PDA

View Full Version : Natamani tanzania tungekuwa kama china!



a2faces
02-19-2009, 04:19 PM
Sitamani CHINA kwa kila kitu lakini natamani sana TANZANIA tungekuwa na utawala wa KIZALENDO hususani katika suala la kushugulikia UFISADI NA RUSHWA.

Inasikitisha sana kuona kuwa kuna matukio mengi sana yaliyotokea na yanayoendelea kutokea(kwa kufichuliwa) ambayo yanahusisha UFISADI NA RUSHWA iliyokithiri lakini hayajashughuliwa kwa UZITO HASAA UNAOSTAHILI, Ni kama vile UFISADI NA RUSHWA ni vitu vya kawaida mno ambavyo havina athari yeyote kwa TAIFA NA WANANCHI wa TANZANIA.

Hivi sijui lifanyike jambo gani hasa ili serikali na viongozi washituke na kusikia UCHUNGU kuwa TAIFA NA WATANZANIA wanadhalilika, kuumia, na kufa? au mpaka kutokee vurugu, migomo, uasi, majaribio ya kupindua inchi au vita ndiyo watajua kuwa sasa mambo ni mabaya?

Kwa tafsiri yangu mimi, MAFISADI NA WALA RUSHWA ni sawa na WAUAJI WA KUKUSUDIA, maana wako radhi kusaliti maisha ya WATANZANIA(ambayo kwao hayana thamani yoyote) kwa ajili ya maslahi yao binafsi na ya jamaa zao wachache wakati WATANZANIA walio wengi WANAPOTEZA maisha yao kwa kujinyonga kutokana na matatizo na maisha magumu, mahospitali hayana huduma na madawa ya kutosha hivyo kupelekea vifo vingi tu vya wagonjwa, wanawake waja wazito na watoto pengine kwa matatizo ambayo yanaepukika kama pesa zile walizochukua MAFISADI zingewafikia WANANCHI WATANZANIA MASIKINI, watoto wa mtaani wanaongezeka kutokana na ugumu wa malezi ya nyumbani kwao, madada zetu wanalazimika kufanya ukahaba wakati mwingine kwa hata MIA TANO TU(500/=) ili angalau wapate mlo mmoja wa siku lakini hatimaye wanaambukizwa magonjwa na UKIMWI, watoto wetu hawana shule nzuri za kusomea, vijiji havina huduma za msingi kama umeme na maji, wakulima wetu wanazaliwa hadi kufa wakilima kwa jembe la mkono tu,barabara zetu mbovu..........yaani matatizo chungu nzima ambayo yote hayo yanapelekea maisha ya WATANZANIA kuwa ya tabu na dhiki siku hadi siku, vifo juu ya vifo.

NCHI ya CHINA ni mfano mzuri sana kwa kujali na kuthamini raia wake hasa linapokuja suala la UFISADI au RUSHWA ambayo kwa tafsiri yangu hapo juu ni MAUAJI, hawana mchezo hata kidogo. Na huo ndiyo utawala wa mfano ambao natamani TANZANIA tungekuwa nao.

Hivi niulize WAHESHIWA, nchi hii haina WENYEWE? au nchi hii haina BABA WALA MAMA? Mbona kila mtu anafanya anavyotaka tuu na serikali inaangalia!? Hivi siku WATANZANIA wenye uchungu watakapochukua nchi yao kuna kitu ambacho mnaweza kuwaeleza kweli wakawaelewa? hivi mnaweza kuwafanyia nini WATANZANIA kufidia madhila na machungu ambayo wanayapata? mnaweza kweli kufidia vifo vinavyoweza kudhibitika ambavyo sasa hivi vinatokea kwa sababu ya UFISADI NA RUSHWA HII AMBAYO INAFUMBIWA MACHO MAKUSUDI?

Hivi kweli FISADI anayetuhumiwa kuiba sh.bilioni 250 anaweza kupewa dhamana kwa sh.milioni 800? tena kwa hati za dhamana za kuku,mbuzi na kondoo?

Hivi kweli MAFISADI wanaotuhumiwa kwa kutuingiza mkenge kwenye mikataba ya RADA walitakiwa mpaka leo wawe huru tu wanakula wali kwa kuku na kushushia na bia? hivi zile pesa zingekuwa zimewafikia wananchi wenyewe ni maisha mangapi yangekuwa yameokolewa?

Jamani hivi EPA,IPTL, RICHMOND, N.K, N.K, N.K ni mchezo wa kuigiza au ni kitu gani?

Hivi mnategemea tutawapa kweli KURA zetu 2010 kwa haya mnayotutendea?

Kwa suala la kupambana na ufisadi, natamani TANZANIA ingekuwa kama CHINA lakini mlio juu kumbukeni kuwa KILA LILILO NA MWANZO LINA MWISHO TU.....!!!

Mpita Njia
02-19-2009, 06:03 PM
Hivi mnategemea tutawapa kweli KURA zetu 2010 kwa haya mnayotutendea?


Hapo mkuu 2faces hauna uchaguzi, lazima watapata tu.... usipowachagua wewe, nitawachagua mimi, nisipowachagua mimi, utawachagua wewe, na tusipowacgaua mimi na wewe, watajichagua wenyewe