PDA

View Full Version : Mawazo ya Baba wa Taifa kwa wapinzani kuwa na viti vingi kwanza Bungeni

dickabudi
02-23-2009, 11:16 AM
Mwanakijiji nina ombi moja zuri tu, baada ya kuona na kusikia sasa waliokuwa na hamu ya kugombea Urais wanarudi kwenye majimbo na kutaka kugombea ubunge naamini ni kutekeleza ushauri wa Marehemu Baba Wa Taifa aliowapa enzi za uhai wake na kweli na kwa nia njema tuwahimize hawa 'impatient childs' kwa manufaa ya taifa letu

Wamejifunza ,wameona kwa vitendo na sasa wanatakiwa kuhakikisha idadi ya wabunge wa upinzani inaongezeka Bungeni kwanza kabla ya kufikiria kushika dola

mwanakijiji
02-23-2009, 06:10 PM

Hilo ndilo gumu kweli... najaribu kuona ni jinsi gani tutaweza kuwasaidia hawa..

Baija Bolobi
02-23-2009, 08:30 PM
Hili ni gumu kweli lakini ni jema pia. Tatizo ninaloliona ni kama hatatokea kabisa wa kugombea urais na kuiacha CCm iwe na mgombea pekee au mgombea msanii. Of course watatokea kina Mtikila na kujaza fomu. Njia ya kuwasaidia ni kuhakikisha kijiji kinahamia katika majimbo yenye wabunge wa CCM vimbelembele na wanaoota kurudi katika chama kimoja.

mwanakijiji
02-23-2009, 11:01 PM

binafsi naamini hili linawezekana lakini kitu cha kwanza nilazime wapinzani wawe hatua 10 mbele ya CCM. Sasa hivi bado CCM wako mbele kwa hatua nyingi tu..

dickabudi
02-24-2009, 10:52 AM
Yupo anaweza kubaki kugombea Urais na wazi ni Prof Lipumba, lakini walobaki ambao wamewahi kuwa wabunge na wakaonyesha kupendwa na kuwakilisha vyema ni vyema warudi majimboni wasaidie upinzani kuongeza viti Bungeni na Prof amsindikize JK ili 2015 tuone upepo unasemaje

Taratibu tutafika si unaona Israel , sasa kushika dola si kitu cha ajabu wote wana uwakilishi mzuri Bungeni na wanaringa, kwao Uwaziri Mkuu na madaraka mengine serikalini siyo tija, kuwajibishana ni kama kawa hata Rais akikiuka maadili anaondoka, taratibu tutafika, tuepuke unafiki kama jirani zetu, uwakilishi, ubunge ni wa hati miliki, tusifike huko.

Pia tuwashukuru wazee waliona mbali kama Mzee Mtei, Bob Makani ambao kwao uongozi umekuwa ni mbio za kupokezana vijiti tuwashauri na kina John Cheyo, Maalim Seif na Mh Lyatonga nao wawape kijiti wengine

Haiwezekani kwamba hakuna mpemba mwingine anyeweza kuwa Katibu Mkuu CUF, maana Wenyeviti CUF wamebadilika mara kwa mara hapo kwa Katibu Mkuu kunaniii???