza jahazi bila kuwaachia wanamipango miji na wachumi wafanye kazi zao- kikowapi sasa? Matokeo yake wanataaluma wanajikuta hawathaminiwi wanakimbilia kwenye ufisadi! Sio kosa lao! TUFANYE NINI KUNUSURU Taifa letu na huu uozo? Wazo ni kwanza tuwe na - Mdahalo wa Kitaifa wa Wanataaluma. Nadhani tutafika kwenye mwanzo na kuanza kuirudisha treni kwenye reli. Hapo tutafahamiana wenye PhD na Diploma bandia na kila mtu arudi kazini! Tutaacha kushangilia vita kati ya "wakulima" na "wafugaji". Nia aibu jamani!
Munyampaa!
Ahungu, R.A Chairman & ED
Advancement for Small & Micro-Enterprises Development in Tanzania (ASMET)
SLP 41005,Tel::+ 255-022-2807082 Cell::+255-78436003 4
Dar es SalaamTanzania