mwanakijiji
02-23-2009, 05:23 PM
Nguvu za Dowans zaibuka upya
2009-02-23 10:01:37
Na Muhibu Said
Kuna kila dalili kwamba nguvu za kampuni ya Dowans iliyorithi mkataba wa Richmond bado zinasumbua na sasa kamati mbili za Bunge ya Nishati na Madini na ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma zinagongana kutokana suala la mitambo ya kampuni hiyo.
Kutokana na uzuri, uimara au upya wa mitambo hiyo, Shirika la Umeme nchini (Tanesco) bado inaililia na inataka kuinunua licha ya maamuzi ya kuachana nayo kutolewa na serikali zaidi ya miezi mitatu sasa.
Hali hii imejitokeza siku mbili tu baada yaTanesco kuibua tena nia yake ya kutaka kuinunua mitambo hiyo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
Wakati Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma ikitaka mwafaka utafutwe kwa kukutanisha wadau wote kwenye suala la ama kununua au la, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imesisitiza msimamo wake wa kupinga ununuzi huo kwa kuwa ni kinyume cha taratibu.
Akizungumza na Nipashe jana, Mwenyekiti wa Kamati Nishati na Madini, William Shellukindo, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), alisema mwenye maamuzi ya kununua mitambo hiyo ni serikali kama imeona kuna dharura ya kufanya hivyo.
Hata hivyo, alisema taratibu zilizopo zinataka suala hilo lifikishwe kwanza bungeni ili likajadiliwe na kupata baraka za Bunge.
``Kuna taratibu za kufuata. Anayetakiwa kununua ni serikali kama imeona kuna dharura. Lakini ilete kwanza hoja hiyo bungeni ili ijadiliwe na Bunge,`` alisema Shellukindo.
Alisema ipo pia sheria ya manunuzi inayozuia kununua mitambo chakavu kwa vile hatua hiyo ni ya hatari.
Kutokana na hali hiyo, alisema haoni kuwa ni busara kung?ang?ania kutaka kununua mitambo ya Dowans kabla taratibu zinazohusika hazijafuatwa na kwa kuzingatia pia kwamba, mitambo ya kampuni hiyo haijulikani ilitumika kwa muda gani.
``Tanesco wanadai kuwa Dowans wanalo jenereta jipya. Lakini mitambo yao iliingizwa nchini mwaka 2006 na utekelezaji ulianza Desemba 2007. Sasa hilo jenereta linaweza kuwa jipya? Na hata yale (majenereta) mengine hatujui kama ni mapya,`` alisema.
Alisema inashangaza kuona Tanesco iking`ang`ania kutaka kununua, huku mkononi mwake ikiwa na amri ya mahakama iliyoomba kuzuia kuuzwa kwa mitambo ya Dowans kwa vile inaidai kampuni hiyo.
``Hatuna uhakika Tanesco wanaidai nini Dowans, hilo haliko wazi, tunataka tujue kwanza hilo. Hata hivyo, kama hilo lipo basi si wangekubaliana wabadilishane badala ya kununua,`` alisema Shellukindo.
Kauli hiyo ya Shellukindo imetolewa siku moja baada ya vyombo vya habari jana kuripoti kwamba juzi Tanesco ilifikisha upya dhamira yao katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).
Tanesco iliifikisha dhamira yake hiyo kwenye kamati hiyo miezi miwili baada ya Kamati ya Nishati na Madini inayoongozwa na Shellukindo, kupinga suala hilo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Desemba mwaka jana.
Akizungumza na Nipashe jana, Zitto alisema katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, Tanesco walitoa hoja za msingi kuhusu dhamira yake ya kutaka kununua mitambo ya Dowans.
Hata hivyo, alisema waliafikiana wamuombe Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuruhusu kuitisha kikao cha kamati zote mbili (ya Hesabu za Mashirika ya Umma na Nishati na Madini), serikali, Tanesco na Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ili wajadili na kufikia mwafaka wa pamoja kuhusu suala la kununua mitambo hiyo ili kuepuka kamati kupingana.
Zitto alisema sababu nyingine ya kamati yake kuomba kibali hicho kwa Spika ni kwa vile Kamati ya Nishati na Madini, haikutoa nafasi ya kukutana na Tanesco ili waeleze kwanini wanataka kununua mitambo hiyo.
``Walikutana tu na Waziri Ngeleja wakapinga Tanesco kununua mtambo huo wa Dowans,`` alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Alisema pia, watatumia fursa ya ruhusu hiyo Spika kujadili kuhusu hatma ya umeme wenye megawati 300 wa Mtwara baada Kampuni ya Barrick kujitoa na hatma ya umeme wa upepo wa Singida.
Alisema kamati yake ilikutana na Tanesco juzi kwa lengo la kukagua hesabu za shirika hilo baada ya kuonekana wanatumia gharama kubwa kulipia umeme na hoja ya kutaka kununua mtambo wa Dowans iliibuka katika kikao hicho.
Hata hivyo, Zitto alisisitiza kwa kusema kuwa: ``Kazi ya Kamati ya Bunge ni ku-oversight (kusimamia) na siyo utendaji wa serikali wa kila siku, kwamba serikali inunue au isinunue.``
Dowans ni mrithi wa kampuni ya Richmond Development Corporation, Kampuni iliyopewa mkataba na serikali wa kuzalisha umeme wa dharura wa megawati 100, lakini ilishindwa na baadaye iligundulika ilikuwa kampuni feki.
Sakata la mkataba wa Richmond ndio ulisababisha kujiuzuku kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, mawaziri Dk Ibrahim Msabaha na Naziri Karamagi. Kutokana na kujiuzulu kwa Lowassa, Baraza lote la Mawaziri lilivunjika Februari mwaka jana.
Tangu wakati huo, kutokana na ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa makataba wa Richmond na maazimio ya Bunge, matukio kadhaa yametokea ikiwa ni pamoja na kumfikisha mmiliki wa Richmond mahakamani.
Aidha viongozi wengine wanachunguzwa na vyombo vya dola juu ya ushiriki wao kwenye mkataba huo.
SOURCE: Nipashe
My Take:
Hili la Dowans lina ugumu gani, kama wanaona bado wanataka kulipwa kwanini tusiamue kununua tu hiyo mitambo yaishe kuliko kuzungushana kama pia?