PDA

View Full Version : Liyumba akamatwa?

mwanakijiji
02-20-2009, 09:56 AM
Habari zinadokeza huyu jamaa atakuwa ametiwa mbaroni usiku wa kuamkia leo na atafikishwa mahakamani... tunasubiri kuzithibitisha. Hakuwa mbali na jiji la Dar ...

Mpita Njia
02-20-2009, 10:53 AM
Alikuwa wapi, Bagamoyo?

Mwipagi
02-20-2009, 10:59 AM
kama watamkamata itakuwa nafuu,make mambo yenyewe kwa sasa yanapelekwa kijotijoti,kila siku hawaishi kutuzuga,au walikuwa wanatest response ya Wadanganyika itakuwaje?

Mwipagi
02-20-2009, 11:06 AM
Alikuwa wapi, Bagamoyo?

Pengine kwa mmoja kati ya Vimwana anaowamiliki,jamaa wamemkurupua nini,ngoja tusubiri habari kamili kama MMM alivyoahidi.

Atubonekisye Massapa
02-20-2009, 11:29 AM
Sasa MMM, unaweza dokeza kama jamaa kwanini 1) walimpa dhamana katika mazingira ya kutatanisha, halafu 2) wameshituka nini hata kuanza kumsaka kama nyoka?

Mpita Njia
02-20-2009, 11:58 AM
Sasa MMM, unaweza dokeza kama jamaa kwanini ...2) wameshituka nini hata kuanza kumsaka kama nyoka?

Nadhani baada ya faili kuitishwa mahakama kuu, hakimu akajishtukia kuwa dili alilokula litabumburuka ndio maana akaamua kujihadhari kabla hatari haijamkuta

The Great Cardinal
02-20-2009, 12:41 PM
Hujapata nyongeza ya liumba?

The Great Cardinal
02-20-2009, 04:00 PM
Nafikiri tuwasaidie hawa jamaa takukuru kwa kuwapa list ya hao mademu ambao mnawajua kuwa huenda ikawa amejificha. Ingawa wao ndio walichemsha kwa kumuachia kabla hajatimiza masharti.

Mpita Njia
02-20-2009, 05:16 PM
Habari kutoka Kisutu zinaeleza kuwa Liumba bado hajapatikana lakini hakimu amefuta arrest warrant ya wadhamini wake. {ia ameiahirisha kesi hiyo hadi tarehe aliyoipangia awali-feb 24

mwanakijiji
02-20-2009, 05:38 PM
basi nadhani ndiyo imetoka hiyo kwani jana majira ya saa nne za usiku kulikuwa na habari kuwa huyu jamaa amekuwa cornered sehemu sehemu.. which reminds me kesi ya wale waliotuhumiwa kubeba mabilioni ya mishahara na kujikuta wameweza kupenyeza rupia hadi kwa maafisa wa Polisi.. we will see.. what is happening.

Mpita Njia
02-20-2009, 05:52 PM

Walivamia hapo mahali lakini hawakumkuta

mwanakijiji
02-20-2009, 11:54 PM
Walivamia hapo mahali lakini hawakumkuta

Inawezekana hilo ni kweli, lakini pia inawezekana (nahofia hili la pili) walimkuta na wamemchukua na kumficha kusikojulikana baada ya kuona jaribio lake hilo. Kwa vile hawawezi kumshikilia wakati wamempa dhamana wanasubiri hadi Jumanne ijayo ambapo watamleta Mahakamani, na dhamana yake kufutwa rasmi.

Mpita Njia
02-21-2009, 05:58 PM

Lakini mahakama ina uhuru wa kumfutia dhamana, kwa nini haikufanya hilo? Kinachoshangaza ni kuwa hakimu ametoa arrest warrant na hataki kueleza kwa nini ameiotoa. Kama wanamtafuta, kwa nini wamfiche iwapo wamemkamata?

mwanakijiji
02-21-2009, 09:29 PM
Lakini mahakama ina uhuru wa kumfutia dhamana, kwa nini haikufanya hilo? Kinachoshangaza ni kuwa hakimu ametoa arrest warrant na hataki kueleza kwa nini ameiotoa. Kama wanamtafuta, kwa nini wamfiche iwapo wamemkamata?

hapa kuna kitu hakiko sahihi... kuna kampeni ya makusudi ya misinformation. Ngoja tusubiri kidogo kuna kitu hakiko sawasawa.

911
02-24-2009, 10:12 AM
Kuna taarifa zinasema kuwa tayari A.Liumba amekwishafika Kisutu leo asubuhi majira ya saa nne kasoro.Chanzo kimoja(some blog) kikisema kuwa amefika bila escort yeyote(pccb or police) isipokuwa familia yake tu.Na kwa upande wake Radio One wametangaza kuwa ameletwa na escort ya pccb.Now which is which??