View Full Version : Mafisadi na Ukabila
Baija Bolobi
02-25-2009, 12:17 AM
Mafisadi wameripotiwa kuhoji imekuwaje wakuu wa vyombo vya kipelelezi wote watoke usukumani, yaani Hosea (TAKUKURU), Feleshi (DPP) na Manumba (DCI).
Wanajisumbua kwani hawajui aliyewateua ni mtani wao?
Wanashangaa kwa nini Chenge hajapelekwa Kisutu? Hata mimi nashangaa, nadhani hata Chenge mwenyewe anashangaa. Wakuu wenyewe hawashangai lakini macho yanaanza kuwashangaa na kudhani kuwa Zimwi likujualo?
Mpita Njia
02-25-2009, 12:00 PM
Wanataka kumaanisha kuwa kuna uukabila kwenye suala hili?
mwanakijiji
02-25-2009, 04:43 PM
Mafisadi wameripotiwa kuhoji imekuwaje wakuu wa vyombo vya kipelelezi wote watoke usukumani, yaani Hosea (TAKUKURU), Feleshi (DPP) na Manumba (DCI).
Wanajisumbua kwani hawajui aliyewateua ni mtani wao?
Wanashangaa kwa nini Chenge hajapelekwa Kisutu? Hata mimi nashangaa, nadhani hata Chenge mwenyewe anashangaa. Wakuu wenyewe hawashangai lakini macho yanaanza kuwashangaa na kudhani kuwa Zimwi likujualo?
Baija, ina maana hawa jamaa wanashindwa kumchukulia hatua Chenge kwa sababu ni mwenzao? Nadhani hilo litakuwa ni jambo la kushangaza, labda hawana ushahidi wa kutosha. Kwani hadi hivi sasa hakuna Msukuma kati ya wote waliokwishafikishwa mahakamani? Sidhani kama hilo ni jambo kubwa isipokuwa kama ushahidi haupo..
Mpita Njia
02-25-2009, 05:37 PM

Nadhani inaweza kuwa 'mwenzao' si kwa maana ya usukuma, bali kuna kingine kinawaunganisha
Baija Bolobi
02-25-2009, 07:40 PM
Nimesema kuwa mafisadi ndivyo wanavyodai hasa wale ambao wameishalala Keko. Ukiwauliza wakuu wenyewe wa vyombo wanasema hawapata ushahidi wa kutosha. Lakini bajameni, ukiangalia hata huo wa rada mbona inatosha angalau kucharge "matumizi mabaya ya madaraka" ambayo ina uwanja mpana!?
mwanakijiji
02-26-2009, 12:20 AM
Nimesema kuwa mafisadi ndivyo wanavyodai hasa wale ambao wameishalala Keko. Ukiwauliza wakuu wenyewe wa vyombo wanasema hawapata ushahidi wa kutosha. Lakini bajameni, ukiangalia hata huo wa rada mbona inatosha angalau kucharge "matumizi mabaya ya madaraka" ambayo ina uwanja mpana!?
Baija, mimi nadhani kwa Manumba sidhani kama inahusiana sana nahawa wawili DPP na Chenge. Nasikia kuna undugu wa aina fulani hivi, sasa kwangu mimi ningeona DPP ajitoe kumchunguza Chenge..
Baija Bolobi
02-26-2009, 12:39 PM
Baija, mimi nadhani kwa Manumba sidhani kama inahusiana sana nahawa wawili DPP na Chenge. Nasikia kuna undugu wa aina fulani hivi, sasa kwangu mimi ningeona DPP ajitoe kumchunguza Chenge..
Kwa nini tusilipigie kelele hilo? Maana kwa kadri linavyokaa muda mrefu, wanazidi kulitungia spin.
Ukiangalia ripoti ya SFO utaona walivyokuwa wameishamkona Chenge kwa kuangalia alivyokuwa akitoa majibu tata na tofauti kwa swali lile lile - oh mara vijisenti ni vya familia, mara ni malipo ya huduma ya kisheria, mara si zangu ni za mama! Typical wizi wa kitanzania.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.