View Full Version : News Alert: Jaji Kiongozi mpya
mwanakijiji
02-24-2009, 10:31 PM
Rais Kikwete amemteua Jaji Fakihi Jandu kutoka Mahakama Kuu Iringa kuwa Jaji Kiongozi mpya kuchukua nafasi ya Jaji Salum Massati ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa.
Jaji Jandu alikuwa Wakili wa kujitegemea kama mwaka mmoja uliopita hadi alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na sasa kuwa Jaji kiongozi.
Baija Bolobi
02-24-2009, 10:53 PM
Laiti ningekuwa najua kuchora cartoon, ningechora picha ya Bajaji ikiwa inavuta Lori la tani 10 lililokwama katika matope mazito. Yaani Jaji Jandu ni Bajaji (Uzoefu mdogo na muda mfupi kwenye benchi) na Lori la tani kumi ni Mahakama ya Tanzania (Mhimili uliokwama katikati ya rushwa, ucheleweshaji haki, kunata kwa wanasheria, bajeti ndogo, kuingiliwa na wanasiasa).
Lakini ukiona Jandu kapita, ujue na Masati yuko njiani kuukwaa Ujaji Mkuu mwisho wa mwaka. Wenyewe huko mahakamani wanasema siku hizi kinachotazamwa katika uteuzi wa majaji ni mtu anasali wapi na kama ana sauti nyeroro au nzito!?
Mpita Njia
02-25-2009, 12:26 PM
Mimi binafsi simfahamu jaji Jundu kwa undani, kama kuna mtu ana profile yake tafadhali aitundike hapa nipate kumjua kidogo
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.