View Full Version : News Alert:Liyumba atinga kizimbani, arudishwa rumande..(progressing)
mwanakijiji
02-24-2009, 03:43 PM
Mshtakiwa wa makosa ya kulisababishia taifa hasara yamabilioni ya shilingi katika ujenzi wenye utata wa Minara Pacha ya Benki Kuu Bw. Amatus Liyumba amefikshwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar-es-Salaama na maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)baada ya siku kadhaa kuzungukwa na utata ni wapi alipo.
Wiki iliyopita kulitolewa hati na mahakama hiyo kwa Bw. Liyumba kutokea mahakamani lakini hakutokea na hivyo uvumi kuwa ametoroka ulianza kuenea kwa kasi. Sasa hivi mahakama imekataa baadhi ya vitu vilivyotolewa mwanzoni ikiwemo pasi ya kusafiria kuwa havitoshelezi masharti ya dhamana na hivyo Liyumba amerudishwa rumande akisubiri kukamilisha masharti yote ya dhamana.
Baija Bolobi
02-24-2009, 04:01 PM
Hii ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Wasanii kwelikweli. kwa kuwa ameonyesha kuwa anapata shida kukaa lupango, sasa tuna mashaka kama hata kulala huko analala. Isije kuwa ni ile tuliyosikia ya marehemu Ditto ya kutoka usiku na kurudi asubuhi.
Spika akisema, tunadai anakosea. Jamani huu uhuni wa mahakama umezidi mno.
asauln
02-24-2009, 04:35 PM
Tatizo la mahakama zetu mizizi yake ni mirefu sana, wasio na hela ndio wanaoumia. Mwenzie Kweka habari zake unazisikia kwani?
mwanakijiji
02-24-2009, 05:02 PM
mimi sielewi hivi hili lilikuwa ni kutingisha kiberiti au nini? maana mambo mengine kwa kweli haya akili kabisa!
Baija Bolobi
02-24-2009, 05:08 PM
Hapo kuna scenario nyingi: Kutayarisha hati za dhamana, kushughulikia au kuharibu nyaraka, kuonana na wakubwa ili kuandaa spinning, kuwaona waganga wa kienyeji- lakini zaidi, kupata matibabu kwa sababu tunajua wote kuwa anaishi kwa matumaini, sasa kwa siku alizokaa keko alivuruga formula akahatarisha maisha yake.
mwanakijiji
02-24-2009, 05:48 PM
Hapo kuna scenario nyingi: Kutayarisha hati za dhamana, kushughulikia au kuharibu nyaraka, kuonana na wakubwa ili kuandaa spinning, kuwaona waganga wa kienyeji- lakini zaidi, kupata matibabu kwa sababu tunajua wote kuwa anaishi kwa matumaini, sasa kwa siku alizokaa keko alivuruga formula akahatarisha maisha yake.
sasa kwanini waseme kuwa wanamtafuta halafu waahidi na kutoa na donge nono?
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.